Ni Mkatoliki 100% ila hizi ni sababu zangu za kwanini Sihudhurii na Sitohudhuria Jumuiya za kila Jumamosi....

BAHATI MBAYA HAKUNA NAMNA!

AMRI ZA KANISA LAKO ZINASEMAJE EBU TUTAJIE tuchambue kutoka kwenye mkataba wako na kanisa ambazo ni AMRI ZA KANISA!

Kingine nikushauri jifunze kupuuzia maneno! Wakati mwingi maneno huwa hayana maana kwa anayeyapuuza!

Waaache wachunguze wewe sali na imani yako jali maisha yako! Kama unalala chini pouw tu kwani nini, kama ni fukara si ni fukara tu kwani uongo! Ujue wakati mwingine kujikubali na hali yako ni tiba!

Wewe ni masikini halafu unataka watu wakuone tajili kweli?

Mimi nilihamia kwangu ikiwa pagala yaani juu HAKUNA kenchi wala bati, na niliona poa tu amani tele na watu walifurahi sana kuja kwangu kuliko kwingine, vikao vingi vya jumuiya walipendekeza wakutanie kwangu wakati palikuwa pagala tupu, palikuwa pa kimaskini sana!

Kila baada ya sala waliomba Mungu anijalie nikamilishe ujenzi! BAADAE NEEMA Ilikuja pagala langu ndiyo miongoni mwa ghorofa na nyumba bora mtaani!

Ushauri wangu! KUJISTUKIA NI UGONJWA WA AKILI MBAYA SANA! Waache waseme, watakuteta watatu au wanne lakini kumi watakuombea mafanikio! ViMANENO HAVIEPUKIKI NDUGU NDO JAMII YETU JIKUBALI

Uzuri jumuiya wakigundua maisha magumu hata michango utachanga KWA uwezo wako mpndwa!

1. Jikubali nyumba ya Kobe ni mgongo wake.
2. Masengenyo iwe motisha tambua kesho INA heli na nawe
3. Michango ya jumuiya haimfungi mtu jela toa KWA Moyo kadri ya uwezo
4. Fuata AMRI za kanisa lako maana ndiyo mkataba wa ushirika wako
5. Amini HAKUNA faida yoyote hata wakikusifia haiongezi kitu kwenye akaunti yako utabakia ni wewe ulivyo
6. Sali KWA imani yako
7. Shiriki kwa kuimarisha umoja
8. Hakuna asiyesemwa! Hata yesu walimchunguza kwao kuna zizi la ng'ombe wewe nani usichunguzwe ndugu!

SALI BHANA HAYO MENGINE NI KUTAFTA KUJIHALALISHIA UJINGA! ACHANA NAYO TAZAMA USO WA MUNGU! YA WANADAMU HAYAISHI
 
Sawa bro, Jumapili tukutane kwa Sinde tupige zetu 🍺🍻
Ratiba yangu ya Kesho Jumapili iko 'tight' sana kwani Asubuhi nitakuwa na some laundry fulani hivi ( ya Kimtindo ) na kama Malaika wataniambia niwahi ibada ya Kwanza kisha Saa 4 hadi Saa 7 Mchana kuna Kidemu fulani ( kimenitesa sana ila kimejaa katika 18 yangu ) nataka nikakipige 'hat trick' kabla ya Moses Phiri kupiga yake kwa Mkapa Saa 11 na Saa 10 nitakuwa ama Uwanjani au katika Ukumbi Mmoja kuiangalia 'Mbungi' ya Yanga SC na Simba SC pale Estadio Du Mkapa.
 
Nilichogundua kupitia haya malalamiko yako; Wewe ni kajitu fulani hivi anti social na kasiko penda kuchangamana na watu! Ni kajitu fulani hivi kenye wivu kupindukia! Sijui mke wako amemsifia jirani yako mnaye sali naye Jumuiya kuwa ni hendsam kuliko wewe, roho ikakuuma!!

Unaishi katika mazingira machafu, nyumba ya hali ya chini kuliko wana jumuiya wenzako, hivyo unajishtukia wana jumuiya wenzako wakija kusali kwako, utaonekana wewe ni mtu wa hali ya chini.

