Elections 2010 Ni nani aliyeingiza udini kwenye kampeni hizi?

Status
Not open for further replies.
Ni magazeti gani yalikuwa ya kwanza kuandika habari za kwamba Slaa katumwa na Kanisa? Nakumbuka magazeti ya Uhuru, Rai, Alnuur, Alhuda na Mtanzania ndiyo yaliyolikalia bango jambo hilo. Haya magazeti ni ya nani? Na je ni magazeti gani yaliyoandika waziwazi kwamba Waislamu wawachague Waislam wenzao. Kwa kumbukumbu zangu ni Al huda na Al nuur. Je ni hatua gani zilizochukuliwa hadi hivi leo dhidi ya magazeti haya? Sikuwa kusikia popote pale, CHADEMA wakiongelea suala la udini. Sasa iweje leo anayakemea aliyoyaanzisha yeye mwenyewe.

Tunataka Kikwete achukue hatua kubwa zaidi ya kukemea kwenye hotuba, tunataka awakamate wahariri wa magazeti ya Al nuur na Al huda, pia Mtanzania na Uhuru. kwa kuchochea udini nchini. Hii itasaidia sana kupunguza idadi ya wahariri wahuni kama hawa wa CCM ambao wanataka kuwagawa watanzania kwa misingi ya udini.

Na kama yeye na CCM aalitoa baraka kwa hayo magazeti, kwanza siyo magazeti tu na zile habari kwenye simu za wananchi nani atawakamata. Si atajikamata yeye mwenyewe? Anajua sana alichofanya kwenye kampeni, hapa anadhani watu wamekuwa wa-jinga.
 
Asante Mwanakijiji. Hii imekaa sawa sana hata sisi tulio nje ya nchi angalau tumeelewa nini
ilikuwa maana ya kususia hotuba ya JK.
SHUKRANI NA TUPO PAMOJA.
 
Mwanzoni anasema CHADEMA wametoka wakati Mh. Rais wa Jamuhuri Ya Muungano akiingia. Hii tayari ni kutambua kuwa kuna Rais. Pia anasema wanapeleka maelezo yao serikalini, inamaana wanaimani na serikali. Je, serikali inaongozwa na nani? Sio kwamba haya maelezo yanapelekwa kwa serikali ya Kikwete? Halafu, tatizo ni madai ya utekelezaji wa madai mbalimbali au tatizo ni uchaguzi? Mbona kama wanalalamikia sheria na madai yasiyo na uhusiano na uchaguzi? Pia anahitaji utekelezaji wa hayo katika uchaguzi wa 2015, inamaana uchaguzi huu amekubali kimsingi kwamba CHADEMA wameyakubali matokeo? Kwahiyo tatizo lipo katika maeneo hayo tu aliyotaja na si Urais? Maana hajazungumzia kabisa uwezekano wa yeye kunyang'anywa Urais.

Rais na serikali siyo halali usichoelewa ni nini? Hao wamechaguliwa na NEC siyo wapiga kura.
 
Kama anatka UDINI ataupata sana tu, kwanza kwa nini anakazania sana suala hili???? Mbona Pinda amezungukwa na Waislam kila upande lakini watu hawalalamiki? (Mkwere, Seif, Shein, Ghalib, Idd). Mkwere ni mtu wa kuogopwa sana atatupeleka pabaya...
 
Tukio la leo litasaidia huyu Mkwere asitembee ovyo kama zaidi ya ombaomba kwa sababu atakuwa na maswali mengi ya kujibu na kule kujiamini kwa kikwere kutakuwa kumekwisha. Na huu ni wakati wa kuona ufinyu wake wa kufikiri na kutenda.
 
Ngoja nikalale nipate ndoto na nitachangia mada hii kesho. Kila nikisoma nasikia usingizi unaofanana na kichefuchefu.
 
Tuache vijembe vya kidini na vya kikabila.. jamani.. tuengelea hoja iliyopo. Tafadhali.
 
Kama kuna ujinga niliouona safari hii ni watu kudandia hii hoja ya CCM kwamba "UDINI ndio umeanza kujitokeza kama tishio kubwa la umoja wa taifa letu". Pure hogwash! Watu wanashindwa kuona kuwa hii ni janja ya kutaka kuhamisha (derail) focus toka kwenye ufisadi na mfumo wa kimafia uliokumbatiwa na CCM ambao unazidi kukandamiza haki za wananchi, kutudhalilisha, kuangamiza rasilimali za taifa na kutudidimiza kwenye lindi la umaskini huku wateule wachache wakijinafasi kama vile wao ndio kila kitu.

