Ni msanii gani wa Comedy unaona kabisa hamnaga kazi ila ndo hivyo tu

Ni msanii gani wa Comedy unaona kabisa hamnaga kazi ila ndo hivyo tu

Chukua list yote ya Cheka Tu & Watu Baki, watoe TX Dullah, Madevu: hawa wanafanya vizuri kotekote kwenye kuigiza (skit) na stand-up comedy, wana story na punchline zitakazokufanya ucheke.

Wapo wengi wanajitahidi ila kwenye angle ya uigizaji zaidi kuliko stand-up comedy:

1. Eliud: yupo vizuri sana kwenye uigizaji kuliko stand-up comedy ila bado anaweza kujiboresha zaidi.

2. Jol Master: tatizo lake kubwa ana mapepe sana awapo jukwaani na maudhui yake kwa asilimia kubwa ni ngono na ndiyo tasnia nzima ya comedy imelalia upande huo, mpaka wakina TX Dullah wanaanza kupita na huo upepo kwenye skit zao. Wengine kwenye skit zao wanahamasisha mpaka ubakaji kwa kigezo cha uchekeshaji bila kujua.

***Leonardo: kipindi anaanza alikuwa anafanya vizuri sana kwenye stand-up comedy, sasa hivi itakuwa kashalewa sifa. Kwenye uigizaji (skit) uhusika wake ni kama anafanya maudhui kwaajili ya watoto.

***Kipotoshi pale Watu Baki naye anajitahidi sana kusukuma gurudumu yupo na dogo mwingine akipanda jukwaani unatamani asishuke.

Wanaobaki: Coy Mzungu, Ndaro, Steve Mweusi, Madirisha (huyu hajui kuchekesha wala kuingiza, anabebwa kishkaji), Mtumishi Obama, Shafii Brand (sharobaro), Mr. Black, MC Kisoli (aweke nguvu kwenye utangazaji na ushereheshaji tu), Chard Talent (muigizaji mzuri ila siyo uchekeshaji), Deo (kelele nyingi tu, kwenye uigizaji anaweza aweke nguvu huko) hawa wangetafuta shughuli nyingine za kufanya, angalau mwenzao Coy Mzungu kajipata. List ni ndefu sana, wapo wanaojitahidi ila wengine ni wasindikizaji tu.

Cha msingi watu wapambane tu wapige madusko yao, muhimu mkate/ugali ukae mezani. Kwa hapa bongo watapiga pesa tu maana tasnia yetu ya sanaa hadhira imeshazoea kupokea kazi mbovu, kuanzia muziki, filamu, uchekeshaji n.k.
Stand comedy is the hardest Job ever
 
Yote tisa kumi, ndo tuone jamii kubwa ya WaTZ either ni stress au masuala ya afya ya akili, wakikaa kwenye hizi live shows za stand up comedy wanachekeshwa na hawa hawa tunaoona hawachekeshi. Tena wanalipia hela kabisa mara kwa mara. Maybe ni audience wana stress sana au sijui ni nini kwakweli...anyways its all about choices...let me not judge..(thou I think I have)
Kuna kujichekelesha kwa mkumbo pia, Waswahili ukiwa na wenzako unaweza kuwa unacheka cheka hovyo tu vitu ambavyo hata havichekeshi.
 
Comedians Hawa hawajui kuchekesha (kwa mujibu wangu), nimewafollow ili niwacheke wasivojua kuchekesha

@shafii_comedian
Mr mwanya
Mr navy og
Chenjeu
neila (Cheka tu)poor presentation
mzee shayo
Mama chanja
asma_comedian
headmaster
ganslay

Hawa wote ni wavivu wa kulima

To be Continued
 
Comedians Hawa hawajui kuchekesha (kwa mujibu wangu), nimewafollow ili niwacheke wasivojua kuchekesha

@shafii_comedian
Mr mwanya
Mr navy og
Chenjeu
neila (Cheka tu)poor presentation
mzee shayo
Mama chanja
asma_comedian
headmaster
ganslay

Hawa wote ni wavivu wa kulima

To be Continued
Ganslay kama huwa namwelewa kiasi
 
Back
Top Bottom