Elections 2010 Ni nani aliyeingiza udini kwenye kampeni hizi?

Elections 2010 Ni nani aliyeingiza udini kwenye kampeni hizi?

Status
Not open for further replies.
Agenda ya udini imesukumwa mbele na CCM baada ya kuzidiwa na vuguvugu la wanaharakati wakati wa kampeni za uchaguzi mkuu kama kete yao ya mwisho ili kuwatisha wapiga kura. Sasa uchaguzi umeisha bado wanasukuma agenda ya udini ionekane ndio kipaumbele ili kuzima agenda za wanaharakati wanaodai tume huru ya uchaguzi ionekane agenda yao sio kipaumbele. Hatudanganyiki. Tanzania hakuna udini CCM ya JK ndio inataka kuleta udini
 
Hakuna udini Tanzania ila mawazo ya udini yanaingizwa vichwani mwa wananchi.
Mawazo hayo yakifanyiwa kazi yakawa vitendo, hali itakuwa mbaya sana.
Ni muhimu sana mjadala huo ufungwe!

Ni kweli kabisa!wananchi wa Tanzania hawana udini,bali wanasiasa ndiyo wanaotaka kuleta udini!!
 
On the grassroots level hakuna suala kama hilo maana Tanzania ni multi religious society na watu wanaishi vizuri na kushirikiana vizuri hata katika sherehe za kidini au misiba, hili suala la udini toka juu ni mstuko mkubwa sana kwa wananchi, ni kosa kubwa sana kama viongozi wanataka kupata mamlaka kutumia kitu kama dini ambacho ni sensitive and deadly kama historia inavyoonyesha. Kwa kweli inasikitisha, maana jamii ya kitanzania inachnaganya sana dini, utakuta hata katika familia moja kuna wakristo wa dhehebu mbalimbali, kuna Waislamu, nk. Watu wana uhuru wa kidini na wanapendana in spite of their religious affiliations. Sasa "rais wa nchi" anapohutubia taifa na kusema juu ya udini, anatoa message gani kwa wananchi ambao hawajawahi kuona kuwa hiyo ndio issue katika jamii zetu? Je, kweli watanzania walihitaji kusikia hilo kama jambo muhimu? Je, yako wapi yale ambayo ndio kweli muhimu kwa watu ambao wanakufa kwa maradhi, umaskini, etc? Watanzania tusidanyanyike na maneno statements ambazo zina lengo la kuficha the real truth. Ukweli ni kwamba Watanzania sio wajinga, tunajua athari za kutumia udini kuchonganyisha watu; mifano hai iko. Nchi kama Indonesia ambayo ni largely Islamic country imeonyesha mfano mzuri wa kidemokrasia na inasifiwa kwa jinsi ambayo imefanikiwa sana kutochanganya siasa na udini na kufungua milango kwa demokrasia ya kweli bila kuchochea watu kutumia udini. Sasa viongozi wetu wanatuchukua totally deadly approach ya udini kuzima demokrasia, tunakwenda wapi kama watanzania tutawasikiliza watu kama hao? Wakati watu wakiamua kupigina kwa maswala ya kidini unafikiri hao wakubwa watadhurika? Wao wana ulizni wa kutosha na fedha za kukimbia nje, je, mwananchi wa kawaida ana uwezo huo? Juzi juzi tu hapa Kenya walipotumia ukabila na kupigana baada ya uchaguzi wa 2007, je, akina Raila na Kibaki walidhurika? Wananchi tusidanganywe na hao wakuuu wambao kazi yao ni kututumia sisi wadogo kupata riziki zao by all costs even the cost of our lives. Hilo bora kila mmoja wetu lazima awe macho. Hakuna dini inaamini juu ya chuki na maangamizi ya uhai....
 
CUF should have won election because majority of Tanzanians are Muslims.Shame to CCM, with smear tactics and incumbent president loses 20 percent? I am astonished.
 
Tuukatae udini kwa nguvu zetu zote,kwa akili zetu zote na kwa moyo wetu wote, makanisani na misikitini na mitaani na kwenye sehemu zote za kazi. Tunachohitaji ni maisha bora kwa kila Mtanzania.
 
