Elections 2010 Ni nani aliyeingiza udini kwenye kampeni hizi?

Elections 2010 Ni nani aliyeingiza udini kwenye kampeni hizi?

Status
Not open for further replies.
even though wengi mnamchukia... lakini kuna kweli ndani ya maneno yake try to read btw his lines ...

Kuna wakati mwizi anaweza kujilinda kwa kupiga kelele za mwizi mwizi mwizi kwa sauti zaidi. Ingawa yeye ndiye anafukuzwa na watu nyuma yake wanapiga kelele hizo, wengine wakimwona yeyeanapiga kelele za mwizi mwizi, wanaweza kudhani kuna mwizi mbele yake.

Anayosema Kikwete yana ukweli, lakini ni kweli anatenda hayo au alitenda hayo? Kwake urais una maana zaidi kuliko umoja na maendeleo ya watanzania.
 
ili kuonesha kuwa jambo la udini linamkera kutoka moyoni anatakiwa kuwafukuza wasaidizi wake wote waliotumia propaganda za udini katika kumpatia jk advantage ya kisiasa. Na kuanzia awafukuze wakurugenzi wa ikulu waliofadhili tangazo la udini kisha ashuke kwa vilaza wake kina tambwe hiza.
kwani hawakujua nuru na giza havikai pamoja?!wanavuna walichopanda mwaka 2000.mmelikoroga mtalinywa.au na hili nalo maigizo tu mjomba??
 
Hawa si ndio walidhamini tangazo la udini kupitia Ikulu kama ilivyolipotiwa na Raia Mwema?

Alafu huu udini wanaohubiri mbona hawatoi evidences watu wanaishia kusema udini udini bila kusubstantiate where
Sahihisho...
Gazeti ni RAI (lile la Rostam) siyo Raia Mwema
 
Swali moja sijapewa jibu bado,

Wabunge wa CHADEMA walivyoshiriki kupiga kura katika kulihakiki pendekezo la Kikwete kwa kiti cha Waziri Mkuu, walikuwa wanalipigia kura pendekezo la nani?

Usitake kutubabaisha na cheap question yako. Kama umechaguliwa mke na humtaki kuna mambo mawili unaweza fanya na hakuna mtu anaweza kukuingilia;
1. Kumkataa
2. Kuoa na kuacha

Ilichofanya CHADEMA ni kumkataa kwa kupiga kura za HAPANA ambazo kila mtu hata Pinda mwenyewe anajua alizipata toka kwa CHADEMA.

Hata mkisemaje ujumbe umefika kisawasawa.
 
Kwa muda mrefu sasa,Rais Jakaya Kikwete amekuwa akitahadharisha kuhusu kuwapo kwa mgawanyiko wa kidini huko nyumbani.Aliongea hayo wakati wa kampeni zake na amerejea tena katika hotuba yake ya uzinduzi wa Bunge.

Tuweke kando mjadala wa namna Kikwete na CCM walivyoshinda uchaguzi mkuu uliopita hivi majuzi.Tuijadili hoja yake ya udini.Hivi kama amepata ushindi halali,anaposema kuna mgawanyiko wa udini anamaanisha kura zote alipigiwa na Waislamu wenzake au?Maana kama kweli kuna mgawanyiko wa udini basi ni dhahiri kuwa matokeo ya uchaguzi huo yasingempa ushindi wa zaidi ya asilimia 60 ( tuki-neglect uchakachuaji).

Let's call a spade a spade.Hivi leo Kikwete anathubutu kulalamika kuhusu tatizo lisilokuwepo la udini ilhali yeye na wanamtandao wenzake walimwaga sumu kubwa ya udini mwaka 2005 to an extent "akawaingiza mkenge" Waislam wenzie kwa kuwaahidi Mahakama ya kadhi na kuahidi kushughulikia uanachama wa OIC?

Na hata tukiweka hilo kando,hivi ile kauli ya "CHAGUO LA MUNGU" haikutokana na jitihada za Kikwete na wanamtandao wenzie kuwaghilibu viongozi wa dini hadi wakamtangaza kuwa amechaguliwa na Mungu kuwakomboa Watanzania?Actually,huo haukuwa udini per se bali kufuru kwa Mwenyezi Mungu.Na kwa sie tunaofahamu kuwa Mungu si Athumani,na hapendi kuchezewa,ipo siku atawaadhibu wale wote waliotumia jina lake kwa minajili ya kusaka kura.

