Ni Mkatoliki 100% ila hizi ni sababu zangu za kwanini Sihudhurii na Sitohudhuria Jumuiya za kila Jumamosi....

Ni Mkatoliki 100% ila hizi ni sababu zangu za kwanini Sihudhurii na Sitohudhuria Jumuiya za kila Jumamosi....

Ratiba yangu ya Kesho Jumapili iko 'tight' sana kwani Asubuhi nitakuwa na some laundry fulani hivi ( ya Kimtindo ) na kama Malaika wataniambia niwahi ibada ya Kwanza kisha Saa 4 hadi Saa 7 Mchana kuna Kidemu fulani ( kimenitesa sana ila kimejaa katika 18 yangu ) nataka nikakipige 'hat trick' kabla ya Moses Phiri kupiga yake kwa Mkapa Saa 11 na Saa 10 nitakuwa ama Uwanjani au katika Ukumbi Mmoja kuiangalia 'Mbungi' ya Yanga SC na Simba SC pale Estadio Du Mkapa.
Utoto bado mwingi sana ...una ratiba ya kwenda kanisani hapo hapo una ratiba ya kugonga demu

No wonder huwezi jua umuhimu wa JNNK
 
Nimecheka mno. Naona umeamua kunipiga Dongo Kiana. Haya bhana ila Jumuiya zenu sihudhurii ng'o na Mbinguni kwa Mungu Baba nitafika tu.
We mtu, hivi unajua maneno yako ya vicheshi yamesababisha maumivu makali ya mbavu za watu!.?

Utaweza kutulipa tulioumizwa na maneno yako haya Kwa kucheka mpaka kuuma Kwa mbavu?
 
Amri ya Kanisa inasema SAIDIA KANISA KATOLIKI KWA ZAKA..
hizo mambo zingine zinatoka wapi?
Wenzetu ulaya hata hiyo sadaka ya katikati ya misa hawatoi.. Kwa sababu Zaka ina fanya kila kitu..

Huku michango michango michango
Mwongo mkubwa wewe. Tumeishi kule na sadaka hizo na michango vipo. Umechoka kuwa mkatoliki hama wala hakuna atakayejali.
 
Michango imekuwa mingi sana Kanisa Katoliki..

Mbaya zaidi ukikaa karibu na hao makuhani unaweza acha kutoa kabisa..

Kuna sadaka ya kawaida ya jumuiya
Kuna tegemeza jimbo
Kuna tegemeza parokia
Kuna mavuno
Kuna zaka
Kuna mchango wa ujenzi
Kuna mchango wa UWAKA/ WAWATA
kuna mchango wa gari la paroko

Michango ni bandika bandua
Wewe umechangia upi katika hiyo uliyo itaja hapo.
 
Njia ya kwenda mbinguni ni nyembamba na wachache wanaiona ! Aidha, kwenye msafara wa mamba na kenge wamo.
 
Unaweza kuwa na point, ila uko totally wrong kwa kuyaleta huku badala uwapelekee wahusika, (M/Kiti wa Jumuiya ) ama paroko wako kabisa.
Pili, Kanisa Katoliki haliwezi kubadili utaratibu wake eti sababu ya mtu au watu wachache wazembe na wavivu na ma cowards kushindwa kuhudhuria jumuiyani na hivyo kutafuta visababu uchwara ambavyo vinaweza kupatikana popote kwenye kikundi cha watu.
Tatu, wewe ni coward na Popoma mkubwa [emoji1787][emoji852][emoji4]
Umetumia kigezo gani kumuita mtu Coward?...Hofu zako za kidini na sheria za kanisani acha huko huko kanisani, Huku ni jukwaa huru la kutoa maoni... utofauti wa mitazamo ya kiimani sio kigezo cha kukosoa mawazo ya mtu kwa kigezo cha kanisa! ...
 
Nakuelewa kwanini umeamua kufanya uchaguzi huu. Mungu aturehemu sana. Watu hatujui kazi ya jumuiya kwa ujumla. Jumuiya ilianzia kwa mitume kwenye Matendo ya mitume 2:yote. Ukisoma mstari wa 46 utaelewa kazi ya jumuiya. Na kiukweli matendo yote ukiisoma utaelewa kazi ya jumuiya.