Udini,ukabila ni silaha ya mwisho kwa anguko la Jk na CCM YAKE ,hv ni nani anayewaza udini Tanzania ....ni hao wenye njaa ya madaraka na kulinda madaraka ......!Hili ni zao la ombwe la uongozi,nchi yetu imefika hatua uongozi umekuwa kama suala la kuigiza ,maadili yamemomomnyolewa kwa kiwango cha kutisha ,uzalendo ndio kabisa .Leo ni mtumishi gani wa umma mwenye moyo wa nchi ....hayupo ,katika vipimo halisi vya ubinadamu hayupo! kwa matendo yanayofanywa na watawala wetu na wakuu wa utimishi hayaleti matumaini hata kidogo.
Hebu tafakari suala moja tu,viongozi wa juu...mawaziri wanahusishwa na kughushi vyeti vyao vya shule ,wanakaa kimya na bado wanapeta ,kama ni uongo kwa nn wasimfkishe mahakamnai aliyewazushia ! Tabia hii inawafundisha nini watoto walioko shule !
Ndio maana masual ya kijinga kama udini yanaibuka ....MZIZI mambo yote ni Uongozi MBAYA uliozalishwa na MCHAKATO WA UCHAGUZI WA 2005,....NA HUU ni mwanzo tu .....kuna mengi yanakuja ,HAKI HUINUA TAIFA KINYUME CHAKE .......!
 
Wanaopandikiza udini kuanzia viongozi, watu wakianza kubaguana kidini watapata faida gani? mifano ya nchi ambazo ni dini moja na bado hawana 'mshikamano', amani, na 'utulivu' kama sisi ipo mingi sana.Tukianzia Africa wasomali majority ni waislam na wanaongea lugha moja.
Mimi ninachojifunza ni kwamba watanzania hatudanganyiki pamoja na kwamba kuna mijitu iko bize kutugawanya kwa dini.Tena dini zenyewe za kuletewa. Aibu yao!
 
KIKWETE NDIYE ANAYEHUBIRI HABARI HIZO.
JANA KULIKUWA NA AROBAINI MTAANI, WAKRISTO KWA WAISLAMU WALIKUWA BEGA KWA BEGA.
SIMUELEWI KABISA HUYU PREZIDAA WA BONGO FLEVA:A S crown-1:
 
CUF should have won election because majority of Tanzanians are Muslims.Shame to CCM, with smear tactics and incumbent president loses 20 percent? I am astonished.
Haaa haaa haaaaa !!!
 
Hakuna udini Tanzania ila mawazo ya udini yanaingizwa vichwani mwa wananchi.
Mawazo hayo yakifanyiwa kazi yakawa vitendo, hali itakuwa mbaya sana.
Ni muhimu sana mjadala huo ufungwe!

Nakuunga mkono kabisa, hiki kitu kinatengenezwa kwenye mindset za watu, nawachukia mno waanzilishi wake.....
 
Kama utafuatilia mtoaji mada wa kwanza kabisa utakuta anulizia swala laudini kushika kasi wakari wa rais kikwete. Ninavyokumbuka ni kua kikwete alizungumzia madhara ya udini baada ya kushinda uchaguzi. kwahiyo maneno ya Mwal Nyerere kua mtu anakimbilia udini hayawezi kuapply hapo.

Kama ukiangalia sana swala la udini kati ya Dr Slaa na Dr kikwete ni wazi kua kwa upande wa Dr Slaa udini unajionyesha wazi zaidi kwani wabunge wake wengi ni wakristo na yeye mwenyewe ni mkiristo, upande wa kikwete wabunge wake wengi na mawaziri wake wengi ni wakiristo na yeye mwenyewe ni muislam.

