Ni michezo gani ya hatari uliwahi kufanya ili utoboe kimaisha?

Yaliwahi kunikuta ....maisha yaliponipiga chini mpaka nikaukimbia mji kwa madeni nikaenda tunduru kulima nyanya sasa mjomba ambae ndie kanilea akaanza kuumwa huko kijijini kwetu...Na bahati mbaya Hana mtoto na mke alimkimbia na wakati huo miche nishaipanda ilikuwa wastani wa 2000 kwahiyo katika stori na huyo binamu yangu nikamweleza hali halisi kuwa kijijini nahitajika na miche nishapanda tayari ishaanza maua kwahiyo inabidi nimuite mtoto wa baba mdogo aje kusimamia..... jamaa akanijibu usimuite yeye huyo ni mdogo atasumbua hebu nije mimi kwasababu ni mzoefu wa mambo ya bustani kwahiyo nikamtumia nauli akaja nikamkabidhi kila kitu mimi nikaondoka ....nikawa nampigia simu kumuulizia maendeleo jamaa ananiambia aisee hizi nyanya umekutana nazo na bei sokoni inapanda kila siku kumbe mshenzi hayupo kule kauza kila kitu kuanzia water pump,mtambo wa Zola,mbolea ,godoro,mtungi wa gesi,baiskel na gunia la mahindi katimkia zake dar,,, kumbe anaponipigia Simu yeye hayupo shambani chakushangaza mama yake ambae ni shangazi yangu akawa upande wa mwanae kwasababu dogo alileta utetezi wa kutunga kuwa nikitaka nimfanye msukule yeye dawa zake alizofanyiwa ndio zikamsaidia...
Mkuu niliita mtu site kupaka rangi..ndugu..akamaliza akakunja hela thrn akaja kusema kuwa nataka nimpe TB mimi nitajirike😀😀😀😀
 
Nilipigiwa simu na jamaa yangu kua Kuna washikaji(wateja wake) wanauza mawe ya dhahabu kama robo mfuko ule wa kg50, na yeye hana hela ya kuyanunua. Hivyo nichukue hela kwa tajiri yangu twende tukafanye nao biashara.

Nikachukua kama millioni 10, gari ya tajiri na nikamuomba bastola ake kama ulinzi wkt huo sijui hata inavyotumiwa, nika drive mpaka walipo nikakuta watu wa nne na mshikaji wangu wa 5.

Ile kuongea nao wakadai tuwape millioni 27, apo ndo nikajua huo mzigo una hela za kutosha. Huku na huku tukapunguziana mpaka million 18, hela sasa ikawa changamoto na ukizingatia hiyo ni saa saba usiku.

Ile kuwapanga jamaa wakagoma na mzigo wao wakautaka ili wasepe maana hela haitoshi, nikaona msinitanie nikajitoa akili maksudi(nikawa mkali). Jamaa wakachomoa mapanga na matusi juu, wakasema wao siyo wachimbaji hivyo mizigo wanaiiba katika mazingira magumu sana.

Nikapata picha kua hapa na Dili na watu gani?, kumbe nao ni vibaka tu nikachomoa bastola nikatishia yoyote atakae nisogelea nampeleka kuzimu, tukawaambia wachukue millioni 8 nyingine waijie asubui sana wakakubali kishingo upande baada ya jamaa yangu kuongea nao na ukizingatia ni wateja wake.

Tukaubeba mzigo, nikawasha gari mpaka kwa washikaji wenye vinu vya kutwangia mawe. Tukafanya process zote usiku huo, tukakamua kama gram 492. Asubui tukauza tukatoa gharama zote tukagawana faida na jamaa yangu.

Tajiri nikampelekea hela yake nikamwambia biashara ilishindikana, ilipofika usiku nikampigia simu askari mmoja jamaa yangu nikampanga anisindikize sehemu na achukue bunduki Kuna posho ya maana. Tukaenda baa Moja hivi siyo maarufu tukiwa watatu, nikamwambia jamaa yangu awapigie wale vibaka waijie hela zao. Wakaja tukawapa hela yao na mikwara mingi sana kua sisi wenyewe siyo wanyonge ni watu wa kazi na ukizingatia askari alikuepo amevaa nguo za kiraia na gobole lake mabegani.

Safari yetu ya kupata hela za kula ilianzia hapo na jamaa yangu.
 
Kupanda jahazi kutoka bagamoyo,Kunduchi,na mbweni kwenda Zanzibar kwenda kununua betri tiger, tv za chogo,sukari,radio,na na fridge tena nauli ilikuwa 3000
Kwenye jahazi hapo inabidi ukaze roho maana mara umepigwa na wimbi maji yanaanza kuingia ndani, mnaanza kuchota na kutoa nnje yaani full risk ila ilikuwa inalipa sn......
 
Hii ndo ilikuwa mara yangu ya kwanza na ya mwisho kupanda boti na kwenda zanzbar miaka ya 2008s huko.

