Ni mechanism gani iko ndani ya risasi (bullet) kiasi cha kuua kwa kasi?

Ni mechanism gani iko ndani ya risasi (bullet) kiasi cha kuua kwa kasi?

Risasi haikwepwi kwa sarakasi wala mazingaombwe ya habari za vita ya maji maji 1905-1907 .

Risasi inakwepwa kwa njia mbili tu
1. Labda ulale kabla haijafyatuliwa. Mfano, Ukiona mtu anainua silaha ili akulenge basi lala faster hapo unaweza ukaikwepa risasi .

Japo , itategemeana na uwezo wako wa kulala kabla haijaachiliwa pia na uwezo wa mpigaji maana mpigaji akiwa na uwezo hata ukilala faster anaweza akapiga ya juu ikakudondokea ulipolala kisha ukalala daima .

2.kujikinga kwenye sehemu ambayo risasi haiwezi kupenya mfano, bullet proof vest au miamba/mawe magumu.

Bila hivyo, you're a dead body or badly injured.
Wahenga walishaimba "ukisikia paaa jua imekukosa",

Sent using Jamii Forums mobile app
 
SMG inatembea kwa sekunde mita 540 umbali wa kutua mita 2160

Hv SMG inatembea au risasi?

Then hapa risasi gani umeizungumzia ambayo inatembea mita 540 kwa sekunde na je hakuna utofauti kwenye risasi? Mfano hai 9mm na 7.62 au 5mm zaweza kuwa sawa kwenye kutembea?
Risasi imejengwa ktk sehem kuu 5,

1-balut .
Balut ni chemical maalum iliotengenezwa kitaalam ,chemical hiyo inaweza kua unyevu au ukavu lakini inalipuka.

2-ganda la risasi.

3-prima.
Ni ile sehem ya kitako cha risasi,

4-cutredge case.
Ni ile sehem risasi ilipounganishwa kati ya kichwa na mwili,

5-properant .
Kichwa cha risasi chenyewe.

Kwenye bunduki kuna vitu muhimu vinavyoshugulika na risasi kulipuka.ambavyo ni ,
Firelling pin,msumari.
Spring leaf. inayokamata huo msumali kwenye mitambo ya triger ,
Unapovuta kockinghandel,msumari unakaa tayari,ukivuta trigger spring inasukuma msumari kwa kasi na kugonga kwenye kitako cha risasi na risasi hainabudi kulipuka na kichwa cha risasi na mwili vinaachana kwa kasi ,mwili wa risas unabaki na kichwa kinatoka nje kwa kasi kwa kufuata mtutu.SMG inatembea kwa sekunde mita 540 umbali wa kutua mita 2160.

TAHADHARI .
RISASI SIO LAZIMA IWEKWE KWENYE BUNDUKI PEKEE NDIO ILIPUKE.UKIOKOTA KITU NAMNA KIYO KISALIMISHE HARAKA KWENYE VYOMBO VYA USALAMA ,MAANA HATA UKIIWEKA KWENYE MOTO ITALIPUKA KWA HARAKA SANA,NA KWAVILE ITAKUA HAINA UELEKEO KAMA MTUTU BASI KUNA HATARI YA KUKUDHURU WEWE MWENYEWE AU HATA WA KALIBUYAKO.

sent from my Samsung smart tv using JamiiForums
 
Wewe utakua unataka kuzifanyia majaribio aisee we noma sana umeona umetengeza butu so unataka maufundi humu mmh ngoja waje wenyewe watakujibu
 
Haya ndyo maajab ya risasi japo cjajua imetengenezwa VP,
1.Risasi ikitoka kwenye mdomo wa bunduki hukimbia kwa kuzunguka mpaka itakapoisha nguvu au kutua
2.Risasi huwaka moto kwa mbele
3.Risasi inapoingilia huwa na kijitundu kdogo lakn inapotokea huacha tundu kubwa sana
3.Risasi huenda umbali unaotegemeana na aina ya bunduki iliyotumika kufyatua Risasi hyo mfn,Risasi ya AkA 47; huweza kwenda umbali wa km 3.8 in a vacuum

Sent from my TECNO-N8 using JamiiForums mobile app
Wali iumba inakimbia huku inazunguka ili ichane mawimbi kiurahisi na iwe fasta
 
Nazidi kuelewa risasi kwenye tukio la mh Lissu kupigwa risasi kumbe inaweza penya kitu still ikafka taget na kusababisha madhara
 
Kile kichwa cha risasi ndani yake kuna kipande cha chuma ambayo ni lead type of iron. Aina hii ya chuma ni sumu kwa afya ya mnyama. Pia kasi ya risasi ni chanzo cha mtu kufa kwasababu ikipenya mwilini inaharibu body tissues kwa kiasi kikubwa na kusababisha damu nyingi kutoka eventually kifo
 
Kati ya vitu ambavyo mpka leo vinanipa shida ni kushindwa kujua ni mechanism gani iko ndani ya risasi (bullet) kiasi cha kuua kwa kasi, kwa sababu kuna vitu mfano kisu ni kikubwa kinaweza kukita ndani ya mwili wa binadam still mtu akawa hai kwa muda fulani kuliko majeruhi wa risasi....tafadhali wenye Kujua

Sent from my HUAWEI TIT-U02 using JamiiForums mobile app
Iko hivi,
Kuna bunduki za aina tatu; kwanza shot gun, semiautomatic na automatic gun.