Sidhani kuwa madai ya mtoa mada yananguvu sana. Anachotakiwa kufahamu mtoa mada ni kua serikali haina dini lakin watu wake wana dini. Ni afadhali kukawa na masharti yanayoeleweka ya mtu kuajiriwa kuliko anavyodai yeye. Dini always zitakuwepo kwahiyo ni afadhali kukubali matokeo na kujaribu kuziaccomodate kuliko kujaribu kudanganya na kusema kua hazina athari katika jamii unless dini mija itokomee kabisa duniani kitu ambacho sioni kua kinaweza kutokea in the near future.
 
Kama utafuatilia mtoaji mada wa kwanza kabisa utakuta anulizia swala laudini kushika kasi wakari wa rais kikwete. Ninavyokumbuka ni kua kikwete alizungumzia madhara ya udini baada ya kushinda uchaguzi. kwahiyo maneno ya Mwal Nyerere kua mtu anakimbilia udini hayawezi kuapply hapo.

Kama ukiangalia sana swala la udini kati ya Dr Slaa na Dr kikwete ni wazi kua kwa upande wa Dr Slaa udini unajionyesha wazi zaidi kwani wabunge wake wengi ni wakristo na yeye mwenyewe ni mkiristo, upande wa kikwete wabunge wake wengi na mawaziri wake wengi ni wakiristo na yeye mwenyewe ni muislam.

Sidhani kuwa madai ya mtoa mada yananguvu sana. Anachotakiwa kufahamu mtoa mada ni kua serikali haina dini lakin watu wake wana dini. Ni afadhali kukawa na masharti yanayoeleweka ya mtu kuajiriwa kuliko anavyodai yeye. Dini always zitakuwepo kwahiyo ni afadhali kukubali matokeo na kujaribu kuziaccomodate kuliko kujaribu kudanganya na kusema kua hazina athari katika jamii unless dini mija itokomee kabisa duniani kitu ambacho sioni kua kinaweza kutokea in the near future.

Wewe ulikuwa wapi wakati JK anafanya kampeni za udini kwa kutumia magazeti ya Rostam Aziz, habari leo, Alnur, TBC, n.k?
 
It reminds me of something that was cooked up during Hitler's reign in German...........his propagander minister used all the lies on earth to make the germans believe that the source for their misery were the JEWS,,the mechanism that was used was pretty simple was to feed the masses with all sorts of lies about Jews, coz a "A lie once repeated people start to believe in it" that wat they are trying to do ryt now....
and surely that what CCM and it leaders are trying to feed us with...''LIES"................
I should say this....TANZANIA HAMNA UDINI........kama utatokea kweli basi itakua ni matokeo ya chama tawala kuvunja umoja wetu kama watanzania kwa manufaa yao binafsi ya kutaka kubakia madarakani daima dumu,ili kutuacha sisi kama watanzania tukitoka katika msingi wetu wa kuhoji,kukosoa na kupinga mambo wanayoyafanya wao ambayo yanaigharimu nchi yetu....na kuhamia kunyoosheana mikono eti wewe dini gani??????????????
.....................................WATANZANIA NA TUWE MAKINI TENA SANA.............................
 
Hakuna udini Tanzania bali kuna dhana ya udini,na dhana hii imeasisiwa na Kikwete na wana mtandao wake kwa nia ya kuwagawa watanzania wakati wa uchaguzi, na kusema kweli imemsaidia Kikwete na CCM yake,tatizo ni kuwa hiyo ni mbegu ameipanda na kadiri siku zinavyokwenda itamea na kustawi na pengine wakati huo hatakuwepo madarakani.Dhambi hii kamwe haitamuacha huru Kikwete ndiyo maana anaweweseka kuomba vyombo vya habari vimsaidie kuing'oa mbegu hii. Alaaniwe JK, ilaaniwe CCM. Kama Mungu aishivyo muasisi wa udini huu lazima aangamien yeye kwanza kabla watu hawajaanza kutoana macho.
 

