Ni Mkatoliki 100% ila hizi ni sababu zangu za kwanini Sihudhurii na Sitohudhuria Jumuiya za kila Jumamosi....

Hana ndugu huyo mtu? Unatetea ujinga tu
 
Wapi Mungu amesema mtu huyo atengwe? Mnajigeuz watoa hukumu sio?
 
Nakubaliana na wewe💯
 
Wewe ni mwenyekiti au Mwekahazina mla michango?
 
Hamnaga fahari kwenye kuzikwa hayo mengine mmejiwekea tu kichwani mwenu
 
Michango ya jumuiya makosa mi naona ni ya kanisa.
Maana huko ndo inakotokea... ila kusema kweli michango inachosha.
Mi binafsi siendi jumuiya uvivu wakuamka saa 12, ukichanganya na majungu , ukienda unatwishwa majukumu mazito! Hujadaiwa mchango daaah!!!
Naishia tu kanisani maana kule hamna hata atakae kukaba
Na hapo ni misa ya 2 maana ya kwanza unakutana na kwanzia mwenyekiti wa jumuiya,katibu sijui nani wa WAWATA mara sijui VIWAWA
EEH
 
kiufupi jumuiya zimeanzishwa ili kuongeza kipato cha sadaka mkamuliwe juma pili kanisani alaff jumamosi au juma tano mnakamuliwa tena mkikutana alaf kero ni pale wanataka kusalia ndani kwako mm nawakaribisha nje tu.
nakumbuka kuna siku kulikua na hali ya mvua nkaandaa vitu kwenye garden wakaja mm nkaingia ndani ghafla mvua ikaanza nkajifungia kimya ilipokata na muda umesogea nkatoka nkawaambia kwa leo mambo yashaharibika wakataka kusalia ndani nakawagomea kwanza ndan kwangu hakuna nafasi bas kile kitu wakaenda sema hadi kwa mchungaji na ndo mwanzo na mwisho kwenda jumuiya wakija kwangu sifungui asubuh wanakuta kimyaaaaaaaaaa tena jumamos ndo kabisaaa naamka saa tano
 
Gentamicin Sisi wengine unaotuelezea hayo ya Jumuia Yako hayatuhusu.Wengine sio Wakatoliki.Ushahuri wangu,mambo hayo ni Bora ukayapeleke kwenye Kigango au Parokiani Kwa ufumbuzi hapa hutopata suruhisho na unatuchanganya tusiokuwa Wakatoliki wenzako.
 
Na ndo maana nimeandika hapa pia. Am not a Catholic lakini ni Mkristo. Kuandika hapa haimaanishi sitaki mabadiliko lakini huu ni mjadala ambao tunaufanya ili ubadilishe fikra zetu. Kama kuna jambo tunakosea ndo tuandike hapa ikiwa ni platform nzuri ya kufikiwa na watu wengi. Kuna atakaesoma hapa na akaona aanzishe au alete mawazo ya kubadilika katika jumuiya yake. Na kuna atakaeona ni upuuzi na akaacha. It all begins with you. Sio every time tunatakiwa kureact negatively...be blessed. And get a lemon too.
 
Elewa miaka ya nyuma kanisa lilikuwa almost fully supported na wazungu sasa mambo yamebadilika mambo yote yanayofanyika lazima pesa itoke kwa waumini.
Kwa hiyo kama hutaki kuchangia mambo ya kanisa unataka nani atoe pesa zake kwa ajili yako?
Nakushauri nenda Mombasa kuna maisha ya bure bure hakuna atakaye kuuliza wewe kutoa pesa yako kamwe.
 

Hiyo ni juu yako mwenyewe.Kuchagua kunyoa au kusuka .Halafu hawajakulazimishi, na wala wewe ukiacha si kwamba jumuiya zitakufa.
 
Ujawai kosa sabb ila muda mwingi unautumia kusisaka Papuchi [emoji3][emoji3][emoji3]
 
Bahati nzuri Kanisa Katoliki lina Mapadre tu. Hao Wachungaji wanapatikana KKKT, Anglikana, nk.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…