Sababu ya kwenda ilikuwa nataka nianze biashara ya simu used baada ya biashara ya simu ya mwisho kuuza kunipeleka police (simu ya wizi).

Kwenye kupambsns kwangu kuuza na kununua simu nikawa nafatilia mchongo wa simu used zanzbar kuwa ni bei rahisi ukija kuuza bongo unaweza kupata hsta faida mara 2 au 3,sema kipengele kikawa kumpata mtu wa kunipa connection.

Hapa niseme tu kuwa ndugu zetu wa zanzbar upande wa kukupa connection hasa kama wewe siyo mtu wa kwao huwa ni ngumu sana jamaa zangu kibao ambso wana asili ya huko wakanitupa mie nkaona syo kesi acha niende nikifeli ntarudi.

Asubuhi na mapema niko zangu feri ndo for the first time napanda boti kwenye maisha yangu kwenye account nna kama 10m cash mfkoni iko 2m.

Katikati ya safari nilitapita mno maana sijawahi kupanda boti kwenye maisha yangu lakini si haba nikafika zanzbar.

Safari sasa ikaanza kuanza kutafuta sehemu tafuta na wewe siku ya kwanza nkalala sasa pale nlipolala ilikuwa ni kama nyumba ya familia lakini vyumba 4 vinakodishwa i hope kama udharnda zanzbar unaelewa hili, basi jioni kwenye story na mwenye nyumba nikampa story ya kilichonipeleka zenj kuwa nmekuja kuanza biashara ya kununua simu used.

Mzee tuliongea nae sana inshort alinipenda by the way am introvert yani siyo muongeaji sana na nna muonekano flani hivi wa uinocent, usiku ule ndo nkajua bwana kuwa mzee ni mganga.

Akanambia mwanangu najua unapambana kesho asubuhi kuna dua zinafanyika hapa kuna vijana wangu wametoka dar nao wana biashara ya kuuza spare za magari hvyo natakiwa kuwafanyia dua na kinga kama uko tayar ntakusaidia na ww bure mie nkajitoa muhanga nkakubali.

Asubuhi kufika kweli walikuja vijana wake pale wa 5 mzee akawaelezea kuhusu mimi moja mbili tatu design kama tuka match basi ikapigwa dua pale na mengineyo ambayo sijawahi kuyaona ama kushuhudia (itoshe kusema mpemba akiwa mchawi au mganga anakuwa mganga hasa)

Mchana hao tukaingia town sasa nikapakua mzgo wa kutosha simu nikaongezea pc na hizi tv zinakuwa zile used za nje.

Tukalala sasa mzee ilikuwa kila akiongea anachomekea kesho wala msijali mtatoboa tu asubuhi nikaanda mzgo wangu sema kulikuwa na pilika pilika nyingi nkaja gundua mwishoni kuwa natakjwa mzgo nlonunua niulipie na kodi kubwa ila mzee akanambia usijali utaondoka na wenzio usiku na jahazi.

Mh hapo nkaguna kwanza nkamwambia mzee mbona katika maisha yangu sijawahi kuliona jahazi la kwenda zanzbar pale kivukoni mzee akacheka akanambia utayaona na utayapanda tu leo ni kama meli ulokuja nayo tu.

Mie baada ya kuambiwa hvyo plus hela nauli ni ndogo sana nkajisemea utajiri ndo huu ngoja npumzike usiku niingie mzgoni kwa safar ya usiku.

Ntakuja malizia kipande cha mwisho soon
 
Nilipigiwa simu na jamaa yangu kua Kuna washikaji(wateja wake) wanauza mawe ya dhahabu kama robo mfuko ule wa kg50, na yeye hana hela ya kuyanunua. Hivyo nichukue hela kwa tajiri yangu twende tukafanye nao biashara.

Nikachukua kama millioni 10, gari ya tajiri na nikamuomba bastola ake kama ulinzi wkt huo sijui hata inavyotumiwa, nika drive mpaka walipo nikakuta watu wa nne na mshikaji wangu wa 5.

Ile kuongea nao wakadai tuwape millioni 27, apo ndo nikajua huo mzigo una hela za kutosha. Huku na huku tukapunguziana mpaka million 18, hela sasa ikawa changamoto na ukizingatia hiyo ni saa saba usiku.

Ile kuwapanga jamaa wakagoma na mzigo wao wakautaka ili wasepe maana hela haitoshi, nikaona msinitanie nikajitoa akili maksudi(nikawa mkali). Jamaa wakachomoa mapanga na matusi juu, wakasema wao siyo wachimbaji hivyo mizigo wanaiiba katika mazingira magumu sana.

Nikapata picha kua hapa na Dili na watu gani?, kumbe nao ni vibaka tu nikachomoa bastola nikatishia yoyote atakae nisogelea nampeleka kuzimu, tukawaambia wachukue millioni 8 nyingine waijie asubui sana wakakubali kishingo upande baada ya jamaa yangu kuongea nao na ukizingatia ni wateja wake.

