Ertugrul Bey
JF-Expert Member
- Aug 6, 2020
- 14,705
- 30,041
Kalamu,Unasikitisha sana na akili za namna hii, mtu ambaye mwanzo ulionekana kuwa 'balanced' kabisa.
Lakini yote haya unalazimika kuzima akili namna hii kwa sababu zipi hasa; kumtetea mwovu Samia kwa kuwa unahusiana naye kivipi?
Unazungumzia "Mondlane", anahusiana vipi na ushetani huu unaofanyika hapa?
Tulijuwa toka mwanzo kabisa; kwamba 'model' aliyopanga kuifuata Samia ni ya huyo Museveni; lakini Samia hakujuwa kuwa Museveni na yeye ni vitu mbalimbali kabisa.
Sasa tazama matatizo makubwa aliyojitengenezea mwenyewe hapa na nyinyi washangiliaji wake mkiendelea huku mkijuwa wazi kuwa mtu wenu kishaharibu vibaya sana.
Binafsi nakuona kama hatred kwa Samia imekuwa kubwa sana kiasi kwamba hakuna lolote ambalo mtu atasema ila moja kwa moja utamnasabisha na Samia,unakosea badilika brother
Mimi utaendelea kuniona katika picha mbali mbali humu kwakuwa sipo upande wowote ule,huwa napambania kile ninachoamini ni sahihi,wala hutaniona nikimsifia mama Samia,kwani sikubaliani nae kwa baadhi ya mambo fulani fulani
Kwahiyo kwakuwa eti sikuunga mkono maandamano basi usinichukulie nipo upande wa ccm au serikali, napinga maandamano kwakuwa yanahatarisha amani ya nchi,siku ambayo watu wataanza tena kuzungumzia maandamano basi nitakuja na kupinga hiyo ishu kama nilivyosimamia msimamo wangu hapo awali
Nimesema jambo moja hapo kwamba kuwa kiongozi wa upinzani ni lazima uwe tayar kulipa gharama ya kile unachokipigania kwa sura yoyote ile kama mifano ya wapinzani nilio wataja hapo awali,si lazima matukio yawe sawa au kuwiana lakini kikubwa upinzani,manyanyaso,kuonewa kupo tu ukiwa upinzani
Relax bro hatred yako kwa mama Samia isikutie upofu ukashindwa kuon uhalisia wa mambo