Nakuelewa kwanini umeamua kufanya uchaguzi huu. Mungu aturehemu sana. Watu hatujui kazi ya jumuiya kwa ujumla. Jumuiya ilianzia kwa mitume kwenye Matendo ya mitume 2:yote. Ukisoma mstari wa 46 utaelewa kazi ya jumuiya. Na kiukweli matendo yote ukiisoma utaelewa kazi ya jumuiya.
Sasa jumuiya saivi usipoenda huzikwi, hawakujali, hawana muda na wewe, haupati msaada. Kinachoniuma kuna bibi mmoja tuko nae huku. Anasali jumuiya ya kanisa fulani. Kuna muda anaweza kulala na njaa hana chochote. Hio ni story nilioikuta huku.
And too bad kazungukwa na wanajumuiya yake plus wakristo. Sasa ni Kristo yupi tunaemhubiri. Nilitegemea jumuiya tupeleke misaada mtaani kwa watu wenye hali ngumu, tuende kwenye mahospitali, vituo vya yatima, kwa wajane ili kuupeleka upendo wa Kristo kwa matendo.
Lakini cha kuumiza unaweza kuta katika jumuiya kuna mjane na hana maisha. Kuna yatima katika jumuiya kakosa hela ya kwendea shule na mlezi wake hali ngumu..shule anasitisha na bado yuko kwenye jumuiya ambayo ndani yake kuna mtu mwenye fedha. Show me Imani yako bila matendo, nikuoneshe Imani iliyo kwenye matendo.
If we are keen tutakosa mbingu wakristo almost wote. Hata Isaya nadhani aliandika dini ya kweli kabisa ni kwenda kutembelea yatima, wajane, kuwavisha maskini nguo, kuwapa chakula. Lakini nachoona saiv ni maigizo tu. Tujifikirie upys na kuchagua mambo sahihi ya kufanya.