Elections 2010 Ni nani aliyeingiza udini kwenye kampeni hizi?

Elections 2010 Ni nani aliyeingiza udini kwenye kampeni hizi?

Status
Not open for further replies.
enadpo rais atakuwa muislam wa tz, makanisa na baadhi ya waandishi wa habri humskama sana. mfano mh Mwinyi alivyoandamwa na makanisa, akaja mkapa wakaa kimya japo mngi maovu yakifanywa. lkn kaja jk sasa yamerudi hayo hayo. lkn 2015 akija manomkubali kutoka dini yernu mabo kimya

Sasa hao watu wanafanya hivyo (kama kweli wanafanya.... sababu mimi sijagundua hilo..) sababu ya dini yao ni wakristu au wanamatatizo yao mengine...... Na kama hawakumsema Mkapa na alikosea basi lilikuwa kosa lao na si kosa la dini yao... Na kama JK atakosea basi waendelee kumsema na hata hao waislamu ambao watamyamazia basi watakuwa wanakosea
 
ndio maana tz kuna udini. sasa mnakataa nini?
Hakuna Udini kuna wapuuzi wachache ambao ukiwapa sentimita moja watachukua mita moja, hata kama wote tungekuwa dini moja wapuuzi hawa wangeleta ukabila, tungekuwa kabila moja wangeleta maumbile tungekuwa maumbile sawa wangetafuta sababu tu.... hawa wapuuzi hawafai ndugu yangu
 
WAZIRI Mkuu wa zamani, Jaji Joseph Warioba amesema udini unaotajwa kuwapo nchini, hasa baada ya Uchaguzi Mkuu wa mwaka huu, umo miongoni mwa viongozi si wananchi wa kawaida.

Kauli hiyo ya Jaji Warioba ni sehemu ya maoni yake ya maadhimisho ya miaka 49 ya Uhuru wa iliyokuwa Tanganyika, Desemba 9, mwaka 1961 yanayofanyika kesho Alhamisi.

Amesema licha ya viongozi waasisi kufanikiwa kujenga Taifa moja, dalili za sasa si njema na kwamba kasi ya viongozi kugawanyika hata katika vyama vyao vya siasa inaelekea kutishia umoja wa nchi.

Katika mahojiano maalumu na Raia Mwema yaliyochapishwa katika kurasa za tisa na 10 za toleo hili, Jaji Warioba anasema wananchi kawaida wamekuwa wakiendelea na shughuli zao bila kuulizana dini wala kabila zao.

“Wanafanya shughuli zao za kawaida iwe za biashara au uzalishaji. Ukikuta kundi la Wamachinga utawakuta vijana wa kutoka sehemu mbali mbali, dini mbali mbali na kabila mbali mbali wanafanya shughuli moja, hawajibagui hata kidogo.

“Inapofika wakati wa uchaguzi ndipo unasikia haya mambo ya ukabila, ukanda na udini. Haya yanaletwa na hawa ambao wanatafuta madaraka. Hawa wanaotafuta madaraka ndio wameleta matumizi ya fedha katika kutafuta uongozi,” alisema Jaji Warioba.

Katika hatua nyingine, Jaji Warioba ambaye amewahi kuwa Mwanasheria Mkuu wa Serikali wakati wa uongozi wa Mwalimu Julius Nyerere, ameonyesha kukerwa na tabia mpya ya kutojiamini kama nchi kiasi cha kutegemea zaidi wafadhili.

“Kwa nini waasisi wetu walijiamini zaidi kuliko sasa hivi? Mimi nadhani wakati ule TANU inadai Uhuru tukiwa vijana ndiyo tumeingia kwenye siasa, hali ilikuwa ngumu sana.

“Watu wengi walikuwa wanasema huyu Nyerere anahangaika…hana uwezo wa kupambana na Mwingereza amuondoe. Kwamba bila msaada hauwezi kumuondoa Mwingireza lakini walijiamini na Uhuru ukapatikana.

“…sasa hivi hatujiamini tunazungumzia sana ufadhili, Serikali inazungumzia ufadhili, wananchi wanazungumzia wafadhili. Tumekuwa na imani kuwa hatuwezi kufanya chochote bila kuwa na wafadhili.

“ Nadhani tunachohitaji sasa ni kubadili akili na mtazamo wetu. Lazima tujiamini hata raia nao wanasema Serikali itufanyie hivi na hivi. Ni lazima tuanze kujiamini mtu mmoja mmoja mpaka jumuiya nzima.

“ Kama tunaendelea hivi na katika nchi tunasema kuna partners in development (wadau wa maendeleo) maana yake sisi hatuwezi kushughulikia maendeleo yetu bila hao wabia na ubia huo uko wapi zaidi?

