Ni michezo gani ya hatari uliwahi kufanya ili utoboe kimaisha?

Yaliwahi kunikuta ....maisha yaliponipiga chini mpaka nikaukimbia mji kwa madeni nikaenda tunduru kulima nyanya sasa mjomba ambae ndie kanilea akaanza kuumwa huko kijijini kwetu...Na bahati mbaya Hana mtoto na mke alimkimbia na wakati huo miche nishaipanda ilikuwa wastani wa 2000 kwahiyo katika stori na huyo binamu yangu nikamweleza hali halisi kuwa kijijini nahitajika na miche nishapanda tayari ishaanza maua kwahiyo inabidi nimuite mtoto wa baba mdogo aje kusimamia..... jamaa akanijibu usimuite yeye huyo ni mdogo atasumbua hebu nije mimi kwasababu ni mzoefu wa mambo ya bustani kwahiyo nikamtumia nauli akaja nikamkabidhi kila kitu mimi nikaondoka ....nikawa nampigia simu kumuulizia maendeleo jamaa ananiambia aisee hizi nyanya umekutana nazo na bei sokoni inapanda kila siku kumbe mshenzi hayupo kule kauza kila kitu kuanzia water pump,mtambo wa Zola,mbolea ,godoro,mtungi wa gesi,baiskel na gunia la mahindi katimkia zake dar,,, kumbe anaponipigia Simu yeye hayupo shambani chakushangaza mama yake ambae ni shangazi yangu akawa upande wa mwanae kwasababu dogo alileta utetezi wa kutunga kuwa nikitaka nimfanye msukule yeye dawa zake alizofanyiwa ndio zikamsaidia...
Ah pole sana mkuu me ningepiga panga mtu aisee
 
Niliajiriwa kwenye NGO fulani nilikuwa nasimamia mradi uliohusu masuala ya kuwawezesha watu fulani. Sasa nilikuwa na team kubwa ya kufanya hiyo kazi na mimi ndo nilikuwa msimaizi wao na malipo yao yalikuwa ni kwa njia ya simu walikuwa wanalipwa laki 1. Siku ya kulipwa ikifika mimi ndio nilikuwa naandaa sheet ya malipo naweka namba zao wanalipwa na ilikuwa kama mhusika hajameet target basi halipwi. Sasa ile kazi ilikuwa ngumu kiasi kwahiyo wengi waliacha.sasa mimi walioacha wote sikuwatoa kwenye pay roll ila nilifanya mchongo na jamaa mmoja alikuwa mtu wa madili madili sana nikampanga anisajililie laini 30 zenye majina tofauti ili ziwe zinapokea fedha za wale waliocha kazi ( ilikuwa kipindi cha nyuma wakati mambo ya kusajili laini hayako complicated kama sasa). Kiufupi nilipiga sana zile hela na jamaa aliyenifanyia mchongo wa laini nilikuwa nampa laki 3 kila malipo yakitoka. Nilijitahidi tu kufanya kila liwezekanalo target isishuke ili nisije kushtukiwa kuwa watu hawapo kazini( hapa kupika taarifa kulihusika sana) nashukuru sikuwahi kushtukiwa maana kila wakija kukagua mradi nilikuwa naandaa mazingira wakute kila kitu fresh mpaka mradi unaisha nilikuwa nimesave si haba
 
Kuna wakati ni bora ujilipue lolote litakalotokea, litokee tu. Hii nchi, ukiwa mfanyabiashara, wakati mwingine ni kama umetangaza vita na serikali. Kuna mifumo kandamizi sana kwa wafanyabiashara.
Binafsi, bila kuwa na roho ngumu, uthubutu na ujasiri wa kuchukua hatua, leo nisingekuwa hapa nilipo.

KISA CHA KWANZA: KUFUNGUA DISPENSARY BILA KUFUATA PROTOCOL ZOZOTE ZA WIZARA YA AFYA​

Ilikuwa mwaka 2010, baada ya kumaliza chuo cha afya na kufanya internship yangu katika Hospitali ya Mwananyamala. Niliporudi mtaani, nilikuwa sina ajira. Cha ajabu ni kwamba, karibu kila mmoja wa wenzangu walipata kazi serikalini, lakini mimi peke yangu nikakosa.
Hali hiyo iliniumiza sana, Nilipoangalia upande wa sekta binafsi, mishahara ilikuwa midogo sana ukilinganisha na matarajio yangu.
Nikaamua kujilipua.
Nikaenda Mbande Chamazi, nikatafuta nyumba ya kawaida na kuamua kufungua dispensary bila kufuata taratibu wala kupata vibali husika. Nikatafuta manesi wa darasa la saba na kuanza kufanya nao kazi.

