Kuna mtu kamwelewa huyu chalii
 
Leo tu Pemba kada amekatwa mapanga. Tunaambiwa tayari watu zaidi ya 40 wametiwa nguvuni !!. Mbunge anamiminiwa risasi 38 na 16 zinampata hakuna hata dalili ya ufuatiliaji wowote ?!.

Kweli mleta mada tukikuita mpuuzi usichukie , unastahili
 
Kwanini serikali haijatoa tamko lolote kuhusu tukio la Lissu? Hata Magu mwenyewe hajasema hata pole Lissu! Mbona hakuna uchunguzi wowote unaoendelea kwa tukio kubwa kama lile? Acha kutetea wauaji na wewe ni muuaji pia.
 
Zaidi ya yote yaliyotajwa hapo juu Mleta Uzi atoe majibu ya maswali haya:-
1. Kwa nini Polisi walizuia watu kuvaa T-Shirt zilizoandikwa "Pray for Tundu Lissu"?
2. Kwa nini Polisi walizuia watu kukusanyika na kumwobea Tundu Lissu?
3. Geti la kuingia kwenye Makazi alipokuwa anakaa Tundu Lissu na viongozi wengine wa serikali huwa linalindwa
na maaskari 24/7. Siku na wakati wa tukio hawakuwapo. Nani alitoa amri ya kuwaondoa maaskari hao?
4. Kwa nini Taarifa ya Uchunguzi wa tukio la jaribio la kumwua Tundu Lissu iliyofanywa na Bunge ilizuiwa isisomwe?

NB: Kama serikali haikuhusika basi ilikuwa imekwenda likizo na hadi sasa haijarudi

Hakuna mwiba ambao ccm imewahi kukutana nao tangu nchi ipate uhuru isipokuwa LISSU.

Mwanamageuzi halisi asiyeyumbishwa na vipande vya mkate na sarafu.

Ni shujaa na jasiri asiogopeshwa kwa mtutu wa bunduki.
 
inaonekana Uzi bado unaendelea Ila umeamua kuufupisha tu kimakusudi.

Ila nipo upande wako huyu jamaa alipigwa shaba na waliokuwa wanamtumia.

MAGUFULI mitano tenaaa.

Sent from my Infinix X5515 using JamiiForums mobile app
 
Uo ndo ukweli halisi kwa akili zangu za ujasusi niliona ilo tangu mwanzo, hata taifa linalotaka kumsababishia vurugu taifa lingine simple tu wanamuua mtu anaekosoa ilo taifa,

Ukitaka kumdhuru mdeni wako msubir agombane na mwingine ndo umdhuru, lisy wanaishi nae wanamlipa mshahara,wanashindwaj kumuua kimya kimya? Ni maboguz pekee wanaodhani lisy kashambuliwa na gover,
 
1. Ni nani aliyemnyima TL hela ya matibabu wakati akiwa mahututi?
2. Nani alimvua ubunge wakati akiwa bado akiendelea na matibabu
3. Nani aliwatoa wale maaskari wa zamu siku ya shambulio?
4. Nani alitoa amri ya line clear barabarani baada ya wahalifu kumaliza kumtwanga risasi Lissu?

5. Ni nani alitoa CCTV cameras baada tu ya shambulio kupoteza ushahidi?

Tuanzie hapo kwanza!!
 
Ndiyo ujue kwamba kwenye hiyo gover yako Kuna utitiri was vilaza
 
Kifyatu, naamini muda utakuwa umekupa majibu yako yote uliyouliza. Sasa sema ni nani aliyempiga Lissu risasi?
 
Nyingi ya hoja zako zinajibiwa na location (eneo tukio lilipotokea)
Kwa mfano raia wenye chuki au Watu wake wa karibu (Maadui ndani ya chama chake) kwa location ile labda kama wangekuwa ni Super man au Spider Man.
 
LIKE liked you

kuondolewa kamera!?
kuondolewa walinzi getiini!?
kunyimwa matibabu!?
Ongeza na kufukuzwa Ubunge...ni sawa na upo kitandani Hospitali alafu aliyepo pale Wodini anachomoa chupa ya damu, ukishtuka ukamuangalia anakukenulia meno.
 
Kama dhana ya pili ingekuwa kweli, nafikiri kungekuwa hata na tamko la kupinga unyama uliotokea na polisi wangefanya uchunguzi na kutoa hata taarifa.
JPM alilaani tukio lile na kusema uchunguzi utafanyika.

Ujinga punguzeni
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…