Ni nani aliyeharibu Mchakato wa Katiba Mpya? Tuanzie hapo

Kumbe haukuangalia bunge la katiba..?ilipigiwa kura na wajumbe na ilifail kupita ndo kukawepo rasimu ya katiba ya chenge,,
Ulikua bado hujazaliwa labda...
Wale wajumbe waliopiga kura walizingua tu. Hawakutakiwa kufanya yale yaliyofanyika. Ndio maana ilifia pale. Ili iwe katiba, ilitakiwa ije kwenye referendum. Wananchi ndio wangeamua. Walioandaa katiba wakawa wajuaji. Wakakutana na wajuaji wengine halafu kura za wananchi hazikupigwa
 


 
Rejea vitimbi vya kupitisha katiba kenya,,sio suala tu la kudumbukiza rasimu ya warioba,,kuna process,,na kura inahusika,,
Rasimu iliyopendekezwa ilipitishwa kwa kura,,ikabaki stage ya wananchi wote kuipigia kura,,
Sasa usidhani hiyo rasimu ilitupwa jalalani,,ipo
 
Katiba mpya itasababisha Muungano ufe. Maana tuliona maoni ya watu wa kule upande wa pili 95% hawautaki Muungano. Hali hii ndio imesababisha mchakato wa Katiba mpya kusitishwa.

Jambo lingine ni Chama tawala kinanufaika na uwepo wa Katiba hii ya zamani.
 
Katiba mpya ianishe,mgawanyo wa madaraka,iwe kwa zamu,bara na visiwani,,vyeo vigawanwaje,,sio mtu anapata madaraka anaanza kubuni mbinu za kutawala milele.
Eti visingizio,utamaduni wa kutawala kwa zamu si lazima,,
Lazima ianishwe na iwe lazima,Rais yeyote asiweze kutengua hicho kifungu
 
Ndio ile ya Warioba? Kizuri ni kuwa haijawahi kupigiwa kura ya wananchi kusema yes au no. Huko kwingine ni mbwembwe za uundaji wake na vita ya makundi maslahi
 
Si kila mtanzania anataka katiba mpya, kwani kuna wanaofaidika na kunufaika na katiba iliyopo sasa hasa waliyopo madarakani, hiyo ni kitu kigumu sana kupata katiba mpya yenye kukidhi matakwa ya wengi hususan wapinzani, hivyo basi busara, hekima na ushawishi ufanyike ili kiongozi wa nchi aridhie suala hili na likamilishwe kwa manufaa ya wananchi na nchi kwa ujumla wake. Haiwezekani kushindana kuvuta kisu wakati mwenziyo ameshika mpini na wewe umesha kunako makali. Na tuliona watu huko nyuma walikuwa wakisema na kuipigania katiba mpya lakini baada ya kupewa fupa msimamo wao ulitoweka. Hivyo basi inabidi wale ambao tunahitaji katiba mpya inabidi tufanye maombi kama vile tulivyofanya kuliombea taifa amani au kuiondoa Corona. Katiba mpya haikwepeki lakini ni lini na vipi itakuwa mambo hayo yanataka ustahamilivu.
 
Wachawi wa katiba mpya ni CCM, wanajua siku katiba mpya ikianza kutumika wao hawana chao...ndiyo maana wakamtisha tisha mwenyekiti wao Rais JK mbaya zaidi na yeye akakubali kutishika mchakato ukaishia kapuni...watu wakaambulia perdiem pale Dodoma...hela mabillion ya watanzania yakapotea.

Sasa CCM wameanza tena kama kawaida yao kumtisha mama kwamba katiba mpya italeta mgawanyiko kati ya Zanzibar na Bara... kwa hiyo waambie si ajenda kwa sasa, muda wako ukiisha kabidhi kujiti kwa mwingine- unakabibidhiwa nchi moja yenye serikali mbili ..ukimaliza kabidhi hivyo hivyo.

Kwa hiyo wananchi wenzangu kama mnasubiri katiba mpya ati mpewe kwa hisani na hawa hawa CCM hii sahauni..mtasubiri sana.

Duniani kote katiba hudaiwa!! wapo watakaoumia, wapo watakaopotea na wapo watakaokufa lakini kizuri zaidi wengi wataifaidi Tanzania yenye demokrasia pana isiyotegemea kauli ya mtu mmoja yeye tu aongee wengine mil 60 wamsikilize yeye tu No.
 
Kwani mchakato huo aliusimamia na kuuendesha nani mkuu, au kichwa chako hakina uwezo wa kuwaza hilo?