Mie nilikuwa Tanzania mwaka from Oktoba 2005 hadi April 2006 kwenye fieldwork yangu.Mungu huyohuyo tuliyeambiwa Kikwete ndio Chaguo lake mwaka 2005 anihukumu iwapo sentensi ifuatayo ni ya uzushi.Miongoni mwa maustaadhi niliowaintavyuu kwenye fieldwork yangu walibainisha waziwazi kuwa waliahidiwa na Kikwete na timu yake kuwa laiti angepata urais angeshughulikia vilio mbalimbali vya Waislam.Kwangu,huo sio udini as such kwa vile kuna matatizo ya msingi yanayowakabili Waislam na ambayo awamu mbalimbali za serikali tangu uhuru zimekwepa kuyashughulikia.Eneo moja la msingi ni elimu.Mwalimu Nyerere alikiri katika hotuba yake ya tarehe 9/12/1962 kwamba " wengi wa waliofanikiwa kupata elimu walifanya hivyo kupitia shule za misheni,na hivyo wengi ni Wakristo.Hapa tena,kwahiyo,tuna mgawanyiko ambao uwepo wake unaweza kuwa tishio kwa umoja wetu".Akaendelea kusema, " marafiki zangu,kila mmoja wetu afanye jitihada za kujenga Tanganyika ambayo hakutakuwa na tofauti na migawanyiko".Japo wakati Nyerere anastaafu mwaka 1985 alidai kuwa amefanikiwa kutimiza azma hiyo,ushahidi wa kitaaluma unapingana na kauli hiyo.

Kwahiyo,binafsi kama Mtanzania ninayependa kuona nchi yetu ikiwa na jamii yenye usawa,naamini kuwa viongozi wetu wana jukumu la kulishughulikia suala hili na kulipatia ufumbuzi.Kumekuwa na unafiki mkubwa katika kushughulikia malalamiko ya msingi ya Waislamu.Lakini kwa vile lengo la makala hii sio kuzungumzia suala hilo,nachoweza kuandika kwa kifupi ni kuwa kwa namna moja ua nyingine awamu zote nne za urais zimezembea kuyapatia ufumbuzi malalamiko ya Waislam huku Awamu ya Nne ikiingia madarakani kwa kujitambulisha waziwazi na kwa siri kuwa sio tu inayatambua matatizo na malalamiko ya Waislam lakini pia imedhamiria kuyatatua.Na katika kuonyesha iko serious,ahadi ya Mahakama ya Kadhi ikaingizwa kwenye manifesto ya uchaguzi ya CCM mwaka 2005.

Waislam wanajua,na sie tusio Waislam pia tunajua,kwamba ahadi hiyo ilikuwa ni danganya toto tu.Miaka mitano baadaye,suala la Mahakama ya Kadhi na kujiunga limeendelea kuwa ngonjera kama ilivyo kwa "maisha bora kwa kila Mtanzania".

Kwahiyo,Kikwete aliingia madarakani kwa kutumia udini lakini sio kwa vile yeye ni Muislam bali alitambua kilio cha Waislam kisha akakitumia kama turufu yake (kwa ahadi kuwa angeshughulikia matatizo yake) kisha baada ya kupata madaraka akajifanya hahusiki na suala hilo (refer kauli ya Kikwete kuwa aliyeanzisha hoja ya Kadhi ni Agustino Mrema-anaedansi nae hapo chini.What a cheap excuse!).Kwa lugha nyepesi,kilichojitokeza ni utapeli kwa kutumia matatizo ya kidini.

Kikwete analalamika kuhusu udini wakati kwa miaka mitano iliyopita Tanzania imekuwa na Rais na Makamu wa Rais Waislam.Na kwa vile Makamu wa sasa nae ni Muislam,inamaanisha kuwa kwa miaka 10 Tanzania itakuwa imekuwa chini ya Rais na Makamu wa Rais Waislam.Hakuna anayelalamika kwa vile wengi wetu tuna upeo mkubwa zaidi ya wa Kikwete anayetaka kulazimisha kuwa tuna mgawanyiko wa kidini.Ishu ya Rais na Makamu wake kutoka dini moja ni muhimu kwa vile Rais asipokuwepo nchini urais unakaimiwa na Makamu wake.Na likitokea lolote la kutokea,Makamu huyo atakuwa Rais kwa muda.