Nashangaa sana hapa JF kuona baadhi ya watu wakitaka kugeuza kila thread kama mada ya kidini. Hakika mafisadi wanakenua tu kuona jinsi "mada mbadala" ikihamisha attention toka kwao. Let's be serious, hakuna mzozo wa kweli kati ya waislam na wakristo katika nchi hii; labda kwa wanasiasa wanafiki na wale wanaotafuta riziki zao kupitia shughuli za dini hizo; sio sisi wananchi wa kawaida. This is where I see JK and the like as strange beings.

The election is over. You have "won". No need to extend this awkward fallacy and rather dangerous assertion into our social fabric. Stop it!
 
Mwanzoni anasema CHADEMA wametoka wakati Mh. Rais wa Jamuhuri Ya Muungano akiingia. Hii tayari ni kutambua kuwa kuna Rais. Pia anasema wanapeleka maelezo yao serikalini, inamaana wanaimani na serikali. Je, serikali inaongozwa na nani? Sio kwamba haya maelezo yanapelekwa kwa serikali ya Kikwete? Halafu, tatizo ni madai ya utekelezaji wa madai mbalimbali au tatizo ni uchaguzi? Mbona kama wanalalamikia sheria na madai yasiyo na uhusiano na uchaguzi? Pia anahitaji utekelezaji wa hayo katika uchaguzi wa 2015, inamaana uchaguzi huu amekubali kimsingi kwamba CHADEMA wameyakubali matokeo? Kwahiyo tatizo lipo katika maeneo hayo tu aliyotaja na si Urais? Maana hajazungumzia kabisa uwezekano wa yeye kunyang'anywa Urais.
Mkuu, mwanzoni kidogo ningekuelewa lakini kwa hili umedelete kila kitu. Kwa serikali kuwa madarakani ndo ishara ya kuwa ni halali? Huu ukombozi wa nchi yetu labda aje dictator. kuna jamaa anatumia hii signature
miafrika ndivyo tulivyo
huu ndo ukweli!
 
ASANTE SANA mwanakijiji ila inasemekana siku zako zinahesabika , jiangalia brother
 
Rais na serikali siyo halali usichoelewa ni nini? Hao wamechaguliwa na NEC siyo wapiga kura.

Kwenye uchaguzi huu hata CHADEMA wamepata wabunge wengi kumbe nao wamechaguliwa na NEC?
 
Mwanzoni anasema CHADEMA wametoka wakati Mh. Rais wa Jamuhuri Ya Muungano akiingia. Hii tayari ni kutambua kuwa kuna Rais. Pia anasema wanapeleka maelezo yao serikalini, inamaana wanaimani na serikali. Je, serikali inaongozwa na nani? Sio kwamba haya maelezo yanapelekwa kwa serikali ya Kikwete? Halafu, tatizo ni madai ya utekelezaji wa madai mbalimbali au tatizo ni uchaguzi? Mbona kama wanalalamikia sheria na madai yasiyo na uhusiano na uchaguzi? Pia anahitaji utekelezaji wa hayo katika uchaguzi wa 2015, inamaana uchaguzi huu amekubali kimsingi kwamba CHADEMA wameyakubali matokeo? Kwahiyo tatizo lipo katika maeneo hayo tu aliyotaja na si Urais? Maana hajazungumzia kabisa uwezekano wa yeye kunyang'anywa Urais.

Ukizoea kumkaba kuku na kunyofoa kichwa siku ukinjiwa unakuja juu kwelikweli.
Kuchinja kuku ni kawaida.
Kutoka nje ya Bunge kupinga jambo ni kitu cha kawaida Duniani kote.
Sisi inaelekea niyo wa misho kufanya jambo hili.

Hawajapiga mtu hawjazomea wamemwachia ukumbi aongee na wafu wenzie.

