Shimba ya Buyenze
JF-Expert Member
- Dec 22, 2014
- 182,097
- 1,099,383
Isaya 41:10-13
Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Isaya 41:10-13
Isaya 41:10Bwana wetu Yesu kristo asifiwe wana Jf
Katika maisha yetu hapa duniani kuna wakati tunapitia nyakati zilizo na mambo magumu sana, kiasi kwamba kwa uwezo wetu unakosa majibu na kubaki kujiuliza maswali magumu yasiyo na majibu.
Nyakati kama za Kufukuzwa kazi, Ugumu wa maisha, kupoteza wapendwa wetu tuliowapenda sana. Usaliti katika maisha ya mahusiano na ndoa, kukosa kazi, kupakaziwa maneno yasiyo na ukweli pengine ugonjwa wa muda mrefu.
Tunapitia dhiki, mateso na maumivu katika maisha. Ukipata hiki unakosa kile ndivyo maisha yalivyo.
Natumaini letu linabakia kwa Muumba wetu.
Je ni mstari gani kutoka kwenye biblia unautumia sana kukupa faraja mpendwa.
Kwa upande wangu, Mstari unaoniongoza kila siku ni
Hakika wema na fadhili zitanifuata Siku zote za maisha yangu; Nami nitakaa nyumbani mwa BWANA milele.
Zaburi 23:6
Karibu.
Tusichoke kutenda wema.
Imeshiba sana hii na imekaa vizuri,shukrani kwa neno zuri!Ayubu 2:10
[10]Lakini yeye akamwambia, Wewe wanena kama mmoja wa hao wanawake wapumbavu anenavyo. Je! Tupate mema mkononi mwa Mungu, nasi tusipate na mabaya? Katika mambo hayo yote Ayubu hakufanya dhambi kwa midomo yake.
Na Muhubiri 3
1 Kwa kila jambo kuna majira yake, Na wakati kwa kila kusudi chini ya mbingu.
2 Wakati wa kuzaliwa, na wakati wa kufa; Wakati wa kupanda, na wakati wa kung'oa yaliyopandwa;
3 Wakati wa kuua, na wakati wa kupoza; Wakati wa kubomoa, na wakati wa kujenga;
4 Wakati wa kulia, na wakati wa kucheka; Wakati wa kuomboleza, na wakati wa kucheza;
5 Wakati wa kutupa mawe, na wakati wa kukusanya mawe; Wakati wa kukumbatia, na wakati wa kutokumbatia;
6 Wakati wa kutafuta, na wakati wa kupoteza; Wakati wa kuweka, na wakati wa kutupa;
7 Wakati wa kurarua, na wakati wa kushona; Wakati wa kunyamaza, na wakati wa kunena;
8 Wakati wa kupenda, na wakati wa kuchukia; Wakati wa vita, na wakati wa amani.
Muhimu sana kama wewe ni Mkristo ujue kwamba lengo la Biblia kuwepo kwa toleo la lugha tofauti tofauti ni ili kila atakaeisoma aielewe kiurahisi kwa lugha anayoielewa na kutafakari kitu akiwa amekielewa Biblia siyo kitabu cha siri au cha uganga kwamba isomwe huku msomaji akifungua codesToleo gani hili linabadili neno tofauti na lilivyo kwenye matoleo mengine?
Wahun huu mstar wanautumia vibaya ili kuhalalisha mambo yao"Nayaweza mambo yote katika yeye anitiaye nguvu"
sijajua ni kitabu gani ila naupenda sana
Bwana ni mchungaji wamaisha yangu sitapungukiwa na kituBwana wetu Yesu kristo asifiwe wana Jf
Katika maisha yetu hapa duniani kuna wakati tunapitia nyakati zilizo na mambo magumu sana, kiasi kwamba kwa uwezo wetu unakosa majibu na kubaki kujiuliza maswali magumu yasiyo na majibu.
Nyakati kama za Kufukuzwa kazi, Ugumu wa maisha, kupoteza wapendwa wetu tuliowapenda sana. Usaliti katika maisha ya mahusiano na ndoa, kukosa kazi, kupakaziwa maneno yasiyo na ukweli pengine ugonjwa wa muda mrefu.
Tunapitia dhiki, mateso na maumivu katika maisha. Ukipata hiki unakosa kile ndivyo maisha yalivyo.
Natumaini letu linabakia kwa Muumba wetu.
Je ni mstari gani kutoka kwenye biblia unautumia sana kukupa faraja mpendwa.
Kwa upande wangu, Mstari unaoniongoza kila siku ni
Hakika wema na fadhili zitanifuata Siku zote za maisha yangu; Nami nitakaa nyumbani mwa BWANA milele.
Zaburi 23:6
Karibu.
Tusichoke kutenda wema.
Fafanua mkuuWahun huu mstar wanautumia vibaya ili kuhalalisha mambo yao
Na ikawe hivyo.Mathayo 7:7 Ombeni, nanyi mtapewa; tafuteni, nanyi mtaona; bisheni, nanyi mtafunguliwa;
Mathayo 7:8 kwa maana kila aombaye hupokea; naye atafutaye huona; naye abishaye atafunguliwa.
Vinatia faraja sana mkuu.Moja ya thread bora ndani ya huu mwaka . Ila zaburi na mithali vitabaki kuwa vitabu bora sana kwenye maswala ya kutafakari .
Hakika . Tunapitia mengi sana ya kuumiza ila ni matumaini tu yanayotufanya tusonge mbele.Vinatia faraja sana mkuu.
Unafahamu maisha yetu nyakati fulani changamoto zinatuumiza.
Km nikifafanua nitaonekana ni muhunFafanua mkuu