SoC03 Ni mhimu kuwa na tovuti au mfumo wa matokeo kwa shule za msingi na sekondari ili kuwarahisishia wazazi na walezi kupata wepesi wa kufuatilia maendeleo

SoC03 Ni mhimu kuwa na tovuti au mfumo wa matokeo kwa shule za msingi na sekondari ili kuwarahisishia wazazi na walezi kupata wepesi wa kufuatilia maendeleo

Stories of Change - 2023 Competition

SEMBOJE

Member
Joined
Aug 31, 2017
Posts
7
Reaction score
11
Ni mda mrefu hata sasa waalimu wa shule za msingi na sekondari wanatumia njia ya kutuma ripoti ya matokeo au karatasi yenye matokeo ya Mwanafunzi, Shule baadhi waalimu huwakusanya wanafunzi na kuanza kuwasomea matokeo yao kuanzia mwanafunzi wa nafasi ya kwanza mpaka kwa mwanafunzi aliyepata nafasi ya mwisho na kuhimizwa kuwa kila mwanafunzi akifika nyumbani awape taarifa wazazi wake kuwa amekuwa wa nafasi gani. Ingawa wanafunzi walio wengi hawafanyi hivyo. Pia zipo shule huwakusanya wanafunzi na kuanza kuwagawia ripoti ya karatasi ya matokeo na kuhimizwa kuwa kila mwanafunzi ahakikishe anamfikishia mzazi au mlezi wake ripoti hiyo ya matokeo.
WALIMU KUTOA RIPOTI ZA MATOKEO.jpg


Ambavyo wanafunzi wengi huwa hawafikishi karatasi ya matokeo yao kulingana na ufaulu walioupata. Hasa Wanafunzi waliopata ufaulu wa chini ndio inakuwa changamoto kufikisha kwa wazazi wao, ingawa hata hivyo wanafunzi wanaopata alama za juu hata wao wanapuzia kuwaonesha matokeo wazazi wao, japokuwa unakuta wazazi na walezi wanakuwa wanatamani kuyaona matokeo hayo.
SIFIKISHI REPORT HII.jpg


Imepelekea wazazi wengi kutopata matokeo ya watoto wao na kutokujua kabisa maendeleo ya mwanafunzi na kubaki kuwalaumu waalimu na kutokuwaamini walimu juu ya mitihani wanayoitoa kwamba inawezekana hawapangi matokeo na kutoa matokeo ya wanafunzi. Maana hata mzazi akijaribu kumuuliza mtoto wake juu ya matokeo, mtoto anamdaganya mzazi wake au mlezi wake kuwa hawajapata matokeo wala karatasi za mitihani.
KWELI.jpg


Hata hivyo njia hii wanayotumia waalimu wamejikuta wanapoteza hata karatasi za ripoti ya matokeo zinazobaki kama kumbukumbu ya mwanafunzi shuleni. Pia ikitokea ajali ya moto shuleni ofisi zikaungua na moto, au ikatokea mende na panya wakala zile karatasi za kumbukumbu au maendeleo ya mwafunzi husika, matokeo yake yaliyobaki shuleni kama kumbukumbu hupotea pia.
JENGO KUUNGUA.jpg


Pia kutokana na upotevu wa kumbukumbu hizo za maendeleo ya mwanafunzi shuleni hata ikitokea Mzazi au Mlezi ameamua kufuatilia shuleni matokeo ya mwanae au maendeleo ya taaluma ya mwanae ili ajue maendeleo yake, mwalimu humwambia kuwa kumbukumbu ya matokeo haipo kumbe imepotea.
KUFUATILIA MAENDELEO.jpg


Njia hii ya kutumia ripoti ya karatasi imekuwa changamoto sana;
  • Katika maendeleo ya mwanafunzi na kuinua taaluma ya mwanafunzi shuleni.​
  • Pia njia hii imefanya maandalizi ya matokeo na ripoti kwa waalimu kuwa kazi ngumu.​
  • Tena njia hii imesababisha wazazi na walezi kupata ugumu wa kujua maendeleo ya wanae.​
NAMNA YA KUFANYA ILI KUTOKANA NA CHANGAMOTO HIYO
Inatakiwa kila shule ya msingi na sekondari kuwa na tovuti au Mfumo utakao ruhusu kuweka matokeo ya kila mwanafunzi na taarifa zingine, yaani tovuti hiyo au mfumo huo uwe na uwezo wa kuruhusu kuweka matokeo ya mitihani ya majaribio, mitihani ya robo mhula, nusu mhula na mitihani ya mhula mzima kwa kila Darasa au kila kidato. Pia mfumo au tovuti hiyo iweze kuruhusu kuweka taarifa zingine za vitu au vifaa vingine vinavyotakiwa shuleni pamoja na michango ya shule inayotakiwa ili mzazi akiingia kwenye mfumo aone vitu vyote. Tovuti au mfumo huo umruhusu mzazi au mlezi kuweka maoni yake juu ya kuendeleza shule pamoja na taaluma ya wanafunzi.
Baada ya kufanya hivyo wazazi wataitwa ili waelezwe juu ya tovuti hiyo au mfumo huo namna gani unavyofanya kazi na umhimu wake.
WAZAZI KUELKEZWA MFUMO.jpg