Sasa jumuiya saivi usipoenda huzikwi, hawakujali, hawana muda na wewe, haupati msaada. Kinachoniuma kuna bibi mmoja tuko nae huku. Anasali jumuiya ya kanisa fulani. Kuna muda anaweza kulala na njaa hana chochote. Hio ni story nilioikuta huku.

And too bad kazungukwa na wanajumuiya yake plus wakristo. Sasa ni Kristo yupi tunaemhubiri. Nilitegemea jumuiya tupeleke misaada mtaani kwa watu wenye hali ngumu, tuende kwenye mahospitali, vituo vya yatima, kwa wajane ili kuupeleka upendo wa Kristo kwa matendo.

Lakini cha kuumiza unaweza kuta katika jumuiya kuna mjane na hana maisha. Kuna yatima katika jumuiya kakosa hela ya kwendea shule na mlezi wake hali ngumu..shule anasitisha na bado yuko kwenye jumuiya ambayo ndani yake kuna mtu mwenye fedha. Show me Imani yako bila matendo, nikuoneshe Imani iliyo kwenye matendo.

If we are keen tutakosa mbingu wakristo almost wote. Hata Isaya nadhani aliandika dini ya kweli kabisa ni kwenda kutembelea yatima, wajane, kuwavisha maskini nguo, kuwapa chakula. Lakini nachoona saiv ni maigizo tu. Tujifikirie upys na kuchagua mambo sahihi ya kufanya.
UMEMALIZA! 📌📌📌📌
 
Ukishajua uwepo wa Mungu ni hadithi ya utakatifu wa kufikirika isiyo na uthibitisho, kimsingi uongo wa kutungwa na watu tu, habari kama hizi hazitakusumbua.
 
If i am going to be honest with you ,in my own humble opinion without being sentimental of course, without offending anyone who thinks differently from my own point of view,but also by looking into this matter in distinctive perspective ,i would like to say i have nothing to say
 
Kwani huwa mnashikiwa bunduki ili mtoe hiyo michango? Malalamiko mengine hayana tija!Halafu usiseme uongo hadharani! Hakuna mchango kwenye Kanisa Katoliki usiojulikana matumizi yake.

Kwa taarifa yako tu hata ile sadaka ya kawaida ya kila Dominika, ukiulizia mgawanyo wa matumizi yake; utaambiwa.

Dawa ya kukataa michango, kusali jumuiya ndogondogo, na taratibu nyingine za Kikatoliki usizo furahishwa nazo, ni kuhama tu Kanisa, kama walivyofanya akina Martin Luther, na wengineo wengi, badala tu ya kulalamika.
Hao sio wakatoliki,niwahuni tu wameamua kuandika upuuzi tu.

Mtu anakuambia michango ni mingi anataja, Mavuno parokia na tegemeza Jimbo, ujenzi wa kanisa na sadaka shilingi miatano yake anayotoa jumamosi kwenye Jumuiya na Kanisani.

Mkristo mkatoliki mwenye akili hawezi kulalamika kwaajili ya kutoa mchango kwaajili ya ujenzi wa kanisa.
 
1. Jumuiya kumekuwa ni sehemu za Majungu.

2. Jumuiya imekuwa ni sehemu za Kuchunguzana Kimaisha.

3. Jumuiya imekuwa ni sehemu ya Masutano.

4. Jumuiya imekuwa ni sehemu ya Wanaume Kutongoza na Wanawake kutafuta wa Kuwachapa Nao ( Kuwabandua )

5. Jumuiya imekuwa ni sehemu ya Kutishana kuwa kama hauhudhurii basi Ukifa ( Ukifariki ) Kanisa Katoliki halitokuombea ukiwa Jenezani Kwako.

6. Jumuiya imekuwa ni sehemu ya kila Siku kuja na Michango isiyo na Kichwa wala Miguu.

7. Jumuiya imekuwa ni Gulio Kuu la kila aina ya Unafiki unaoujua na usioujua hapa duniani.

Halafu Wewe Mwenyekiti, Katibu na Mweka Hazina wa Jumuiya yangu hivi mnavyonitishia kuwa kama nisipohudhuria Jumuiya Nikifa hamtoniombea mmeshazungumza na Baba Mungu na akawaambieni kuwa ataanza Kunitanguliza Mimi Kaburini kabla yenu? Wapuuzi wakubwa nyie.