“ Sina matatizo na mfadhili ambaye anataka kujua fedha alizotoa zimetumika vizuri, lakini nadhani wafadhili wengi wanatia masharti ambayo ndiyo yanaamua ni sera ya aina gani tuwe nayo na kuitekeleza.

“ Ni kama tumepoteza uwezo wetu wa kuamua sera zetu. Nadhani tuanze kuwa wakorofi katika eneo hili. Inawezekana, kwamba siku hizi mwananchi hahusishwi sana katika kuunda sera zetu, inakuwa ni viongozi na hawa wanaoitwa partners wanakubaliana kisha ndiyo inapelekwa kwa wananchi wakubali au wakatae na mara nyingi wanakubali. Inabidi sasa tuanze kuwa na kiburi kile tulichokuwa nacho.”

Katika kusisitiza anaongeza: “Naamini kama tukiamua kwamba hapana, mambo ya sera tutaamua wenyewe, siamini kama hawa wafadhili watatulazimisha tuwasilikize, lakini nadhani tumezoea hii ya wafadhili. Uhuru wetu sasa unaanza kupungua, kwa mawili yale tuliyoanzisha…umoja wa nchi na uhuru wa kuamua mambo ya nchi yetu tukaweka misingi, haya yameanza kuingiliwa.”

Alionyesha pia kutofurahia kuingia mwaka wa 49 wa Uhuru wa iliyokuwa Tanganyika wakati vyombo vya dola Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (Takukuru) na ofisi ya Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali zikiwa zinaingiliwa kisiasa.


si kweli''
 
Hakuna Udini kuna wapuuzi wachache ambao ukiwapa sentimita moja watachukua mita moja, hata kama wote tungekuwa dini moja wapuuzi hawa wangeleta ukabila, tungekuwa kabila moja wangeleta maumbile tungekuwa maumbile sawa wangetafuta sababu tu.... hawa wapuuzi hawafai ndugu yangu

Ndiyo maana ukaitwa VoiceOfReason you tink well and analize tings man. Dis thugs are cursed man. dem always find reason to take peace off man. dem never want see a mankind in peace man. dem tink different to really mankind man.
Big up VoiceOfReason. i like ur comments man.
 
Nafikiri akina Warioba pia wana mchango katika yote yaliyotokea mpaka hapa tulipofika! labda mimi ni mchanga bado, Hivi katika miaka 30 iliyopita tuliwahi kuwa na waziri mkuu Muislamu? Naomba msaada kwenye hili tuta.
 
Nafikiri akina Warioba pia wana mchango katika yote yaliyotokea mpaka hapa tulipofika! labda mimi ni mchanga bado, Hivi katika miaka 30 iliyopita tuliwahi kuwa na waziri mkuu Muislamu? Naomba msaada kwenye hili tuta.
Una maana kama tungekuwa na waziri mkuu muislam matatizo yangekwisha au kutokuwa na PM mwislam ndiyo sababu ya kuenea kwa udini sidhani kama hizo ni sababu.
 
Nafikiri akina Warioba pia wana mchango katika yote yaliyotokea mpaka hapa tulipofika! labda mimi ni mchanga bado, Hivi katika miaka 30 iliyopita tuliwahi kuwa na waziri mkuu Muislamu? Naomba msaada kwenye hili tuta.
Tukianza kujibu hayo maswali kaka..... tutakuwa tunakwenda ambako siko..... swali ni kuuliza Je mawaziri wakuu waliopita je walifanya kazi yao vizuri.... Lets not look at a person beyond their abilities basi..... tukienda on that road tutaanza kusema hivi tulishakuwa na waziri mkuu, mhaya msukuma, mchagga (ukiuliza why??? , watakujibu ndio makabila makubwa Tanzania).... You see...... This is a dangerous road to go...
 
Kujadili watu kwa misingi ya dini ni UPUMBAVU. Tujenge hoja, siyo kuteteana wala kushambuliana kwa misingi ya dini.
 
Jaji Sinde umesema vema sana katika thread hii!!!!!! ila tu kasoro mojaa kubwa kwamba sijui kama wanaJF nao wataku-rate kama mimi!!!!!!! Sioni tofauti na wanaJF wengine ambao ni walalahoi tu wa kawaida, ambao michango yao husomwa, hufurahiwa kwisha habari!!!!!!!!!
Wewe Jaji Sinde na akina Butiku mmeamua kuisusa CCM na kumwachia muiran na watanzania wendawazimu Lowasa na Chenge wanaangamiza nchi hii, Tanzania aliyotuachia Mwl; yaani ni kama vile hampo, ama mnawaogopa hawa jamaa watatu-au na ninyi mna share katika haya wanayofanya????????????
Mimi nadhani kama ninyi tunaowategemea hamuwezi kutueleza hatua gani mnachukua kunuisuru taifa hili kutoka mikononi mwa genge hili la RA, EC, EL, basi your contribution here ni kututia kichefuchefu!!!!!!!!!!!!!!!Ni heri mnyamaze kabisa!!!!!!!!!!!!
Mmewaachia hawa watu watatu, RA, AC, EL chama na serikali, na bunge, wanafanya kila wanachotaka, utadhani nchi hii tumelogwa sijui?????? Ni heri mnyamaze kama na ninyi mnaishia kuchangia kama sisi walala hoi halafu basi!!!!!!!!!!!
 