Sio siri, miezi 9 ya mwanzo nilipiga sana pesa—na nilipiga pesa vibaya mno kwa siku net profit nilikuwa naingiza mpaka 800k-500k. Wakati huo kulikuwa na uhaba mkubwa wa vituo vya afya katika eneo lile, hivyo watu walikuwa wengi na biashara ilikuwa inaenda sana.

Lakini kuna jambo moja nililojifunza hapo:
Siku zote ukizoea kufanya vitu visivyo sahihi, baada ya muda vinakuwa mazoea. Unaacha kuona kama ni kosa na unaanza kuona ni jambo la kawaida. Unajisahau.
Hapo ndipo nilipoanza kuelewa kwamba wakati mwingine mafanikio ya haraka yanaweza kukufanya uzowee njia ambazo baadaye zinaweza kukugharimu sana.
Kiukweli nilijisahau sana nilikuwa nimevimbiwa mafanikio,ghafla siku isiyo na jina ikaja team ya wizara,halmashauri na TRA kituo kikafungwa nikabebwa police mpaka mahakamani kwenye account nilikuwa na pesa za kutosha tu nikahonga sana si chini ya mil 40 nikaja nikatoka ila nikapigwa stop nisipractice tena huduma ya afya leseni yangu ikapigwa pin.

KISA CHA PILI: MUENDELEZO — KUFANYA FRAUD BIMA NHIF

NIKAAMUA KURUDI KWENYE GAME KIBISHI — SAFARI HII NIKASEMA NIFATE PROTOCOL WANAZOZITAKA WAO.
Safari hii nikatafuta eneo lingine Mbagala, maana pale Mbande nilikuta tayari wamefungua dispensary nyingine, tena kwenye eneo lilelile nililokuwepo hapo awali.
Nilikodi nyumba, nikafanya ukarabati mzuri na kuanza biashara. Tuseme nilikuwa na kismati sana, maana wateja walikuwa wengi kupita kawaida, hususani wagonjwa waliokuwa wanatumia bima ya NHIF.
Kwa kuona fursa hiyo, nikaamua kwenda ofisi za NHIF Bendera Tatu, Bandari, kuomba kibali cha kuanza kutoa huduma kwa wagonjwa wa bima.
Ndani ya miezi mitatu tu, nikaruhusiwa.
Nikaanza kutoa huduma za matibabu kwa wagonjwa wa bima.

MWANZO WA BIASHARA ULINIPA SOMO KUBWA.
Mwanzo, malipo niliyokuwa napata kutoka NHIF yalikuwa madogo sana ukilinganisha na gharama nilizokuwa natumia. Gharama zilikuwa kubwa, lakini faida ilikuwa ndogo.
Hapo ndipo nikaanza kufanya ujanja.
Nikaanza kufoji baadhi ya fomu za wagonjwa wa bima.
Mwanzoni niliona kama nimepata njia ya kutengeneza pesa. Kipato kikaongezeka sana, mpaka nikawa napata karibu MILIONI 14 kwa mwezi.
Lakini kama usemavyo, “UKICHEZA NA MOTO, MWISHO WAKE UTAKUUNGA.”
Baadaye wenyewe wakaja kushtuka.
Kesi ikawa kubwa sana.
Kwa kipindi hicho, nilikuwa nimeisababishia mfuko wa bima hasara ya takribani MILIONI 125.
Nilipoona mambo yamekuwa mazito, sikusubiri.
NIKAFUNGASHA VIRAGO VYANGU FASTA.
Nikaiuza ile dispensary kwa mtu mwingine, nikatembea zangu.
Baadaye nikaja kusikia kwamba kile kituo nacho kilifungwa nikawa most wanted.shukrani sana marehemu dada fortnatus raymond huyu alikuwa kitengo bima alinipambania kesi ikaishia hewani

Kisa cha mwisho iki siwezi kukisimulia kilikuwa upotevu wa dawa katika bohari kuu la dawa MSD .

Ila kwa sasa nimeachana na hiyo michezo nimekoswa koswa mara mbili kwenda jela.

Karibu na wewe ulete mkasa wako
Life ain’t for the weak.

Wale wanangu wa MSD mpo hapa ☝🏽☝🏽?

🏃🏾‍♂️🏃🏾‍♂️ kadeti,shati, moka na koti jeupe lakini roho ya paka 😎😁
 
Emergency department… kuna majeruhi wa ajali ya bodaboda uku mpakani

Ambulance ikifika jaza machanjio.. 🚨🚨🚨 mzigo unafika town mapema sana.. Michezo hatari

LIFE ANT’T FOR THE WEAK. Kunja moyo broo get the fucin bag. Get the fucin paper.
 
Mtu unaandaa uzi na kuuhariri..alafu unaenda bar kushtua..unagundua kwamba nchii hii maaskari wanapiga mpaka mtu ana ejaculate..unarudi nyumbani kuufuta kabla ya kuupandisha...
 
Back
Top Bottom