Baada ya wazazi kupewa taarifa juu ya kuanzishwa kwa mfumo, na waalimu kuwa tayari kutekeleza wajibu wao wa kuingiza matokeo kwenye mfumo huo, tayari wazazi wameanza kufuatilia maendeleo ya watoto wao kwenye mfumo huo.
MFUMO NI MZURI AMEFELI.jpg
TOVUTI NURI MWANANGU YUPO VIZUR.jpg


Tunaona vyuo vikuu vimefanikiwa juu ya kutengeneza tovuti na mifumo. Na imekuwa rahisi kwa wazazi kufuatilia maendeleo ya mtoto, hata akiwa nyumbani kwenye simu janja (smartphone) au kwenye kompyuta anafuatilia taarifa ya chuo na maendeleo ya mwanachuo husika. Pia hata kutuma maombi imekuwa rahisi na kupokea fomu ya kujiunga na chuo imekuwa rahisi kuliko zamani ulikuwa unafuata fomu ya maombi na ya kujiunga baada ya kuchaguliwa kwenye chuo husika. Pia imewarahisishia wazazi na walezi kutambua sifa za chuo, ada za chuo pamoja na michango mingine ya chuo husika wakiwa nyumbani.
Hata hivyo mfumo au tovuti zikitengenezwa shule ya msingi na shule za sekondari zitasaidia sana kwa wanafunzi, wazazi na walezi husika juu ya uwajibikaji wao, hata kabla ya kufika shule husika sifa za shule pamoja na michango watazipata mtandaoni.

MALENGO YA KUUNDA KWA TOVUTI AU MFUMO SHULENI.
  • Lengo kuu ni kuwarahisishia wazazi na walezi kupata ripoti ya wanafunzi wao, kwa wakati pamoja na maendeleo yao shuleni kiurahisi na kwa wakati.​
  • Pia ni kwa lengo la kuinua taaluma ya mwanafunzi na shule husika na kuwarahisishia kazi waalimu juu ya maandalizi ya matokeo na ripoti za wanafunzi mtandaoni.​
HITIMISHO NA MAPENDEKEZO

Napenda kutoa ushauri kwamba serikali itengeneze mfumo ambao utaruhusu kila shule ya msingi na sekondari kujisajili na kumwezesha mwalimu husika kuweka matokeo ya wanafunzi au serikali ianze kuajiri wataalamu wa Tehama (IT) kwa kila shule ili ‘IT’’huyo awajibike kuitengenezea shule tovuti au mfumo wa kuweka matokeo ya wanafunzi.
MPYA MFUMO MPYA.jpg


Pia njia hii itawasaidia sana waalimu, wazazi na walezi kuinua taaluma ya wanafunzi pamoja na shule yenyewe. Na itasaidia pia kurahisisha kufuatilia maendeleo ya wanafunzi.
NIMEINGIA TAZAMA MATOKEO.jpg


Ili kutengeneza tovuti au mfumo huu napendekeza mtaalamu wa kompyuta (IT) atumie lugha zifuatazo ili mfumo uwe imara na ulinzi wa kutosha na baadhi za lugha zitasaidia mfumo uonekane na kusomeka vizuri kwenye Simu, Kompyuta aina ya ‘Desktop’ na ‘Laptop’, pia lugha hizo chini zingine zitasaidia kutengeneza “application’ (APP) ya mfumo husika ya matokeo;
  • HTML​
  • CSS​
  • PHP​
  • JAVASCRIPT​
  • JAVA​
  • SQL​
  • C++​
  • C#​
  • OBJECTIVE C​
  • ANGULAR​
  • GOLANG​
  • SCALAR​
ASANTENI MUNGU AWABARIKI.
 
Upvote 12
Back
Top Bottom