Ni michezo gani ya hatari uliwahi kufanya ili utoboe kimaisha?

Ni michezo gani ya hatari uliwahi kufanya ili utoboe kimaisha?

Kuna wakati ni bora ujilipue lolote litakalotokea, litokee tu. Hii nchi, ukiwa mfanyabiashara, wakati mwingine ni kama umetangaza vita na serikali. Kuna mifumo kandamizi sana kwa wafanyabiashara.
Binafsi, bila kuwa na roho ngumu, uthubutu na ujasiri wa kuchukua hatua, leo nisingekuwa hapa nilipo.

KISA CHA KWANZA: KUFUNGUA DISPENSARY BILA KUFUATA PROTOCOL ZOZOTE ZA WIZARA YA AFYA​


Ilikuwa mwaka 2010, baada ya kumaliza chuo cha afya na kufanya internship yangu katika Hospitali ya Mwananyamala. Niliporudi mtaani, nilikuwa sina ajira. Cha ajabu ni kwamba, karibu kila mmoja wa wenzangu walipata kazi serikalini, lakini mimi peke yangu nikakosa.
Hali hiyo iliniumiza sana, Nilipoangalia upande wa sekta binafsi, mishahara ilikuwa midogo sana ukilinganisha na matarajio yangu.
Nikaamua kujilipua.
Nikaenda Mbande Chamazi, nikatafuta nyumba ya kawaida na kuamua kufungua dispensary bila kufuata taratibu wala kupata vibali husika. Nikatafuta manesi wa darasa la saba na kuanza kufanya nao kazi.

Sio siri, miezi 9 ya mwanzo nilipiga sana pesa—na nilipiga pesa vibaya mno kwa siku net profit nilikuwa naingiza mpaka 800k-500k. Wakati huo kulikuwa na uhaba mkubwa wa vituo vya afya katika eneo lile, hivyo watu walikuwa wengi na biashara ilikuwa inaenda sana.

Lakini kuna jambo moja nililojifunza hapo:
Siku zote ukizoea kufanya vitu visivyo sahihi, baada ya muda vinakuwa mazoea. Unaacha kuona kama ni kosa na unaanza kuona ni jambo la kawaida. Unajisahau.
Hapo ndipo nilipoanza kuelewa kwamba wakati mwingine mafanikio ya haraka yanaweza kukufanya uzowee njia ambazo baadaye zinaweza kukugharimu sana.
Kiukweli nilijisahau sana nilikuwa nimevimbiwa mafanikio,ghafla siku isiyo na jina ikaja team ya wizara,halmashauri na TRA kituo kikafungwa nikabebwa police mpaka mahakamani kwenye account nilikuwa na pesa za kutosha tu nikahonga sana si chini ya mil 40 nikaja nikatoka ila nikapigwa stop nisipractice tena huduma ya afya leseni yangu ikapigwa pin.

KISA CHA PILI: MUENDELEZO — KUFANYA FRAUD BIMA NHIF

NIKAAMUA KURUDI KWENYE GAME KIBISHI — SAFARI HII NIKASEMA NIFATE PROTOCOL WANAZOZITAKA WAO.
Safari hii nikatafuta eneo lingine Mbagala, maana pale Mbande nilikuta tayari wamefungua dispensary nyingine, tena kwenye eneo lilelile nililokuwepo hapo awali.
Nilikodi nyumba, nikafanya ukarabati mzuri na kuanza biashara. Tuseme nilikuwa na kismati sana, maana wateja walikuwa wengi kupita kawaida, hususani wagonjwa waliokuwa wanatumia bima ya NHIF.
Kwa kuona fursa hiyo, nikaamua kwenda ofisi za NHIF Bendera Tatu, Bandari, kuomba kibali cha kuanza kutoa huduma kwa wagonjwa wa bima.
Ndani ya miezi mitatu tu, nikaruhusiwa.
Nikaanza kutoa huduma za matibabu kwa wagonjwa wa bima.

MWANZO WA BIASHARA ULINIPA SOMO KUBWA.
Mwanzo, malipo niliyokuwa napata kutoka NHIF yalikuwa madogo sana ukilinganisha na gharama nilizokuwa natumia. Gharama zilikuwa kubwa, lakini faida ilikuwa ndogo.
Hapo ndipo nikaanza kufanya ujanja.
Nikaanza kufoji baadhi ya fomu za wagonjwa wa bima.
Mwanzoni niliona kama nimepata njia ya kutengeneza pesa. Kipato kikaongezeka sana, mpaka nikawa napata karibu MILIONI 14 kwa mwezi.
Lakini kama usemavyo, “UKICHEZA NA MOTO, MWISHO WAKE UTAKUUNGA.”
Baadaye wenyewe wakaja kushtuka.
Kesi ikawa kubwa sana.
Kwa kipindi hicho, nilikuwa nimeisababishia mfuko wa bima hasara ya takribani MILIONI 125.
Nilipoona mambo yamekuwa mazito, sikusubiri.
NIKAFUNGASHA VIRAGO VYANGU FASTA.
Nikaiuza ile dispensary kwa mtu mwingine, nikatembea zangu.
Baadaye nikaja kusikia kwamba kile kituo nacho kilifungwa nikawa most wanted.shukrani sana marehemu dada fortnatus raymond huyu alikuwa kitengo bima alinipambania kesi ikaishia hewani

Kisa cha mwisho iki siwezi kukisimulia kilikuwa upotevu wa dawa katika bohari kuu la dawa MSD .