Pia unaonekana ni kajitu fulani hivi kafupi na kabishi ka kila kitu! Unaishi maisha ya kuunga unga, hata kama wewe ni genius uliyesoma SAUT! Maana unalalamikia michango ya elfu 5 tu ya kulitegemeza Kanisa la Mungu! Huku ukiombwa elfu 50 na mchepuko, unatuma na ya kutolea!

Mwisho kabisa unaonekana una itikadi za kiukawa ukawa! Halafu unashangilia timu mbovu ya simba, ambayo kila siku ni kuwalalamikia tu wachezaji, kocha Matola, na CEO Barbara! Hivyo akili yako imevurugwa kiasi cha kuhamishia malalamiko yako Jumuiyani.

Ushauri; hujalazimishwa kwenda kusali kwenye Jumuiya. Na hata usipozikwa kwa kuombewa, who cares!!
 
Amri ya Kanisa inasema SAIDIA KANISA KATOLIKI KWA ZAKA..
hizo mambo zingine zinatoka wapi?
Wenzetu ulaya hata hiyo sadaka ya katikati ya misa hawatoi.. Kwa sababu Zaka ina fanya kila kitu..

Huku michango michango michango
 
😁😁😁 mwanajumuhiya nakutzama tu
 
Nasikitika umechelewa kujua kuwa JamiiForums nzima Mtu Masikini, Duni na asiye na Elimu Kubwa na yupo yupo tu ni Mimi GENTAMYCINE.

Hongera nyingi Kwako kwa kuwa Mtu Tajiri, Msomi na unayeishi Ushuani kwa Tanzania na Washington DC kwa huko Marekani.
 
Asipo ufuata huu ushauri, basi ahamie tu Kanisa la Masanja Mkandamizaji. Huko hakuna michango na pia hakuna ibada za Jumuiya.
 
Mwamba shida anapenda sana kujipa umuhimu ukute yeye ndo huangalia leo mwenyekiti kaja na gari gani ,ukute ndo kanachunguza wenzake akija hapa full majivuno utadhani ruwaichi anaenda kuripoti kwake
 
Kwa kweli michango ya hili kanisa ni mingi sana hadi imekuwa kero.Mbaya zaidi ukichunguza hiyo michango inakoenda utaona haina maana kanisa ya kutoa michango
Kwani huwa mnashikiwa bunduki ili mtoe hiyo michango? Malalamiko mengine hayana tija!Halafu usiseme uongo hadharani! Hakuna mchango kwenye Kanisa Katoliki usiojulikana matumizi yake.

Kwa taarifa yako tu hata ile sadaka ya kawaida ya kila Dominika, ukiulizia mgawanyo wa matumizi yake; utaambiwa.

Dawa ya kukataa michango, kusali jumuiya ndogondogo, na taratibu nyingine za Kikatoliki usizo furahishwa nazo, ni kuhama tu Kanisa, kama walivyofanya akina Martin Luther, na wengineo wengi, badala tu ya kulalamika.
 
Tatizo ni Jumuia kupewa mamlaka Makubwa wakati zinaongozwa na watu wa kawaida kitabia, wa kawaida kiimani, wa kawaida kimwenendo, wasio na skills za Uongozi nk.
 
Kama ungekua una akili japo chembe usingeweza kubeza umuhimu wa ibada za jumuia ndogondogo.

Watu wanasema tu ila mimi nimeshuhudia mtu akizikwa na serikali ya mtaa. Hata walokole hawakujihusha nae.
Asikuambie mtu inauma sana kuona ndugu yako anazikwa kama mzoga wa mbwa aliyegongwa barabarani
 
Kweli kabisaa Mkuu mimi nahisigi huyu jamaa ni Trans-gender au Ambiguous Genitalia.
 
Ukilijua kanisa katoliki lenyewe lilivyo, hasa hasa huko makao makuu, Vatican sidhani kama na uiatoliki wenyewe utaendelea kuwa muumini wake. Cha msingi tu ni imani kwa Mungu, kufanya ibada na kutoa sadaka.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…