On the grassroots level hakuna suala kama hilo maana Tanzania ni multi religious society na watu wanaishi vizuri na kushirikiana vizuri hata katika sherehe za kidini au misiba, hili suala la udini toka juu ni mstuko mkubwa sana kwa wananchi, ni kosa kubwa sana kama viongozi wanataka kupata mamlaka kutumia kitu kama dini ambacho ni sensitive and deadly kama historia inavyoonyesha. Kwa kweli inasikitisha, maana jamii ya kitanzania inachnaganya sana dini, utakuta hata katika familia moja kuna wakristo wa dhehebu mbalimbali, kuna Waislamu, nk. Watu wana uhuru wa kidini na wanapendana in spite of their religious affiliations. Sasa "rais wa nchi" anapohutubia taifa na kusema juu ya udini, anatoa message gani kwa wananchi ambao hawajawahi kuona kuwa hiyo ndio issue katika jamii zetu? Je, kweli watanzania walihitaji kusikia hilo kama jambo muhimu? Je, yako wapi yale ambayo ndio kweli muhimu kwa watu ambao wanakufa kwa maradhi, umaskini, etc? Watanzania tusidanyanyike na maneno statements ambazo zina lengo la kuficha the real truth. Ukweli ni kwamba Watanzania sio wajinga, tunajua athari za kutumia udini kuchonganyisha watu; mifano hai iko. Nchi kama Indonesia ambayo ni largely Islamic country imeonyesha mfano mzuri wa kidemokrasia na inasifiwa kwa jinsi ambayo imefanikiwa sana kutochanganya siasa na udini na kufungua milango kwa demokrasia ya kweli bila kuchochea watu kutumia udini. Sasa viongozi wetu wanatuchukua totally deadly approach ya udini kuzima demokrasia, tunakwenda wapi kama watanzania tutawasikiliza watu kama hao? Wakati watu wakiamua kupigina kwa maswala ya kidini unafikiri hao wakubwa watadhurika? Wao wana ulizni wa kutosha na fedha za kukimbia nje, je, mwananchi wa kawaida ana uwezo huo? Juzi juzi tu hapa Kenya walipotumia ukabila na kupigana baada ya uchaguzi wa 2007, je, akina Raila na Kibaki walidhurika? Wananchi tusidanganywe na hao wakuuu wambao kazi yao ni kututumia sisi wadogo kupata riziki zao by all costs even the cost of our lives. Hilo bora kila mmoja wetu lazima awe macho. Hakuna dini inaamini juu ya chuki na maangamizi ya uhai....