Sasa huyu Mkwere anapotuambia kuna mgawanyiko wa udini anaashiria kitu gani?Wakristo hawajalalamika muundo wa uongozi wa juu wa CCM ambapo idadi ya Waislam ni kubwa kuliko ya Wakristo (rejea wajumbe wa Kamati Kuu ya CCM).Kikwete hakuwahi kuekemea jitihada zilizokuwa zikifanywa na magazeti ya Kiislam kujenga picha kuwa Dkt Wilbroad Slaa ni mgombea alietumwa na Kanisa Katoliki.Kikwete hakukemea pale Daily News na Habari Leo,magazeti yanayoendeshwa kwa fedha za walipa kodi,yalifuata mkumbo wa magazeti hayo ya Kiislam kumtambulisha Dkt Slaa kama mgombea aliyetumwa na Kanisa.Hakukemea kwa vile nafsini mwake alikuwa na imani potofu kama hiyo ya wababaishaji hao kuwa Dkt Slaa ana ajenda ya Ukristo.

Tatizo ni kwamba Katiba yetu haitoi fursa ya kumkalia kooni Kikwete.Tatizo jingine ni kukosekana kwa ujasiri huko nyumbani wa kumkalia kooni Kikwete kisheria kwa tuhuma za kuhatarisha usalama wa taifa.Laiti Idara ya Usalama wa Taifa ingekuwa serious basi ni wazi wangemshauri Kikwete aache kuhatarisha usalama wa taifa kwa kauli zake zisizoambatana na uthibitisho kuwa kuna mgawanyiko wa kidini.Au inawezekana wanausalama wetu ndio wanamhadaa Kikwete kuwa kuna mgawanyiko wa udini?

Au inawezekana kuna tatizo kubwa zaidi kuhusu Kikwete,kwamba anaona vitu ambayo sie wengine hatuvioni?Je ni maono ya Sheikh Yahya?Au je kelele hizo za mgawanyiko wa kidini ni maandalizi ya kuihujumu Chadema,au pengine kumuibulia kesi Dkt Slaa kwa kigezo cha kucbochea vurugu za kidini?

Jamani,hata mwezi haujapita na tayari tunashuhudia mazingaombwe tusiyohitaji.Mara TAKUKURU wanamsafisha Chenge.Mara Kikwete anaendeleza ngonjera za mgawanyiko wa udini,mara Kikwete anamchagua Zakia Meghji kuwa mbunge licha ya mwanamama huyo kuhusishwa na suala la EPA ( na taarifa kuwa ana uhusiano wa kifamilia na Kikwete).

Tuspokuwa makini,2010-2015 itashuhudia miujiza ambayo haijawahi kutokea mahala popote duniani katika ulingo wa uongozi na siasa.Sad news is,sie kama wahanga tunaweza tusipate wasaa wa "kushangaa" na kujiuliza "what the hell is going on?"

KULIKONI UGHAIBUNI: Udini Anaozungumzia Kikwete ni Upi?
 
UDINI ANAOZUNGUMZIA KIKWETE NI ULE ALIOUANZISHA NA ANADHANI UMEKOLEA KUMBE HATA BADO HAUJAKOLEA.

Mara nyingi maraisi wakitaka kuonyesha kutokufungamana na upande wao, huwa wanafanya kinyume na matarajio ya watu katika mambo mbalimbali. Huwa wanaweka uangalifu katika uteuzi na hata timu zao za mambo mbalimbali.
Kwa mfano Nyerere alitaifisha shule za wakristo ili kutoa nafasi kwa watu wa dini zote, Pia badala ya kumpendekeza mkristo katika nafasi ya mrithi wake alimpendekeza Muislam na hilo likaondoa dhana ya udini.

Rais mwinyi alitoa uhuru na hata akaruhusu huduma nyingi za Kikristo zilizokuwa zimezuiliwa kuandikishwa akaziandikisha.

Rais Mkapa akawapa waislamu chuo cha uma cha TANESCO kuwa chuo kikuu cha waislamu.

Kikwete alipoingia akingia na ilani ya uchaguzi kuwabeba waislamu. Akashabikia OIC iliyokuwa imeachwa na wenzake wote.
Akaingia kwenye uteuzi wenye kuleta mashaka wa wakuu wa wilaya na mabalozi.
Timu yake ya kampeni bila kujali hakuweka mtu wa nje na dini yake.
Sasa hapa ni nani anaanzisha udini?
 
