Ni Mkatoliki 100% ila hizi ni sababu zangu za kwanini Sihudhurii na Sitohudhuria Jumuiya za kila Jumamosi....

Ni Mkatoliki 100% ila hizi ni sababu zangu za kwanini Sihudhurii na Sitohudhuria Jumuiya za kila Jumamosi....

Dini ni kivuli cha kutawaliwa hao viongozi wenu wapo chini ya utawala!

Baadhi yenu kufunguka itawachukua muda sana haswa hivi vichwa vyetu vya kiafrika mtaliwa mno..
Nani ambaye hatawaliwi?
 
The only easy day was yesterday,life is meaningless brothers and sisters,just love your neiba,kusali na wenzako kijumuiya ni furaha,kama kuna changamoto yeyote kwenye jumuiya yako!! wewe kuwa shujaa wa kuleta mabadiliko na sio malalamiko! Shujaa akimbii bali ukimbiliwa.

Wengine tupo mbali na nyumbani tukitafuta amani ya wenzetu,tunatamani tupate angalau nafasi ya kufurahi na majirani zetu,ila wakati hauruhusu! Upweke tu ndio unatubusu! Uso wa MUNGU unaonekana kwa majirani zako kuliko kanisani kwako.
 
Kuna wakati nilitafakari kurudi jumuia. Nilimtafuta mwenyekiti nikamweleza nia yangu.

Akaniambia kwa kuwa alishanifuta kwenye register, basi niende akanipe maelekezo.

Maelekezo yenyewe alimuita Katibu ambaye alikuja na karatasi yenye list ya michango ya miaka mitatu. Kila mwaka ni laki na nusu, kwa hiyo, nilipe laki 4 na nusu ili niweze kuendelea na Jumuia.

Nilimwambia sawa. Sikutekeleza na jumuia siendi, maana sikumwelewa kabisa
 
Unaweza kuwa na point, ila uko totally wrong kwa kuyaleta huku badala uwapelekee wahusika, (M/Kiti wa Jumuiya ) ama paroko wako kabisa.
Pili, Kanisa Katoliki haliwezi kubadili utaratibu wake eti sababu ya mtu au watu wachache wazembe na wavivu na ma cowards kushindwa kuhudhuria jumuiyani na hivyo kutafuta visababu uchwara ambavyo vinaweza kupatikana popote kwenye kikundi cha watu.
Tatu, wewe ni coward na Popoma mkubwa 🤣☹😊
 
Kuna wakati nilitafakari kurudi jumuia. Nilimtafuta mwenyekiti nikamweleza nia yangu.

Akaniambia kwa kuwa alishanifuta kwenye register, basi niende akanipe maelekezo.

Maelekezo yenyewe alimuita Katibu ambaye alikuja na karatasi yenye list ya michango ya miaka mitatu. Kila mwaka ni laki na nusu, kwa hiyo, nilipe laki 4 na nusu ili niweze kuendelea na Jumuia.

Nilimwambia sawa. Sikutekeleza na jumuia siendi, maana sikumwelewa kabisa
Oteee oteee
 
Jumuiya yako sio jumuiya ya wengine semea yako. Yetu ina umoja upendo na mshikamano kuwa pamoja kwenye shida na raha
 
BAHATI MBAYA HAKUNA NAMNA!

AMRI ZA KANISA LAKO ZINASEMAJE EBU TUTAJIE tuchambue kutoka kwenye mkataba wako na kanisa ambazo ni AMRI ZA KANISA!

Kingine nikushauri jifunze kupuuzia maneno! Wakati mwingi maneno huwa hayana maana kwa anayeyapuuza!

Waaache wachunguze wewe sali na imani yako jali maisha yako! Kama unalala chini pouw tu kwani nini, kama ni fukara si ni fukara tu kwani uongo! Ujue wakati mwingine kujikubali na hali yako ni tiba!

Wewe ni masikini halafu unataka watu wakuone tajili kweli?

Mimi nilihamia kwangu ikiwa pagala yaani juu HAKUNA kenchi wala bati, na niliona poa tu amani tele na watu walifurahi sana kuja kwangu kuliko kwingine, vikao vingi vya jumuiya walipendekeza wakutanie kwangu wakati palikuwa pagala tupu, palikuwa pa kimaskini sana!

Kila baada ya sala waliomba Mungu anijalie nikamilishe ujenzi! BAADAE NEEMA Ilikuja pagala langu ndiyo miongoni mwa ghorofa na nyumba bora mtaani!

Ushauri wangu! KUJISTUKIA NI UGONJWA WA AKILI MBAYA SANA! Waache waseme, watakuteta watatu au wanne lakini kumi watakuombea mafanikio! ViMANENO HAVIEPUKIKI NDUGU NDO JAMII YETU JIKUBALI

Uzuri jumuiya wakigundua maisha magumu hata michango utachanga KWA uwezo wako mpndwa!

1. Jikubali nyumba ya Kobe ni mgongo wake.
2. Masengenyo iwe motisha tambua kesho INA heli na nawe
3. Michango ya jumuiya haimfungi mtu jela toa KWA Moyo kadri ya uwezo
4. Fuata AMRI za kanisa lako maana ndiyo mkataba wa ushirika wako
5. Amini HAKUNA faida yoyote hata wakikusifia haiongezi kitu kwenye akaunti yako utabakia ni wewe ulivyo
6. Sali KWA imani yako
7. Shiriki kwa kuimarisha umoja
8. Hakuna asiyesemwa! Hata yesu walimchunguza kwao kuna zizi la ng'ombe wewe nani usichunguzwe ndugu!

SALI BHANA HAYO MENGINE NI KUTAFTA KUJIHALALISHIA UJINGA! ACHANA NAYO TAZAMA USO WA MUNGU! YA WANADAMU HAYAISHI
Mungu akubariki kwa somo na ushuhuda Mzuri.
 
