Ni mstari gani kwenye biblia unautumia sana upitiapo nyakati ngumu katika Maisha

Ni mstari gani kwenye biblia unautumia sana upitiapo nyakati ngumu katika Maisha

Bwana wetu Yesu kristo asifiwe wana Jf

Katika maisha yetu hapa duniani kuna wakati tunapitia nyakati zilizo na mambo magumu sana, kiasi kwamba kwa uwezo wetu unakosa majibu na kubaki kujiuliza maswali magumu yasiyo na majibu.

Nyakati kama za Kufukuzwa kazi, Ugumu wa maisha, kupoteza wapendwa wetu tuliowapenda sana. Usaliti katika maisha ya mahusiano na ndoa, kukosa kazi, kupakaziwa maneno yasiyo na ukweli pengine ugonjwa wa muda mrefu.

Tunapitia dhiki, mateso na maumivu katika maisha. Ukipata hiki unakosa kile ndivyo maisha yalivyo.

Natumaini letu linabakia kwa Muumba wetu.

Je ni mstari gani kutoka kwenye biblia unautumia sana kukupa faraja mpendwa.

Kwa upande wangu, Mstari unaoniongoza kila siku ni

Hakika wema na fadhili zitanifuata Siku zote za maisha yangu; Nami nitakaa nyumbani mwa BWANA milele.
Zaburi 23:6

Karibu.
Tusichoke kutenda wema.
Zaburi 23.
 
2 Wafalme 4:34-35

34. Ndipo akajilaza juu ya mtoto, mdomo wake juu ya mdomo wa mtoto, na macho yake juu ya macho ya mtoto na mikono yake juu ya mikono ya mtoto. Na alipokuwa amekaa hivyo, mwili wa mtoto ukaanza kupata joto.

35. Elisha akasimama na kutembeatembea chumbani, kisha akarudi na kujilaza tena juu ya mtoto. Mtoto akapiga chafya mara saba, halafu akafungua macho.
 
Screenshot_20231006_064847_Swahili Bible Offline.jpg
 
Back
Top Bottom