Kama JK anazungumzia udini kwanza ajiulize ni waislam wangapi waliosoma katika shule za mission na wanaoendelea kusoma katika shule hizo, ukweli utabaki kuwa ndugu zangu waislam hawana mwamko wa kupeleka watoto wao shule, hivyo ndiyo maana JK sasa hivyo anataka kila mwislam aliyepata degree kumpa cheo, kwake yeye siyo udini. na kama wakristo si elimu yao kuwa hakuna ambaye angekuwa kwenye serikali yake. ukianza kufanya utafiti kwenye nafasi za kuteuliwa 80% ni waislam hivyo wakristu kaeni chojo
 
hizo ni mbinu za kubomoa CHADEMA na CUF ,watanzania hawana habari na udini ila anayeibuaibua jambo hilo ni kama kukumbusha na kufanya wananchi popote walipo,iwe shuleni,maofisini na hata majumbani waanze kujiuliza hivi fulani ni dini gani.Na sisi wana CHADEMA na CUF ndiyo tunaolengwa maana walishapandikiza kwamba vyama hivi ni vya kidini, ila wamejionea wenyewe kwamba hatuna udini wala ukanda wowote hivyo CCM waache kabisa mbinu hii dhaifu maana imeshashindwa maana sisi wananchi tumesha n'gamua.
 
Mkuu MJJ
wanaendelea kumtishia mtu mzima nyau..
Ukweli ni kwamba miti yote sasa inateleza!!
 
Huyu mkwere jana alinishangaza kweli alipoingiza issue ya udini utawagawa WaTZ.
Inavoonekana huyu jamaa sasa hivi ana ile hali ya guilty consciousness kwa vile yeye ndiye alitembea nchi nzima akimwaga upupu wa Udini kwa kumhofia Dr. Slaa. Sasa anakimbia kivuli chake mwenyewe.

Cha ajabu analalamikia udini wakti bado anauendeleza. Mpaka sasa katika wabunge 3 aliowateua wote ni muslims:Zakhia Meghji,Nahodha na Mnyaa. Kiwete atuambie nani alihubiri sera ya udini na wapi? Alete ushahidi vingine anajikaanga mwenyewe!


Udini kuwepo upo na wanaouendekeza ni waikristu na historia ya dini ya kikristu ina dhihilisha hilo. Ndio maana waliopinga hii hoja kwa asilimia kubwa ni waikristu ambao wanaficha iliwasionekane wadini. Mungekuwa si wadini wala msingejadili hii hoja.

Rais mpaka sasa ameshateua watu 5. 2 wakristu tena uongozi wa juu na wa3 waislam ubunge tu.
 
Jamani hembu nifafanulieni, huo udini uko pande za wapi kwa sasa?? naishi tabata kisiwani, huku bado udini haujafika, mnihabarishe udini ulipo saiz ili ukikaribia huku tabata kisiwani niweke bango kubwa pale maeneo ya mwananchi ili wasifike huku maana ni juzi tu nimelipa kodi ya nyumba ya mwaka, mama mwenye nyumba ni muislam swala 5 na tunaelewana sana, udini ukifika huku ntafukuzwa na hela yangu sitarudishiwa, jirani kuna kanisa na msikiti halafu mbele kidogo kunapikwa kitimoto, udini ukifika huku hapatakalika, mama muuza mihogo hutuuzia mihogo sote waislam na wakristo bila kuuliza dini zetu, udini ukifika ntakosa mihogo ya chai asubuhi, ndo maana ninawaomba wanajamvi wenzangu mnijulishe udini ulipo kwa sasa ili nijiandae kukabiliana nao ukikaribia kufika huku tabata kisiwani. nawakilisha.
 
Jamani hembu nifafanulieni, huo udini uko pande za wapi kwa sasa?? naishi tabata kisiwani, huku bado udini haujafika, mnihabarishe udini ulipo saiz ili ukikaribia huku tabata kisiwani niweke bango kubwa pale maeneo ya mwananchi ili wasifike huku maana ni juzi tu nimelipa kodi ya nyumba ya mwaka, mama mwenye nyumba ni muislam swala 5 na tunaelewana sana, udini ukifika huku ntafukuzwa na hela yangu sitarudishiwa, jirani kuna kanisa na msikiti halafu mbele kidogo kunapikwa kitimoto, udini ukifika huku hapatakalika, mama muuza mihogo hutuuzia mihogo sote waislam na wakristo bila kuuliza dini zetu, udini ukifika ntakosa mihogo ya chai asubuhi, ndo maana ninawaomba wanajamvi wenzangu mnijulishe udini ulipo kwa sasa ili nijiandae kukabiliana nao ukikaribia kufika huku tabata kisiwani.