Msomaji Raia




Uchaguzi Mkuu umekwisha, kilichobaki ni historia iliyowekwa na uchaguzi huo. Rais Jakaya Kikwete akizindua bunge la kumi amesema; uchaguzi huu umeacha majeraha kadhaa, kubwa sana likiwa la udini.
Walio karibu naye wanasema kuwa hata katika maandalizi ya hotuba yake hiyo alikuwa ametaja watu anaodai wanahusika na jeraha hili wakiwamo viongozi wa dini na wana habari. Kwa kuwa hakudiriki kuwataja kwenye hotuba yake, si vema kumhukumu kwa hili.
Kazi moja ya watu walio karibu na Rais ni kueneza uvumi na hili la kutaja majina ya watuhumiwa wa udini linaangukia mlengo ule ule wa kujipendekeza kwa Rais. Lakini pia ni vema kujiuliza kwa nini Rais amechagua jeraha la udini wakati kuna majeraha mengi yameachwa na uchaguzi huu.
Lipo jeraha la wizi wa kura ulioanzia katika kura za maoni; lipo jeraha la donda ndugu la rushwa katika uchaguzi; lipo jeraha la tume ya uchaguzi kuelemewa na mashinikizo ya dola na chama tawala ili kutangaza matokeo yenye utata; lipo la kutumia vyombo vya dola kuwapiga na kuwajeruhi wapiga kura kana kwamba wamefanya makosa kupiga kura; lipo la idadi ndogo ya waliojitokeza kupiga kura; na lipo la chama tawala kuwazuia wagombea kushiriki midahalo ya wazi ili wapiga kura wapate kuwahoji.
Yako majeraha mengi, lakini Mheshimiwa Rais amechagua jeraha la udini. Makala hii inajadili dhana hii ya udini kama ilivyojitokeza katika hotuba za Rais, wakati wa kampeini na wakati anazindua bunge.
Nirudie tena kusisitiza mambo machache ya msingi kuhusiana na mjadala huu. Kwanza, Jakaya Kikwete alikuwa Mwislamu alipogombea mwaka 2005. Ndani ya CCM aligombea na Wakiristo lakini akachaguliwa yeye. Katika uchaguzi nkuu wa mwaka huo, akagombea na Wakiristo, akashinda kwa kishindo kikubwa akiwaacha mbali sana Wakiristo.
Mwaka huu, Jakaya bado ni Mwislamu yule yule. Amegombea akipambana na baadhi ya Wakiristo. Hakushinda kwa kishindo kama alivyotegemea. Dai lake la udini yawezekana linaanzia hapa. Kwa dhati naamini kuwa wapiga kura walimjua kuwa ni Mwislamu 2005 na 2010. Kilichobadilika ama ni ufahamu wa wapiga kura au uwezo wa kuongoza wa Jakaya.
Ninapata shida kuamini kuwa mabadiliko haya kama yana uhusiano na dini ya Jakaya au dini ya waliopiga kura.
Jambo la pili, nashawishika kuamini kuwa Jakaya anapotamka neno “viongozi wa dini” katika hotuba zake anamaanisha “maaskofu, mapadre na wachungaji”. Nitaeleza. Mara kadhaa amelalamika katika vikao vya ndani ya chama kuwa maaskofu hawampendi.
Hivi sasa kamati za siasa za CCM katika wilaya na mikoa yote zinafanya tathmini ya uchaguzi, na inavyoelekea kuna maelekezo maalumu yaliyotolewa “kuwashughulikia” maaskofu na wachungaji wanaodaiwa kutokuiunga mkono CCM.
Siku chache kabla ya uchaguzi, wakuu wa mikoa waliagizwa kuwaita “viongozi wa dini” ili kuwatisha na kuwaeleza masikitiko ya Jakaya juu ya udini. Badala yake, walioitwa ni maaskofu tu.
Kuna malalamiko kutoka pande zote za nchi kuwa wakuu wa wilaya wanakataa kutoa barua za utambulisho kwa madhehebu ya Kikiristo kwa ajili ya misamaha ya kodi. Kwa ujumla tathmini ya uchaguzi mkuu ndani ya CCM imegeuka zoezi la kutafuta mchawi aliyesababisha ushindi mdogo kwa CCM.
Jakaya Kikwete anaujua ukweli lakini anaukwepa. Mwaka 2005, watu wengi walikuwa hawajamjua Jakaya kwa undani. Miaka mitano ya utawala wake, imeonyesha nyufa za kutisha katika uwezo wake wa kufanya maamuzi ya kuwaletea watu maisha bora aliyoyaahidi.
Hata ndani ya CCM, upo mgawanyiko mkubwa wa maoni juu ya uwezo wa Jakaya katika kukiongoza chama na serikali yake. Kwa hiyo, waliopiga kura kumkataa Jakaya mwaka huu, waliukataa uwezo wake mdogo wa kuongoza, hawakuikataa dini yake. Wapo waliokataa chama cha Jakaya lakini hawana tatizo na Jakaya.
Chama chake kinakabiliwa na matatizo makubwa na sehemu nyingi nchini sasa hakikubaliki. Waliokikataa chama si kwa sababu ya udini kwa sababu CCM haina dini ya kukataliwa.