1. Jumuiya kumekuwa ni sehemu za Majungu.

2. Jumuiya imekuwa ni sehemu za Kuchunguzana Kimaisha.

3. Jumuiya imekuwa ni sehemu ya Masutano
Haya yoote umesema ukweli mkuu wala haujadanganya chochote, anaepinga na apinge ila ukweli umewafikia
5. Jumuiya imekuwa ni sehemu ya Kutishana kuwa kama hauhudhurii basi Ukifa ( Ukifariki ) Kanisa Katoliki halitokuombea ukiwa Jenezani Kwako.

6. Jumuiya imekuwa ni sehemu ya kila Siku kuja na Michango isiyo na Kichwa wala Miguu.

7. Jumuiya imekuwa ni Gulio Kuu la kila aina ya Unafiki unaoujua na usioujua hapa duniani.
Yaan ni ukweli na nusu mkuu yote haya nmeyaona, Jumuiya ilikua zamani miaka ya nyuma kulikua hakuna hizi habari za mamichango ya ajabu ajabu tulikua tunafurahia jumuiya lakini siku hizi jumuiya zimekua chungu mno michango haiishi

Yaan jumuiya kuna makaunta buku ya mamichango ya kila aina mpaka una data michango mfululizo tena sio kwamba ni michango ya hiari useme km nnayo ntatoa sina siwezi kutoa bali ni lazima uchangie na unakumbushwa deni kila jumuiya kwamba una deni
 
Ratiba yangu ya Kesho Jumapili iko 'tight' sana kwani Asubuhi nitakuwa na some laundry fulani hivi ( ya Kimtindo ) na kama Malaika wataniambia niwahi ibada ya Kwanza kisha Saa 4 hadi Saa 7 Mchana kuna Kidemu fulani ( kimenitesa sana ila kimejaa katika 18 yangu ) nataka nikakipige 'hat trick' kabla ya Moses Phiri kupiga yake kwa Mkapa Saa 11 na Saa 10 nitakuwa ama Uwanjani au katika Ukumbi Mmoja kuiangalia 'Mbungi' ya Yanga SC na Simba SC pale Estadio Du Mkapa.
🤣🤣🤣wew jamaa
 
Mimi nasikia nadaiwa viwawa huko hata sielewi. Tena kibabe na kilazima. Katika suala la michango hapana aisee. Too much. Sihudguriagu hata ikiwa inasali kwetu. Wengi naonaga wanafiki tu. Kama mtu siongei nar naenda kusali Mungu si ataniadhibu kwa unafki?
Ila kweny harusi unachangia vizur na Vijora vya laki laki🤣🤣🤣
 
Michango imekuwa mingi sana Kanisa Katoliki..

Mbaya zaidi ukikaa karibu na hao makuhani unaweza acha kutoa kabisa..

Kuna sadaka ya kawaida ya jumuiya
Kuna tegemeza jimbo
Kuna tegemeza parokia
Kuna mavuno
Kuna zaka
Kuna mchango wa ujenzi
Kuna mchango wa UWAKA/ WAWATA
kuna mchango wa gari la paroko


Michango ni bandika bandua
Sasa unataka hela zitoke wapi?
 
1. Jumuiya kumekuwa ni sehemu za Majungu.

2. Jumuiya imekuwa ni sehemu za Kuchunguzana Kimaisha.

3. Jumuiya imekuwa ni sehemu ya Masutano.

4. Jumuiya imekuwa ni sehemu ya Wanaume Kutongoza na Wanawake kutafuta wa Kuwachapa Nao ( Kuwabandua )

5. Jumuiya imekuwa ni sehemu ya Kutishana kuwa kama hauhudhurii basi Ukifa ( Ukifariki ) Kanisa Katoliki halitokuombea ukiwa Jenezani Kwako.

6. Jumuiya imekuwa ni sehemu ya kila Siku kuja na Michango isiyo na Kichwa wala Miguu.

7. Jumuiya imekuwa ni Gulio Kuu la kila aina ya Unafiki unaoujua na usioujua hapa duniani.

Halafu Wewe Mwenyekiti, Katibu na Mweka Hazina wa Jumuiya yangu hivi mnavyonitishia kuwa kama nisipohudhuria Jumuiya Nikifa hamtoniombea mmeshazungumza na Baba Mungu na akawaambieni kuwa ataanza Kunitanguliza Mimi Kaburini kabla yenu? Wapuuzi wakubwa nyie.

Je, mnavyong'ang'ania Kutoniombea GENTAMYCINE pale Nikifa je, ile Siku ninazaliwa mlikuja Agha Khan Hospital mbele ya Sister Brendah na Sister Aghata waliohakikisha Nazaliwa vyema na salama Kuniombea? Wapuuzi wakubwa nyie.

Na nani aliyewadanganyeni kuwa Imani ya Ukatoliki inapimwa kwa Kuja Kwake ( Kuhudhuria ) katika Jumuiya za Kikatoliki kila Jumamosi kama ya hii leo?

Nilichoamua tu na najua hata Mwenyezi Mungu ananibariki nacho ni kwamba nitajitahidi Kuhudhuria Ibada zote za kila Jumapili ( hasa Misa yangu pendwa ya Kwanza ) na kutoa Sadaka na Michango ya Kikanisa kama tu nitakuwa Nimebarikiwa na Uchumi kwa wakati huo na kama sina najua hata Mola / Maulana nae atajua na hatonichukia au kuwa na Usununu ( Kinyongo ) nami.

Nawatakieni nyote Jumuiya njema!!!!
Kumbe wakati mwingine data zinajiwasha zenyewe. Nikajua ni kujizima tu
 
Back
Top Bottom