Nyumbani nako huko kijijini kutakuwa hakukaliki maana mama yangu alikuwa muislam kabadilishwa dini, na shangazi zangu nao baadhi yao wameolewa na waislam na wamebadili dini, udini ukifika huko wajomba zangu wataenda nyumbani kumchukua dada yao na baba atabaki mpweke, baba nae hatavumilia ataenda kuwachukua dada zake waliolewa na waislam,

hatari hiyo naiona, nilipopata kipaimara wajomba zangu na mama zangu wakubwa walileta mbuzi kwa ajili ya sherehe, tena mjomba ndo kamchinja maana yeye ni ustaadhi, udiini ukifika huko hatutakuwa na sherehe za pamoja tena,

wanajamvi tuhabarishane, UDINI UPO HUKU MITAANI AU IKULU??
nawakilisha.
 
Uko Ikulu na Mjengoni pale Dodoma, tunausubiri kwa hofu sana hapa Mtaani kwetu! Sijui itakuwaje ukifika hapa na hivi wazee wa Bible majamvia kwao n mwiko itakuwa balaa, Hata hivyo hatuwahi kuziona Spika za Misikitini kama kero, Nadhani huo Udini unaishi Ikulu na Mjengoni tunaomba usije huku kwetu maana tunapendana na kujaliana mno kama watanzania na sio kama watu wa dini moja
 
Uko Ikulu na Mjengoni pale Dodoma, tunausubiri kwa hofu sana hapa Mtaani kwetu! Sijui itakuwaje ukifika hapa na hivi wazee wa Bible majamvia kwao n mwiko itakuwa balaa, Hata hivyo hatuwahi kuziona Spika za Misikitini kama kero, Nadhani huo Udini unaishi Ikulu na Mjengoni tunaomba usije huku kwetu maana tunapendana na kujaliana mno kama watanzania na sio kama watu wa dini moja

mkuu hilo ndo neno kubwa, inabidi sisi wa chini tuukatae kwa nguvu zote huo udini japo viongozi wetu wanatumia mamlaka na uwezo na sauti tena kupitia vyombo mbali mbali, hata mihimili mikubwa ya nchi kama bunge kututangazia sisi wachini ili tuupokee, HATUDANGANYIKI NG'OO!! wabaki na biblia zao na misahafu yao huko huko bungeni na ikulu.
 
Usihofu sana kwani udini hadi sasa upo ikulu na ndani ya ccm tu. Haujatoka nje ya wigo huo. Sasa fikiria utoke ikulu na ccm hadi ufike tabata lini!!!
 
Mimi ni mluteri na mke wangu ni mwislamu. Kila siku ninapata mgao wangu kama kawaida inapokuwa ni sahihi kwetu sote, hajawahi kuniambia kuwa mimi ni kafiri kwa hiyo sina haki ya kutapa epo kutoka kwake. Udini ni kitu ambacho kiko out of bounds kwenye kibanda chetu.
 
inabidi tusali, tushikamane watanzania wote......
tusije ingia kwa Waisrael na Wapalestine.......
maana vita vya kidini haviishagi...
itanza na sisi,watoto zetu, wajukuu wetu, vitukuu vetu........n.k
kama Muislam msikitini kwa sana, kama Mkristu Kanisani kwa sana, na kama we ni Budah ingia kwenye tample....n.k
Tuombe amani...
Ni borea tuishi maskini kuliko kingia kwenye vita vya kidini.....
 
Zumbe,

Unaitwa Mtanzania, una haki kukaa popote utakako maana ni nyumbani kwako, kwa asili.
 
Jamii hivi ni kweli muafaka wa CCM na CUF ndio unaoleta gumzo la UDINI hapa kwetu? na tutegemee mpasuko mkubwa ndani ya CCM wakati wa uchaguzi mkuu ujao wa 2015?
 
Status
Not open for further replies.
Back
Top Bottom