Je, mnavyong'ang'ania Kutoniombea GENTAMYCINE pale Nikifa je, ile Siku ninazaliwa mlikuja Agha Khan Hospital mbele ya Sister Brendah na Sister Aghata waliohakikisha Nazaliwa vyema na salama Kuniombea? Wapuuzi wakubwa nyie.

Na nani aliyewadanganyeni kuwa Imani ya Ukatoliki inapimwa kwa Kuja Kwake ( Kuhudhuria ) katika Jumuiya za Kikatoliki kila Jumamosi kama ya hii leo?

Nilichoamua tu na najua hata Mwenyezi Mungu ananibariki nacho ni kwamba nitajitahidi Kuhudhuria Ibada zote za kila Jumapili ( hasa Misa yangu pendwa ya Kwanza ) na kutoa Sadaka na Michango ya Kikanisa kama tu nitakuwa Nimebarikiwa na Uchumi kwa wakati huo na kama sina najua hata Mola / Maulana nae atajua na hatonichukia au kuwa na Usununu ( Kinyongo ) nami.

Nawatakieni nyote Jumuiya njema!!!!
Genta kama JF humu una majungu huko kwenye jumuia si ndio balaa tupu
 
Tatizo ni Jumuia kupewa mamlaka Makubwa wakati zinaongozwa na watu wa kawaida kitabia, wa kawaida kiimani, wa kawaida kimwenendo, wasio na skills za Uongozi nk.
Unaweza kuyataja hayo mamlaka makubwa unayo sema??.
 
Ukilijua kanisa katoliki lenyewe lilivyo, hasa hasa huko makao makuu, Vatican sidhani kama na uiatoliki wenyewe utaendelea kuwa muumini wake. Cha msingi tu ni imani kwa Mungu, kufanya ibada na kutoa sadaka.
Acha umbeaumbea mkuu, kama unajuwa siuwekewazi hapa iliuokoe wenzako.
 
Nakuelewa kwanini umeamua kufanya uchaguzi huu. Mungu aturehemu sana. Watu hatujui kazi ya jumuiya kwa ujumla. Jumuiya ilianzia kwa mitume kwenye Matendo ya mitume 2:yote. Ukisoma mstari wa 46 utaelewa kazi ya jumuiya. Na kiukweli matendo yote ukiisoma utaelewa kazi ya jumuiya.

Sasa jumuiya saivi usipoenda huzikwi, hawakujali, hawana muda na wewe, haupati msaada. Kinachoniuma kuna bibi mmoja tuko nae huku. Anasali jumuiya ya kanisa fulani. Kuna muda anaweza kulala na njaa hana chochote. Hio ni story nilioikuta huku.

And too bad kazungukwa na wanajumuiya yake plus wakristo. Sasa ni Kristo yupi tunaemhubiri. Nilitegemea jumuiya tupeleke misaada mtaani kwa watu wenye hali ngumu, tuende kwenye mahospitali, vituo vya yatima, kwa wajane ili kuupeleka upendo wa Kristo kwa matendo.

Lakini cha kuumiza unaweza kuta katika jumuiya kuna mjane na hana maisha. Kuna yatima katika jumuiya kakosa hela ya kwendea shule na mlezi wake hali ngumu..shule anasitisha na bado yuko kwenye jumuiya ambayo ndani yake kuna mtu mwenye fedha. Show me Imani yako bila matendo, nikuoneshe Imani iliyo kwenye matendo.

If we are keen tutakosa mbingu wakristo almost wote. Hata Isaya nadhani aliandika dini ya kweli kabisa ni kwenda kutembelea yatima, wajane, kuwavisha maskini nguo, kuwapa chakula. Lakini nachoona saiv ni maigizo tu. Tujifikirie upys na kuchagua mambo sahihi ya kufanya.
Kama nawewe nimkatoliki naumeona mazingira kama hayo umechukua hatuagani, umezungumzia hilojambo kwenye Jumuiya? amaunalileta huku nawewe uonekane umeandika.
Taratibu zakufuata ukiona jambo kama hilo umezifuata?
Kama umewaeleza wanajumuiya wenzako ama viongozi wajumuiya wakapuuza je, ulienda kumueleza paroko katika parokia yenu kwamba kuna muhitaji katika Jumuiya yenu ambae kwa ngazi ya Jumuiya hamnauwezo wa kumsaidia?.
 
Back
Top Bottom