Ila kwa sasa nimeachana na hiyo michezo nimekoswa koswa mara mbili kwenda jela.

Karibu na wewe ulete mkasa wako
Scare money don't make money
 
3FB39378-9DF8-4C3B-AD88-E6305D33E519.jpeg
 
Hapana..shida nilifanikiwa nipo mdogo sana wakati nina miaka 20 nilikuwa na pesa ndefu Sana.....kwahiyo watu wakawa na wivu na mafanikio sasa Kuna vifo vilitokea kwenye ukoo wetu nikaangushiwa lawama ndio maana ilifikia hatua wakati ule nina pesa sikuwa napenda kwenda kuangalia wagonjwa labda wawe wazazi wangu kwasababu isije unaenda kumuona ghafla Hali ikabadilika...kwahiyo hata nilipofilisika jamii ya kule kwetu wakaamini nilivunja mashart jambo linaloumiza mno
😅😅😅😅
 
Nimeandika mara nne nikafuta. Ngoja nikae kimya tu mambo yasiwe mengi nikaja kupewa Economic case. Ila itoshe tu kusema uhaba wa maji Dar Es Salaam ulikuwa FURSA kubwa sana kwangu miaka ya 2011-2013.
😅😅😅 Daah huu uzi ndio nauona leo 😅😅😅
 
Nilipigiwa simu na jamaa yangu kua Kuna washikaji(wateja wake) wanauza mawe ya dhahabu kama robo mfuko ule wa kg50, na yeye hana hela ya kuyanunua. Hivyo nichukue hela kwa tajiri yangu twende tukafanye nao biashara.

Nikachukua kama millioni 10, gari ya tajiri na nikamuomba bastola ake kama ulinzi wkt huo sijui hata inavyotumiwa, nika drive mpaka walipo nikakuta watu wa nne na mshikaji wangu wa 5.

Ile kuongea nao wakadai tuwape millioni 27, apo ndo nikajua huo mzigo una hela za kutosha. Huku na huku tukapunguziana mpaka million 18, hela sasa ikawa changamoto na ukizingatia hiyo ni saa saba usiku.

Ile kuwapanga jamaa wakagoma na mzigo wao wakautaka ili wasepe maana hela haitoshi, nikaona msinitanie nikajitoa akili maksudi(nikawa mkali). Jamaa wakachomoa mapanga na matusi juu, wakasema wao siyo wachimbaji hivyo mizigo wanaiiba katika mazingira magumu sana.

Nikapata picha kua hapa na Dili na watu gani?, kumbe nao ni vibaka tu nikachomoa bastola nikatishia yoyote atakae nisogelea nampeleka kuzimu, tukawaambia wachukue millioni 8 nyingine waijie asubui sana wakakubali kishingo upande baada ya jamaa yangu kuongea nao na ukizingatia ni wateja wake.

Tukaubeba mzigo, nikawasha gari mpaka kwa washikaji wenye vinu vya kutwangia mawe. Tukafanya process zote usiku huo, tukakamua kama gram 492. Asubui tukauza tukatoa gharama zote tukagawana faida na jamaa yangu.

Tajiri nikampelekea hela yake nikamwambia biashara ilishindikana, ilipofika usiku nikampigia simu askari mmoja jamaa yangu nikampanga anisindikize sehemu na achukue bunduki Kuna posho ya maana. Tukaenda baa Moja hivi siyo maarufu tukiwa watatu, nikamwambia jamaa yangu awapigie wale vibaka waijie hela zao. Wakaja tukawapa hela yao na mikwara mingi sana kua sisi wenyewe siyo wanyonge ni watu wa kazi na ukizingatia askari alikuepo amevaa nguo za kiraia na gobole lake mabegani.

Safari yetu ya kupata hela za kula ilianzia hapo na jamaa yangu.
😂😂😂 Biashara ilishindikana aisee!
 
Mimi kisa changu nikikielezea humu watu watanifahamu, ila enzi za mzee Magu tulikula economic case na kupelekwa mahakama ya uhujumu uchumi pale ubungo,mixer kutoka hadi kweny Gazeti la NIPASHE 2018...
enzi za magu tushashtakiwa mara mbili,2016, 2018!

tulikula kisago kweny Base ya wazee kule Mikocheni (Task force)... aisee yule Bora alivyokufa,alitaka watu wote wawe masikini,pesa wawe nazo wasukuma wenzie tu, watani zangu washamba sana......
Kesi yetu dhamana ilikuwa ya PESA CASH mamilioni au hati za nyumba....uzuri tuliweka wakili na wale madoni tulioshtakiwanao......baada ya hapo na kufirisika juu! Sasaivi nataka niwe chawa wa mama nipige pesa kimtindo!!!!
Nakukumbuka kipindi hicho ulikuwa unakaa Kili-mnjr kutoka bank flan hivi
 
Back
Top Bottom