Ni michezo gani ya hatari uliwahi kufanya ili utoboe kimaisha?

Ni michezo gani ya hatari uliwahi kufanya ili utoboe kimaisha?

Kuna wakati ni bora ujilipue lolote litakalotokea, litokee tu. Hii nchi, ukiwa mfanyabiashara, wakati mwingine ni kama umetangaza vita na serikali. Kuna mifumo kandamizi sana kwa wafanyabiashara.
Binafsi, bila kuwa na roho ngumu, uthubutu na ujasiri wa kuchukua hatua, leo nisingekuwa hapa nilipo.

KISA CHA KWANZA: KUFUNGUA DISPENSARY BILA KUFUATA PROTOCOL ZOZOTE ZA WIZARA YA AFYA​

Ilikuwa mwaka 2010, baada ya kumaliza chuo cha afya na kufanya internship yangu katika Hospitali ya Mwananyamala. Niliporudi mtaani, nilikuwa sina ajira. Cha ajabu ni kwamba, karibu kila mmoja wa wenzangu walipata kazi serikalini, lakini mimi peke yangu nikakosa.
Hali hiyo iliniumiza sana, Nilipoangalia upande wa sekta binafsi, mishahara ilikuwa midogo sana ukilinganisha na matarajio yangu.
Nikaamua kujilipua.
Nikaenda Mbande Chamazi, nikatafuta nyumba ya kawaida na kuamua kufungua dispensary bila kufuata taratibu wala kupata vibali husika. Nikatafuta manesi wa darasa la saba na kuanza kufanya nao kazi.

Sio siri, miezi 9 ya mwanzo nilipiga sana pesa—na nilipiga pesa vibaya mno kwa siku net profit nilikuwa naingiza mpaka 800k-500k. Wakati huo kulikuwa na uhaba mkubwa wa vituo vya afya katika eneo lile, hivyo watu walikuwa wengi na biashara ilikuwa inaenda sana.

Lakini kuna jambo moja nililojifunza hapo:
Siku zote ukizoea kufanya vitu visivyo sahihi, baada ya muda vinakuwa mazoea. Unaacha kuona kama ni kosa na unaanza kuona ni jambo la kawaida. Unajisahau.
Hapo ndipo nilipoanza kuelewa kwamba wakati mwingine mafanikio ya haraka yanaweza kukufanya uzowee njia ambazo baadaye zinaweza kukugharimu sana.
Kiukweli nilijisahau sana nilikuwa nimevimbiwa mafanikio,ghafla siku isiyo na jina ikaja team ya wizara,halmashauri na TRA kituo kikafungwa nikabebwa police mpaka mahakamani kwenye account nilikuwa na pesa za kutosha tu nikahonga sana si chini ya mil 40 nikaja nikatoka ila nikapigwa stop nisipractice tena huduma ya afya leseni yangu ikapigwa pin.

KISA CHA PILI: MUENDELEZO — KUFANYA FRAUD BIMA NHIF

NIKAAMUA KURUDI KWENYE GAME KIBISHI — SAFARI HII NIKASEMA NIFATE PROTOCOL WANAZOZITAKA WAO.
Safari hii nikatafuta eneo lingine Mbagala, maana pale Mbande nilikuta tayari wamefungua dispensary nyingine, tena kwenye eneo lilelile nililokuwepo hapo awali.
Nilikodi nyumba, nikafanya ukarabati mzuri na kuanza biashara. Tuseme nilikuwa na kismati sana, maana wateja walikuwa wengi kupita kawaida, hususani wagonjwa waliokuwa wanatumia bima ya NHIF.
Kwa kuona fursa hiyo, nikaamua kwenda ofisi za NHIF Bendera Tatu, Bandari, kuomba kibali cha kuanza kutoa huduma kwa wagonjwa wa bima.
Ndani ya miezi mitatu tu, nikaruhusiwa.
Nikaanza kutoa huduma za matibabu kwa wagonjwa wa bima.