Hii hiihii:first::first::first:
 
Mkuu, mwanzoni kidogo ningekuelewa lakini kwa hili umedelete kila kitu. Kwa serikali kuwa madarakani ndo ishara ya kuwa ni halali? Huu ukombozi wa nchi yetu labda aje dictator. kuna jamaa anatumia hii signature huu ndo ukweli!
Labda hatujaelewana, kama serikali iliopo madarakani si halali na uitambui kwanini shida yako uipelekee serikali hiyo? Dhana nzima ya kutoka ukumbi wa Bunge kama maelezo yake ndiyo haya yaliyotolewa basi dhana hiyo inaweza kuwa sahihi ila kama maelezo hayo yanahusu kutomtambua Rais basi aidha dhana au maelezo ya Dr Slaa kimojawapo kinapwaya.
 
Mwanakijiji naona umempa heshima sawa na ya Rais wa nchi kwa kuuweka wimbo wa Taifa kabla ya hotuba. Nimeipenda sana hii!! Inaonyesha kwamba huyu naye ni Rais kama alivyo Kikwete. Great job.
 
Ukizoea kumkaba kuku na kunyofoa kichwa siku ukinjiwa unakuja juu kwelikweli.
Kuchinja kuku ni kawaida.
Kutoka nje ya Bunge kupinga jambo ni kitu cha kawaida Duniani kote.
Sisi inaelekea niyo wa misho kufanya jambo hili.

Hawajapiga mtu hawjazomea wamemwachia ukumbi aongee na wafu wenzie.

Hii hiihii:first::first::first:
Sina tatizo na CHADEMA kutoka nje naomba nieleweke hivyo. Tatizo ni kwamba msingi wa madai yao haueleweki. Kifupi kama maelezo ni clip hii basi msingi mkubwa ni sheria kandamizi na kutofanyiwa kazi kwa madai yao mbalimbali. Lakini si utambuzi wa Kura za Urais. Na kama ni utambuzi wa kura za Urais hata mlolongo wa ufuatiliaji madai hayo unawalakini. Maana maelezo ya Dr Slaa yanaonyesha kuwa wangependa matatizo yaoyashughulikiwe kabla ya 2015.
 
Labda hatujaelewana, kama serikali iliopo madarakani si halali na uitambui kwanini shida yako uipelekee serikali hiyo? Dhana nzima ya kutoka ukumbi wa Bunge kama maelezo yake ndiyo haya yaliyotolewa basi dhana hiyo inaweza kuwa sahihi ila kama maelezo hayo yanahusu kutomtambua Rais basi aidha dhana au maelezo ya Dr Slaa kimojawapo kinapwaya.

Kwani wewe umeelewa vipi? au unataka ku-spin??
Ujumbe umeshafika right on the target!!
 
Haya ndio mambo ndugu zangu!!! Mwanakijiji, kalitupe hilo jembe mbali sana tu maana umeshakua zaidi ya Mwana-Kinyanambo C kule tunakolimaga vingamba!! Tangu leo wewe Mwanamji kwa kututumia hutuba wa Raisi wa Umma wa Jamhuri ya Mungano wa Tanzania, Daktari (PhD Darasani ktk Sheria, na Malezi Mema Vijana Tanzania) kwa tchnolojia hii ya hali ya juu. Sema Mwanamji tangu leo.
 
Last edited by a moderator:
Eeeeeh Mwaka huu kazi ipo!..shukran Dr.Slaa tumekuelewa sana, lakini natatizwa kitu kimoja tu - Ujumbe huu hasa unamlenga nani? Yaani nani hasa anayeweza kuleta mabadiliko hayo...?
 
Mwanzoni anasema CHADEMA wametoka wakati Mh. Rais wa Jamuhuri Ya Muungano akiingia. Hii tayari ni kutambua kuwa kuna Rais. Pia anasema wanapeleka maelezo yao serikalini, inamaana wanaimani na serikali. Je, serikali inaongozwa na nani? Sio kwamba haya maelezo yanapelekwa kwa serikali ya Kikwete? Halafu, tatizo ni madai ya utekelezaji wa madai mbalimbali au tatizo ni uchaguzi? Mbona kama wanalalamikia sheria na madai yasiyo na uhusiano na uchaguzi? Pia anahitaji utekelezaji wa hayo katika uchaguzi wa 2015, inamaana uchaguzi huu amekubali kimsingi kwamba CHADEMA wameyakubali matokeo? Kwahiyo tatizo lipo katika maeneo hayo tu aliyotaja na si Urais? Maana hajazungumzia kabisa uwezekano wa yeye kunyang'anywa Urais.
tatizo la chadema wana wivu wa kike!
 
Status
Not open for further replies.
Back
Top Bottom