Liko kundi jingine japo ni dogo ambalo halina shida na Jakaya, halina shida na CCM kama taasisi, lakini lina shida na umakini wa sera za CCM. Hawa nao hawakumchagua Jakaya kwa sababu labda kwa bahati njema safari hii waliona sera zinazovutia katika chama kingine. Hawa nao hawakuongozwa kufanya hivyo na kiongozi yeyote wa dini.
Ni uzembe wa hali ya juu kufikiri na hatimaye kusema kuwa makundi haya matatu hapo juu, yana udini.
Liko suala la ufisadi katika mjadala wa kitaifa. CCM walidhani litapita kama yalivyowahi kupita mengine. Jitihada za kuwafikisha baadhi ya vigogo mahakamani hazijasaidia kuzima mjadala huu. Uamuzi wa kupuuza suala la ufisadi katika kampeni za CCM hazijasaidia kuufanya mjadala usishabikiwe na wapiga kura.
Propoganda za makada wa CCM kuwa CHADEMA hakina agenda nyingine zaidi ya ufisadi, hazikusaidia kuzima kiu ya watu kutaka kujua undani wa ufisadi. Hii ni kwa sababu, ufisadi hauna dini wala itikadi hata kama unaweza kukumbatiwa bila shida na chama fulani.
Kwa bahati mbaya, hata ndani ya CCM wamo waliojeruhiwa na ufisadi. Wapo waliofukuzwa kazi au kunyimwa haki fulani kwa sababu tu walishabikia mjadala huu. Kwa maneno mengine, agenda ya ufisadi inawaunganisha Watanzania bila kujali dini zao.
Kwa kuwa maisha ya Watanzania kiuchumi yanazidi kuwa mabaya, wapiga kura wengi lazima wapige ramli kutafuta sababu ya kuwapa usingizi wa muda. Na sababu nyepesi inayovutia ni ufisadi uliotamalaki kila sekta ya umma katika taifa letu.
Uamuzi wa CHADEMA kuufanya ufisadi kuwa moja ya agenda kuu katika kampeni zake, uliiweka CCM mahali pagumu sana kwa sababu, wanaoitwa mafisadi katika taifa letu ni wana CCM.
Kutokana na kuwa CCM imekuwa madarakani kwa nusu karne, ni wazi kuwa mafisadi na wahujumu wa uchumi, watakuwa ni wale walio au waliowahi kuwa katika tabaka tawala. Mpaka hapa, ni vigumu kuitakasa CCM na ufisadi kwa kutumia maneno matupu.
Liko kundi kubwa la wapiga kura walioamua kutoipigia CCM kwa sababu ya jinsi CCM inavyoshughulikia suala la ufisadi nchini chini ya Jakaya. Hawa nao walipiga kura kuukataa ufisadi, si dini ya Jakaya wala ya wagombea wa chama cha Jakaya.
Nayasema haya kwa sababu, wagombea wa CCM walioanguka kwa ngazi za udiwani na ubunge, wamo Waislamu kwa Wakiristo. Hali kadhalika walioshinda ni wa dini zote mbili.
Ni matusi kwa wapiga kura kuanza sasa kuwasingizia dhambi ya udini eti tu kwa sababu CCM imeonekana kukataliwa katika sehemu mbalimbali hapa nchini. Dhambi ya udini haiwezi kuonekana kwa kuikataa CCM tu, na pale CCM inaposhinda ionekane hakuna udini.
Anayepalilia fikra hizi ndiye anayepandikiza fikra za udini na Watanzania tuwe macho naye.
Imefikia mahali ikakubalika kuwa kupiga vita ufisadi ni kuipinga CCM na Jakaya amekwama katika fikra hizi nyepesi! Hata maaskofu anaowakamia Jakaya ni wale waliowahi kusimama na kukemea ufisadi na ndipo Jakaya na wenzake wakadhani maaskofu hao wanaipinga CCM.
Ikiwa sasa imekubalika kuwa ufisadi maana yake ni CCM, na kuwa maaskofu walipinga ufisadi wakadhaniwa wanaipinga CCM, basi nawashauri wakubali “kushughulikiwa” na serikali ya Jakaya kwa sababu thawabu yao ni kubwa mbele za Mwenyezi Mungu na waja wake walio hapa Tanzania.
Nayasema haya kwa sababu naamini kwa uthabiti wa moyo wangu kuwa ufisadi hauna dini.
Wako pia wanaohoji kwa nini chini ya utawala wa Jakaya, mijadala ya kidini ndipo imeibuka na kupoteza muda mwingi wa watu. Hivi sasa ofisi ya Waziri Mkuu inatumia muda mwingi na fedha nyingi kuratibu uanzishwaji wa Mahakama ya Kadhi na fedha nyingi za walipa kodi zimeishatumika bila kuwajulisha Watanzania kuwa mahakama hii imo mbioni kuanzishwa kwa gharama za serikali japo inadaiwa kuwa ikianzishwa “haitaendeshwa” na fedha za serikali.
Kama serikali haitaiendesha mahakama hiyo kwa nini imetumia mabilioni kuianzisha?
Ni wakati wa Jakaya suala la kujiunga na OIC limechukua sura mpya na sasa Wizara husika iko mbioni kurasmisha hatua za kujiunga.
Kwa wenye akili wangedhani madai ya CHADEMA ya kuharakisha Katiba mpya yangekubaliwa haraka ili Katiba hiyo sasa itamke kuwa Serikali yaTanzania ina dini kuliko ilivyo sasa inapotamka kuwa haina dini wakati inatumia fedha kuanzisha taasisi za kidini!
 
