Kalunguine
JF-Expert Member
- Jul 27, 2010
- 2,543
- 134
Ni magazeti gani yalikuwa ya kwanza kuandika habari za kwamba Slaa katumwa na Kanisa? Nakumbuka magazeti ya Uhuru, Rai, Alnuur, Alhuda na Mtanzania ndiyo yaliyolikalia bango jambo hilo. Haya magazeti ni ya nani? Na je ni magazeti gani yaliyoandika waziwazi kwamba Waislamu wawachague Waislam wenzao. Kwa kumbukumbu zangu ni Al huda na Al nuur. Je ni hatua gani zilizochukuliwa hadi hivi leo dhidi ya magazeti haya? Sikuwa kusikia popote pale, CHADEMA wakiongelea suala la udini. Sasa iweje leo anayakemea aliyoyaanzisha yeye mwenyewe.
Tunataka Kikwete achukue hatua kubwa zaidi ya kukemea kwenye hotuba, tunataka awakamate wahariri wa magazeti ya Al nuur na Al huda, pia Mtanzania na Uhuru. kwa kuchochea udini nchini. Hii itasaidia sana kupunguza idadi ya wahariri wahuni kama hawa wa CCM ambao wanataka kuwagawa watanzania kwa misingi ya udini.
Na kama yeye na CCM aalitoa baraka kwa hayo magazeti, kwanza siyo magazeti tu na zile habari kwenye simu za wananchi nani atawakamata. Si atajikamata yeye mwenyewe? Anajua sana alichofanya kwenye kampeni, hapa anadhani watu wamekuwa wa-jinga.