Kumpika mtu and kumuamulia his/her destiny ni tofauti.
Ndio maana ktk ishu ya mpira kuna ACADEMY mbn hao hutolei mfano?
Same applied here, Programming si ya kuisoma ukiwa ushakomaa akili kupitiliza utapasuka kichwa, ile inatakiwa iwe ni culture yake anayopractice kila siku. Akiamua aachane nayo ni yeye sasa.
Epuka lawama kutoka kwa Watoto wako, just fanya kila kitu ambacho unaona ni sahihi.
Ni kheri apoteze muda akisoma mambo ya maana kuliko apoteze muda kuangalia katuni.
Sawa ila ni muhimu kujua uwezo, interest na maono ya mtoto. Unaweza kumlazimisha awe IT kumbe bongo yake haiendani.
Nimetolea mfano zidane kwa sababu una maono kama yake na ni mfano wa watu waliofeli kukuza kipaji cha mtoto.
Mess, Ronaldo nao wamefuata maono yao ila time will tell kama wapo right.
Academy ni mpango madhubuti wa kuinua vipaji.Academy zimejikita kwenye kukuza kipaji sio interest.
USA wana Mensah club ambayo kazi yake ni kuthibitisha na kugundua watoto wenye IQ kubwa ili wapewe mtaala wao.
Nimuhimu sana kuzingatia uwezo wa mtoto vinginevyo utapoteza muda na rasilimali.
Kumbuka muda ni mali.
Nakutahadharisha tu usije poteza nguvu na rasilimali, kama unataka kwenda kitaalamu basi waone wana saokilojia au walimu wabobevu ktk makuzi ya mtoto.
Wewe kusoma jambo fulani haikufanyi kuwa career guider vinginevyo uwe psychologist.
Watu wengi sana wamepotezwa na matamanio ya nyakati bila kujali mahitaji na mazingira ya nyakati.
Jaribu kuepuka kitu kinaitwa" Emotional Intelligence" , huu ndio ugonjwa mkubwa unaotukumba waafrika na matokeo yake hatueleweki.
Jikite zaidi ktk Rational intelligence ambayo itakusaidia kufanya rational decision ambayo itazaa matunda chanya na ustawi wa familia yako.