Ni mimi tu au? Maji ya DAWASA ukinywa bila ya kuchemsha yanaumiza tumbo

Robert Heriel Mtibeli

JF-Expert Member
Joined
Mar 24, 2018
Posts
28,297
Reaction score
68,017
Habari za Majukumu!

Tangu mwaka huu uanze haya maji ya DAWASA nikiyanywa tumbo linaniuma. Zamani nilikuwa nakunywa ya kuchemsha yaani bila kuchemsha maji sinywi labda ninunue.

Mwaka jana nikajaribu kunywa maji ya bomba (DAWASA) bila kuchemsha nikaona hayana shida. Ni mpaka mwaka huu Januari ndio nakutwa na hali kama hii. Yaani nikiyanywa tuu tumbo linauma, ila nikinunua ya dukani au nikiyachemsha tumbo haliumi.

Hii maana yake nini? Ni mimi pekeangu?

Karibuni.
 
Mkuu, kunywa maji ya DAWASA bila kuyachemsha ni sawa na ku-commit suicide. Kuna wengine tuliacha hata hiyo kuchemsha tukifikiria wadudu waliomo ndani ya hayo maji ambao tunawameza hata kama wamekufa! Wazia kumeza hawa jamaa

 
Serikali inahimiza na kuelemisha chemsha maji au tia water guard? Unafikiri wanafanya kazi bure? Unataka wakuchemshie?
 
Miaka yote mamlaka za kiserikali na DAWASCO wenyewe wanasisitiza uchemshe maji kabla ya kuyanywa, sasa wewe jitie nunda ukuze typhoid na amoeba tumboni kwako, na hizi heka heka za bima zinazoendelea, ukikanyaga hospitali ndo utakiona cha mtema kuni. Wabongo acheni ubishi wa ki-uwendawazimu. Yaani wao wenyewe wanaoyachakata hayo maji wanawaambia mchemshe kabla ya kuyanywa, ila nyie mnajitia ununda, muishie kuumwa Typhoid sugu halafu muanze kuilaumu serikali tena.
 
Duh sikumbuki mara ya mwisho kunywa maji ya bomba mwaka gani baada ya 2022..mimi nanunua tu japo natumia pesa nyingi ila kunywa maji ya bomba(dawasco ) ten yalivyo na harufu ya madawa hapana.
 

Ni mwehu tu anaweza kunywa hayo. Maji bila kuchemsha, ngoja wendawazimu wenzako waje, Angalau ya Arusha, Dar es salaam na muingiliano wote wa sewage?
 
Nawakumbusha ndugu zangu Watz tumchemshe maji. Hali ni mbaya sana sasa. Vyanzo vya maji vingi viko kwenye hatari ya uchafuzi.
Wizara ya maji ilimwalika waziri mkuu kwenye kikao fulani chini ya waziri wa maji Juma Aweso, walikuwa wanajadili mabonde ya maji nchini. Hali sio nzuri kunywa maji bila kuchemsha.

Sent from my SM-A025F using JamiiForums mobile app
 
Wakuu leo nimeona mpenzi wangu kapiga picha yupo kwenye ndege na sijui anaelekea wapi kwasababu pia hajaniambia kuhusu hiyo safari yake. Hii kitu ishanichanganya... nifanyeje kuhusu huyu mwanamke?
Dawasa wana visima vya maji pia, mara nyingine hufungulia maji toka huko visimani.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…