Nipende kutoa wito kwa vijana tunaochipukia kwenye siasa lakini pia nitoe angalizo kwa wanajamii kuhusu kutofautisha kati ya Serikali(ambayo unaweza kuinyanyasa utakavyo) na Dola(ambalo ni dubwana kubwa sana lisilojali )
Unapaswa kutambua na kutofautisha vitu hivi viwili kwa umakini mkubwa ...
Dola linaweza kukushughulikia kwa namna zote ziwezekanazo ziwe halali au haramu au za uchawi au dini lakini ni lazima likunyooshe na hakuna namna unaweza kuliadhibu...DOLA halitishwi na chombo au mtu yoyote ndani au nje ya nchi...
Yaani DOLA ina maamuzi yote kwa kutumia mbinu zote na wala halijali ...lenyewe linakunyoosha tu ...halafu haliathiriki kwa chochote au lolote ....DOLA halina mshikamano na Serikali ...halibanwi na sheria yoyote...ni DUBWANA korofi mno...halina formalities au regularities ...DOLA NI DOLA HALIJALI KELELE WALA ATHARI ...
EWE KIUMBE LIHESHIMU DOLA SIKU ZOTE....DOLA NI ALFA NA OMEGA.!!
DOLA HUTUMIA MAGUVU ILI LIENDELEE KUITWA DOLA.SIO BAHATI MBAYA BALI NDIO LIMEUMBIWA HAYO
KWA HISANI YA MTU WA TANZANIA!!