Mimi nakuuliza tu swali, kama unaweza kujibu hilo swali vizuri, basi hukuwa na sababu yoyote ya kuleta mada kama hii hapa.

Lakini najua, kutokana na ulivyowasilisha mada yako, uwezo wa kujibu hilo swali huna.

Na sipendi kuendelea kujibishana na wewe juu ya hili.
 
Ccm hawataki kabisa kusikia katiba mpya kwa sababu hii katiba ya sasa ni yao kwa asilimia mia moja na ndio inaendelea kuwaweka madarakani.

Ili katiba mpya ipatikane lazima liwepo shinikizo kali lisilo la kawaida hasa kutoka kwa mataifa ya wafadhili ambalo serikali itaona kabisa kwamba isipokubali uchumi utaangamia hapo ndipo wataufyata, vinginevyo hamna kitu.
 
We ulijuaje nchi haitaji katiba? Unanuuliza % ngapi hivi kitu kikiwa kibovu kikamilishwa kwa 199% kitakuwa na mantiki kwel we msukule?

Hili swali la kijinga kabisa, kaulize bunge liliwezaje kutenga, kutoa na kuidhinisha mabilioni ya fedha ili kugharamia katiba mpya

Ukipata majibu utajuwa watanzania ndio wanahitaki katiba
 

Ule upumbavu wa samweli sita na ccm wake, Badala ya maoni ya watanzania?
 
Rwanda ya Kagame inaendeshwa kibabe na wanayo katiba mbovu tu lakini kiuchumi wamesimama. Sisi tunaweza kupaa kiuchumi kwa katiba hii hii.

Hakuna uwekezaji unaokatazwa kwa kigezo cha katiba. Hakuna mwenye akili za kimaendeleo ambaye kanyimwa kufanya shughuli zake kwa kigezo cha katiba.
 

..Katiba pendekezwa iliyoandikwa na CCM iko wapi?

..Kwanini hawaileti kwa wananchi kwa hatua zinazofuata?

..Au, CCM hawaitaki tena katiba waliyoiandika wao wenyewe?

..Kitendo cha CCM kuifungia kabatini katiba iliyopendekezwa ndio kinawapa wapinzani uhalali wa kudai katiba mpya kama ilivyopendekezwa na TUME YA WARIOBA.
 
Katiba iliharibiwa na lile bunge maalum la wahuni (bunge la katiba), wakiongozwa na Mhe. Samweli Sitta. Ukada wa vyama kwenye lile bunge ndio ulioharibu mchakato mzima wa katiba, hadi wakaja na katiba pendekezwa ambayo ilikuwa pro-Chama tawala.
Sitta alikuwa na uwezo wa kuharibu mchakato? Alikuwa mkubwa sana kicheo?
 
Kiufupi ccm chini ya mwenyekiti wake kipindi kile Kikwete, alianzisha mchakato ana alipita mlango wa nyuma KWA kushirikiana na wanaccm wenzake kuharibu , KWA kulazimisha ingiza hoja ambazo zilionekana wazi kuondoa maana halisi ya mchakato mzima, usitafute mchawi ,
 
ulijuaje kama nchi inahitaji katiba mpya?..
Je katiba iliyopo inatekelezwa kwa asilimia ngapi?

Maisha ya watu na mahitaji ya watu hayajasimama (static) na ni kengefu (dynamic). Leo hii hakuna kampuni inayoishi ambayo inatumia njia zote ilizotumia 1977!! Hakuna!! Swala la kuhitaji Katiba huwa ni hisia kwanza ili wakati wa mchakato upimaji uoneshe kama kunahitajika kuendelea na jambo hilo au la! Kwa sasa mambo mengi yamebadilika, tafasiri ya uhuru mwaka 1960 ni tofauti na 1977 na 2020 pia. Kama uhuru wa 2020 sio ule ulioainishwa 1977 basi kuna haja ya kupanua uwigo au kuwa na tafsiri mpya!!

Other than God, the only other permanent thing is change!! Change hata usipoikiri na kuikubali, itaendelea kuwepo!! Kuikubali ni jambo jema kuliko kuipinga na ikahitajika kukulazimisha kuikubali!

Umeuliza maswali ya kidwanzi utadhani kuna uwezekano wa jamaa kujua kuna mambo mangapi katika Katiba na yanavunjwa kwa udogo au ukubwa gani. Sasa akikupata hizo asilimia unazotaka kupata, kwako zina hoja gani?? Au unataka kusema una kiwango cha uvunjaji ambacho kinakubaliwa?

Paper samurai!!
 
Tatizo Hakuna muungano, ni uvamizi uliopewa Jina la muungano
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…