Hizo shotgun ni bunduki za kizamani kama gobore au wanazotumia kiwindia.

Semiautomatic ni kama vile Semiautomatic riffle (SAR) ambazo hutumika sana kwenye gwaride.

Automatic zinatumika zaidi vitani, kama SMG, AK47, G3, Uzi gun etc.
Zipo za masafa marefu kama LMG (zenye risasi za mikanda) etc

Sasa zinavyofanya kazi nadhani ndio swali lako. Kwenye automatic ndio Mpango mzima.
Risasi zinakaa kwenye magazine (kama 30-40). Hatua ya kwanza inavuta cocking handle ili kuweka risasi chamber, pili unafungua usalama, hapo unaweza kuweka rapid au moja moja.
Hatua ya tatu unafyatua.
Sasa unapofyatua ile trigger kuna vitendo vinne vinafanyika kwa sekunde moja.
Kwanza baruti iliyomo kwenye ganda la risasi italipuka na kusababisha risasi iende mbele.
Mlipuko ule husababisha cocking handle iliyoshikwa na spring irudi nyuma na kuchota risasi nyingine kutoka kwenye magazine na kuiweka chamber huku lile ganda la risasi iliyolipuka likiruka nje. Mapigo hayo huendelea mithili ya machine hadi uachie trigger.
Hiyo ndio maana ya automatic.
Uchawi wote uko kwenye baruti inapolipuka na ndio inayotoa sauti kali. Risasi ina uwezo wa kuua ndani ya meter 100.
 
Kuna baadhi ya risasi nasikia ikifika mwilini inapasuka kuwa vipande hivyo kuleta athari kubwa sn..na ile speed/velocity yake mhh
 
Kati ya vitu ambavyo mpka leo vinanipa shida ni kushindwa kujua ni mechanism gani iko ndani ya risasi (bullet) kiasi cha kuua kwa kasi, kwa sababu kuna vitu mfano kisu ni kikubwa kinaweza kukita ndani ya mwili wa binadam still mtu akawa hai kwa muda fulani kuliko majeruhi wa risasi....tafadhali wenye Kujua

Sent from my HUAWEI TIT-U02 using JamiiForums mobile app
Kinachofyatua risasi itoke kwa kasi ni mlipuko wa baruti uliomo ndani ya risasi unachokifanya kichwa cha baruti kurushwa mbali kwa kasi na ganda linalobeba baruti kudondoka chini.
 
Risasi inaua haraka ikitegemeana na position mtu alipopigwa......ukipigwa moyo, au manleneo ya uti wa mgongo au kichwani ni rahisi kufa in less than a minute tofauti na aliyepigwa tumboni ambapo unaweza hata kwenda kufia mbele ya safari.......

Sent from my LG-F600K using JamiiForums mobile app
Ila tundu lissu hakufa kweli mungu yupo !!
 
Iko hivi,
Kuna bunduki za aina tatu; kwanza shot gun, semiautomatic na automatic gun.

Hizo shotgun ni bunduki za kizamani kama gobore au wanazotumia kiwindia.

Semiautomatic ni kama vile Semiautomatic riffle (SAR) ambazo hutumika sana kwenye gwaride.

Automatic zinatumika zaidi vitani, kama SMG, AK47, G3, Uzi gun etc.
Zipo za masafa marefu kama LMG (zenye risasi za mikanda) etc

Sasa zinavyofanya kazi nadhani ndio swali lako. Kwenye automatic ndio Mpango mzima.
Risasi zinakaa kwenye magazine (kama 30-40). Hatua ya kwanza inavuta cocking handle ili kuweka risasi chamber, pili unafungua usalama, hapo unaweza kuweka rapid au moja moja.
Hatua ya tatu unafyatua.
Sasa unapofyatua ile trigger kuna vitendo vinne vinafanyika kwa sekunde moja.
Kwanza baruti iliyomo kwenye ganda la risasi italipuka na kusababisha risasi iende mbele.
Mlipuko ule husababisha cocking handle iliyoshikwa na spring irudi nyuma na kuchota risasi nyingine kutoka kwenye magazine na kuiweka chamber huku lile ganda la risasi iliyolipuka likiruka nje. Mapigo hayo huendelea mithili ya machine hadi uachie trigger.
Hiyo ndio maana ya automatic.
Uchawi wote uko kwenye baruti inapolipuka na ndio inayotoa sauti kali. Risasi ina uwezo wa kuua ndani ya meter 100.
Kweli humu ni darasa. Asante kwa elimu.
 
Kam umeenda shule ni desa ka muingereza bw.isaac.newton na ile sheria yake namba tatu ya mwendo
Newton third "to every action there's equal and opposite reaction"
 
Back
Top Bottom