Ni mstari gani kwenye biblia unautumia sana upitiapo nyakati ngumu katika Maisha

Isaya 41:10
[10]usiogope, kwa maana mimi ni pamoja nawe; usifadhaike, kwa maana mimi ni Mungu wako; nitakutia nguvu, naam, nitakusaidia, naam, nitakushika kwa mkono wa kuume wa haki yangu.
 
Imeshiba sana hii na imekaa vizuri,shukrani kwa neno zuri!
 
Toleo gani hili linabadili neno tofauti na lilivyo kwenye matoleo mengine?
Muhimu sana kama wewe ni Mkristo ujue kwamba lengo la Biblia kuwepo kwa toleo la lugha tofauti tofauti ni ili kila atakaeisoma aielewe kiurahisi kwa lugha anayoielewa na kutafakari kitu akiwa amekielewa Biblia siyo kitabu cha siri au cha uganga kwamba isomwe huku msomaji akifungua codes

Na tujue huwa hakipungui kitu neno na maana inabaki vile vile muhimu ni mimi ninaesoma naelewa?mfano huo mstari uliopandishwa hapo kuna eneo ukisomwa wasikilizaji wanabaki njia panda same to unaoujua wewe ukisomwa watu hawauelewi.
 
Bwana ni mchungaji wamaisha yangu sitapungukiwa na kitu
 
Mathayo 7:7 Ombeni, nanyi mtapewa; tafuteni, nanyi mtaona; bisheni, nanyi mtafunguliwa;

Mathayo 7:8 kwa maana kila aombaye hupokea; naye atafutaye huona; naye abishaye atafunguliwa.
Na ikawe hivyo.
Naona unatembea na neno lenye pumzi ya Bwana!
 
Moja ya thread bora ndani ya huu mwaka . Ila zaburi na mithali vitabaki kuwa vitabu bora sana kwenye maswala ya kutafakari .
Vinatia faraja sana mkuu.
Unafahamu maisha yetu nyakati fulani changamoto zinatuumiza.
 
Mithali 3:1 Mwanangu, usiisahau sheria yangu, Bali moyo wako uzishike amri zangu.

Mithali 3:2 Maana zitakuongezea wingi wa siku. Na miaka ya uzima, na amani.

Mithali 3:3 Rehema na kweli zisifarakane nawe; Zifunge shingoni mwako; Ziandike juu ya kibao cha moyo wako.

Mithali 3:4 Ndivyo utakavyopata kibali na akili nzuri, Mbele za Mungu na mbele ya mwanadamu

Mithali 3:5 Mtumaini BWANA kwa moyo wako wote, Wala usizitegemee akili zako mwenyewe..

Mithali 3:6 Katika njia zako zote mkiri yeye, Naye atayanyosha mapito yako.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…