Tukaubeba mzigo, nikawasha gari mpaka kwa washikaji wenye vinu vya kutwangia mawe. Tukafanya process zote usiku huo, tukakamua kama gram 492. Asubui tukauza tukatoa gharama zote tukagawana faida na jamaa yangu.

Tajiri nikampelekea hela yake nikamwambia biashara ilishindikana, ilipofika usiku nikampigia simu askari mmoja jamaa yangu nikampanga anisindikize sehemu na achukue bunduki Kuna posho ya maana. Tukaenda baa Moja hivi siyo maarufu tukiwa watatu, nikamwambia jamaa yangu awapigie wale vibaka waijie hela zao. Wakaja tukawapa hela yao na mikwara mingi sana kua sisi wenyewe siyo wanyonge ni watu wa kazi na ukizingatia askari alikuepo amevaa nguo za kiraia na gobole lake mabegani.

Safari yetu ya kupata hela za kula ilianzia hapo na jamaa yangu.
Hii weka mbali na watoto, sijapenda pale ulipo mgeuka tajirii Yako na kusema biashara ilishindikana
 
Hii ndo ilikuwa mara yangu ya kwanza na ya mwisho kupanda boti na kwenda zanzbar miaka ya 2008s huko.

Sababu ya kwenda ilikuwa nataka nianze biashara ya simu used baada ya biashara ya simu ya mwisho kuuza kunipeleka police (simu ya wizi).

Kwenye kupambsns kwangu kuuza na kununua simu nikawa nafatilia mchongo wa simu used zanzbar kuwa ni bei rahisi ukija kuuza bongo unaweza kupata hsta faida mara 2 au 3,sema kipengele kikawa kumpata mtu wa kunipa connection.

Hapa niseme tu kuwa ndugu zetu wa zanzbar upande wa kukupa connection hasa kama wewe siyo mtu wa kwao huwa ni ngumu sana jamaa zangu kibao ambso wana asili ya huko wakanitupa mie nkaona syo kesi acha niende nikifeli ntarudi.

Asubuhi na mapema niko zangu feri ndo for the first time napanda boti kwenye maisha yangu kwenye account nna kama 10m cash mfkoni iko 2m.

Katikati ya safari nilitapita mno maana sijawahi kupanda boti kwenye maisha yangu lakini si haba nikafika zanzbar.

Safari sasa ikaanza kuanza kutafuta sehemu tafuta na wewe siku ya kwanza nkalala sasa pale nlipolala ilikuwa ni kama nyumba ya familia lakini vyumba 4 vinakodishwa i hope kama udharnda zanzbar unaelewa hili, basi jioni kwenye story na mwenye nyumba nikampa story ya kilichonipeleka zenj kuwa nmekuja kuanza biashara ya kununua simu used.

Mzee tuliongea nae sana inshort alinipenda by the way am introvert yani siyo muongeaji sana na nna muonekano flani hivi wa uinocent, usiku ule ndo nkajua bwana kuwa mzee ni mganga.

Akanambia mwanangu najua unapambana kesho asubuhi kuna dua zinafanyika hapa kuna vijana wangu wametoka dar nao wana biashara ya kuuza spare za magari hvyo natakiwa kuwafanyia dua na kinga kama uko tayar ntakusaidia na ww bure mie nkajitoa muhanga nkakubali.

Asubuhi kufika kweli walikuja vijana wake pale wa 5 mzee akawaelezea kuhusu mimi moja mbili tatu design kama tuka match basi ikapigwa dua pale na mengineyo ambayo sijawahi kuyaona ama kushuhudia (itoshe kusema mpemba akiwa mchawi au mganga anakuwa mganga hasa)

Mchana hao tukaingia town sasa nikapakua mzgo wa kutosha simu nikaongezea pc na hizi tv zinakuwa zile used za nje.

Tukalala sasa mzee ilikuwa kila akiongea anachomekea kesho wala msijali mtatoboa tu asubuhi nikaanda mzgo wangu sema kulikuwa na pilika pilika nyingi nkaja gundua mwishoni kuwa natakjwa mzgo nlonunua niulipie na kodi kubwa ila mzee akanambia usijali utaondoka na wenzio usiku na jahazi.

Mh hapo nkaguna kwanza nkamwambia mzee mbona katika maisha yangu sijawahi kuliona jahazi la kwenda zanzbar pale kivukoni mzee akacheka akanambia utayaona na utayapanda tu leo ni kama meli ulokuja nayo tu.

Mie baada ya kuambiwa hvyo plus hela nauli ni ndogo sana nkajisemea utajiri ndo huu ngoja npumzike usiku niingie mzgoni kwa safar ya usiku.

Ntakuja malizia kipande cha mwisho soon
Nitag
 
Back
Top Bottom