Sijui km hili swali limejificha kiasi hicho............udini ni kwa mfano kikwete kuweka mambo ya dini ya kiislamu kwenye ilani ya ccm na kuinadi.......udini na unafiki ni pale unapomsikia kikwete akisema kuna watu wanaeneza udini kwa maneno wakati yeye anaeneza kwa vitendo.............udini ni kwa mfano kikwete kujaribu kuivunja katiba ya nchi aliyoamua kuilinda na kuruhusu mijadala na kwa kutumia kodi za watz kujadili mambo ya kiislamu yaani mahakama na kadhi na oic...............
 
Kweli JK wetu hajui kuchambua mambo. Je hata waliomsaidia wizi wa kura sasa wameanza kuamini uongo walioutumia.
Mwambieni Raisi wetu kuwa tulimnyima kura tena sana baada ya yeye kujitambulisha na MAFISADI kwa kuwakampeinia na kuwanyanyua mikono hadharani tena mchana kweupe!!!

Sasa kama kungekuwa na udini tungempa kura kwa kuwa hao mafisadi aliowakampeinia ni wakristo. Cha ajabu Maaskofu na Wachungaji ndio wanaowashambulia zaidi hawa wakristo wenzao.Raisi wetu haoni kavaa makengeza ya udini. Kaingia na sera ya udini kwenye uchaguzi imebididi achakachuliwe kura kwani aliwaudhi sana wananchi
Alitoka hoi ,kapa bin taaban.
 
Status
Not open for further replies.
Back
Top Bottom