Habari Wakuu,
Safari City ni mradi wa Satellite City uliobuniwa na NHC mwaka 2016 ni miaka 10 imepita bila mradi kuendelezwa ukienda sasa ivi unakutana na mapori,barabara zimefunikwa na nyasi, ni muda sasa wa kufufua mradi huu muhimu kwani uko pembezoni panapojengwa uwanja wa Afcon nashauri serikali na wahusika waufufue huu mradi, kulikua na malalamiko watu waliolipia viwanja walikua wanazungushwa kuoneshwa viwanja vyao na kupatiwa hati ili waweze kuviendeleza.