Tony Cipriano
JF-Expert Member
- Nov 17, 2022
- 2,139
- 5,109
njururuHivi hapo inaongelewa fedha makini au pesa?
Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
njururuHivi hapo inaongelewa fedha makini au pesa?
ahsantee mkuu ngoja niwekee kambiiKaribu sana
Sasa pesa si ni Man made?njururu
Filp 4:13"Nayaweza mambo yote katika yeye anitiaye nguvu"
sijajua ni kitabu gani ila naupenda sana
Kila jambo na wakati wake.Ayubu 2:10
[10]Lakini yeye akamwambia, Wewe wanena kama mmoja wa hao wanawake wapumbavu anenavyo. Je! Tupate mema mkononi mwa Mungu, nasi tusipate na mabaya? Katika mambo hayo yote Ayubu hakufanya dhambi kwa midomo yake.
Na Muhubiri 3
1 Kwa kila jambo kuna majira yake, Na wakati kwa kila kusudi chini ya mbingu.
2 Wakati wa kuzaliwa, na wakati wa kufa; Wakati wa kupanda, na wakati wa kung'oa yaliyopandwa;
3 Wakati wa kuua, na wakati wa kupoza; Wakati wa kubomoa, na wakati wa kujenga;
4 Wakati wa kulia, na wakati wa kucheka; Wakati wa kuomboleza, na wakati wa kucheza;
5 Wakati wa kutupa mawe, na wakati wa kukusanya mawe; Wakati wa kukumbatia, na wakati wa kutokumbatia;
6 Wakati wa kutafuta, na wakati wa kupoteza; Wakati wa kuweka, na wakati wa kutupa;
7 Wakati wa kurarua, na wakati wa kushona; Wakati wa kunyamaza, na wakati wa kunena;
8 Wakati wa kupenda, na wakati wa kuchukia; Wakati wa vita, na wakati wa amani.
Nimeoona1 Kor 10:13
Jaribu halikuwapata ninyi, isipokuwa lililo kawaida ya wanadamu; ila Mungu ni mwaminifu; ambaye hatawaacha mjaribiwe kupita mwezavyo; lakini pamoja na lile jaribu atafanya na mlango wa kutokea, ili mweze kustahimili
Nayakumbuka maneno yenye ujumbe mzito kutoka mt. Paul akiwa gerezani.Wfilipi 1;21
Kwa maana kwangu Mimi kuishi ni Kristo kufa ni faida.......