MWANZO WA BIASHARA ULINIPA SOMO KUBWA.
Mwanzo, malipo niliyokuwa napata kutoka NHIF yalikuwa madogo sana ukilinganisha na gharama nilizokuwa natumia. Gharama zilikuwa kubwa, lakini faida ilikuwa ndogo.
Hapo ndipo nikaanza kufanya ujanja.
Nikaanza kufoji baadhi ya fomu za wagonjwa wa bima.
Mwanzoni niliona kama nimepata njia ya kutengeneza pesa. Kipato kikaongezeka sana, mpaka nikawa napata karibu MILIONI 14 kwa mwezi.
Lakini kama usemavyo, “UKICHEZA NA MOTO, MWISHO WAKE UTAKUUNGA.”
Baadaye wenyewe wakaja kushtuka.
Kesi ikawa kubwa sana.
Kwa kipindi hicho, nilikuwa nimeisababishia mfuko wa bima hasara ya takribani MILIONI 125.
Nilipoona mambo yamekuwa mazito, sikusubiri.
NIKAFUNGASHA VIRAGO VYANGU FASTA.
Nikaiuza ile dispensary kwa mtu mwingine, nikatembea zangu.
Baadaye nikaja kusikia kwamba kile kituo nacho kilifungwa nikawa most wanted.shukrani sana marehemu dada fortnatus raymond huyu alikuwa kitengo bima alinipambania kesi ikaishia hewani

Kisa cha mwisho iki siwezi kukisimulia kilikuwa upotevu wa dawa katika bohari kuu la dawa MSD wenye thamani ya bil 14,wenzangu 4 wapo rumande kesi yao ilisomwa majuzi

Ila kwa sasa nimeachana na hiyo michezo nimekoswa koswa mara mbili kwenda jela.

Karibu na wewe ulete mkasa wako

Bongo bila michezo michafu hutoboi. Utasubiri Sana
 
Kama hapa wapo watakaoibuka kusema chai.. Watu unarisk ili upate na kweli unapata. Mimi nilikuja kukodi gari la polisi nkabebea bangi hadi sehem husika tukapewa zetu tukarudi mwisho wa siku tukazoea ila siku moja tukikiona cha moto pesa tulizotoa kujisafisha ili pesa kweli acha sasa hivi bangi inauzwa na halaiki ya watu. Mda ule ilikuwa ni connection.
 
Sahihi kabisa mkuu...japo huwa siyo mtu wa kukata tamaa..ntarudia tena kwa ubora zaidi.
Yaliwahi kunikuta ....maisha yaliponipiga chini mpaka nikaukimbia mji kwa madeni nikaenda tunduru kulima nyanya sasa mjomba ambae ndie kanilea akaanza kuumwa huko kijijini kwetu...Na bahati mbaya Hana mtoto na mke alimkimbia na wakati huo miche nishaipanda ilikuwa wastani wa 2000 kwahiyo katika stori na huyo binamu yangu nikamweleza hali halisi kuwa kijijini nahitajika na miche nishapanda tayari ishaanza maua kwahiyo inabidi nimuite mtoto wa baba mdogo aje kusimamia..... jamaa akanijibu usimuite yeye huyo ni mdogo atasumbua hebu nije mimi kwasababu ni mzoefu wa mambo ya bustani kwahiyo nikamtumia nauli akaja nikamkabidhi kila kitu mimi nikaondoka ....nikawa nampigia simu kumuulizia maendeleo jamaa ananiambia aisee hizi nyanya umekutana nazo na bei sokoni inapanda kila siku kumbe mshenzi hayupo kule kauza kila kitu kuanzia water pump,mtambo wa Zola,mbolea ,godoro,mtungi wa gesi,baiskel na gunia la mahindi katimkia zake dar,,, kumbe anaponipigia Simu yeye hayupo shambani chakushangaza mama yake ambae ni shangazi yangu akawa upande wa mwanae kwasababu dogo alileta utetezi wa kutunga kuwa nikitaka nimfanye msukule yeye dawa zake alizofanyiwa ndio zikamsaidia...
 
Ulitaka kumtoa msukule😃
 
Ulitaka kumtoa msukule😃
Hapana..shida nilifanikiwa nipo mdogo sana wakati nina miaka 20 nilikuwa na pesa ndefu Sana.....kwahiyo watu wakawa na wivu na mafanikio sasa Kuna vifo vilitokea kwenye ukoo wetu nikaangushiwa lawama ndio maana ilifikia hatua wakati ule nina pesa sikuwa napenda kwenda kuangalia wagonjwa labda wawe wazazi wangu kwasababu isije unaenda kumuona ghafla Hali ikabadilika...kwahiyo hata nilipofilisika jamii ya kule kwetu wakaamini nilivunja mashart jambo linaloumiza mno
 
Back
Top Bottom