Hii movie nakumbuka enzi tunaiangalia ilikua n mkanda wa VHS tena tukikodisha.
Uncle hapendi tuazime Mikanda ya watu,hiyo siku akakuta tunaangalia nae akakaa chini,toka mwanzo hadi mwishoni
ilifika mahali sebuleni wote kimya kila mtu anavuta makamasi kimya kimya asisikike analia, Tunaemuogopa uncle yakamshinda machozi yakawa yanamtoka akainuka akaondoka nnje tukawa tunamskia analia LIVE LIVE.
Aunt akaondoka na njia yake kulia anapojua,tuliobaki tukaondoka usiku ule hatukufanya maombi ya usiku kila mtu alipita na njia yake ni kama Vile Movie ilienda tonesha kidonda cha kila mtu.
Kwa uncle nadhani ni sababu MAMA yake (bibi) alikua kafariki so nikaelewa movie ilimkumbusha mama ake.
ila ile Movie kama unaiangalia mara ya kwanza na Una Moyo,chozi lazima Umwage yani no discusion REMEMBER YOUR MOTHER story inagusa bwana.