You must be sick!! I mean you're seriously sick in your head, you need to see your doctor immediately.

Huyu MS ni bendera fuata upepo tu udini ukiongewa na Kikwete anasema ule si udini ukiongewa na mwingine ni udini, ni ule ushabiki wa kitoto kufuata mdundiko bila kujua ulikotoka na unakoelekea.

quote_icon.png
Originally Posted by Malaria Sugu
hakuna udini, kuna ukiristo dhidi ya uislam?

quote_icon.png
Originally Posted by Malaria Sugu
ndio maana tz kuna udini. sasa mnakataa nini?
 
JAMANI ndugu zangu hapa JF tunaanza kupoteza njia kwa kujadili hoja za watu kama Maria Sugu. Hoja hizo inabidi zipuuzwe kila anapoziweka. Kufanya hivyo kutasaidia kuondoa mambo ya Udini katika post zetu. MS ni mgonjwa na madaktari pale muhimbili wanajua hili kuwa alishakuwa na maralia ya ubongo siku nyingi!!!

NAomba tuendelee kujadili hoja kama ilivyo kwenye Post.
 
Issue ya udini Tanzania inatumiwa na watu hasa viongozi wa kisiasa ili kuwapumbaza wananchi. Inatumika kupoteza muelekeo wa mijadala ya mambo muhimu ya nchi hasa yale yanatokana na utendaji mbovu wa viongozi. Hizi ni mbinu chafu za divide and rule, hawa viongozi wa siasa wanajua kabisa kuwa watanzania wengi wanachukulia dini kama very sensitive issue hivyo ni rahisi sana kuwayumbisha watu kama watasema kuna mgogoro wa kidini hapa nchini. Watu watapoteza uaminifu miongoni mwao na badala ya kuhoji issue muhimu katika nchi wataishia kufikiria mipasuko ya dini na kujenga kutokuaminiana.


Watanzania wanatakiwa wao makini sana na viongozi wanazungumza kuwa kuna migogoro ya dini hapa nchini. Kiukweli kila mtu ana uhuru wa kufuata dini anayopenda, na mpaka sasa watanzania bado wanaishi na kushirikiana kwenye shughuli zao za kila siku bila kujali dini ya mtu. Siku ya Ijumaa waislam wengi wanaende misikitini, na siku ya jumapili wakristo wengi wanaenda makanisani, na watanzania wengine waneenda kwenye shughuli za kuabudu siku yeyote wanayotaka bila kuingiliwa.
 
Hakuna udini wowote, NI MAJI YAMEWAFIKIA SHINGONI, sasa pa kukimbilia kupata SUPPORT wameona waende kwenye udini kwani wanajua kuna baadhi ya Watanzania wasiokaa chini na kutafakari kabla ya kuamua jambo, Watakurupuka na kuwafuata hao
 
Kujadili watu kwa misingi ya dini ni UPUMBAVU. Tujenge hoja, siyo kuteteana wala kushambuliana kwa misingi ya dini.



Hapo umenena kweli ndugu yangu, tupate viongozi kwa misingi ya uwajibikaji na si dini! What is dini by then? Ina maana hata mtu hawezi kazi ili mradi tu awe dini fulani, Ndugu zangu kwa mtindo huu hatuwezi kufika tuendako hata kidogo! Huu ni ufinyu wa fikra na ni watu wachache wanajaribu kupanda mbegu hii mbaya ambayo itavitafuna vizazi vijavyo.
 
Nafikiri akina Warioba pia wana mchango katika yote yaliyotokea mpaka hapa tulipofika! labda mimi ni mchanga bado, Hivi katika miaka 30 iliyopita tuliwahi kuwa na waziri mkuu Muislamu? Naomba msaada kwenye hili tuta.


Ndiyo waziri mkuu muislam alikuwepo naye ni Dr. Salim Ahmed Salim kutoka Zanzibar.
 
Nafikiri akina Warioba pia wana mchango katika yote yaliyotokea mpaka hapa tulipofika! labda mimi ni mchanga bado, Hivi katika miaka 30 iliyopita tuliwahi kuwa na waziri mkuu Muislamu? Naomba msaada kwenye hili tuta.

Wewe una upeo finyu sana. Kwani waziri mkuu anachaguliwa kwa misingi ya dini yake? Mkiambiwa muende shule mfute ujinga uliowajaa hamtaki, sasa angalia ulivyokuwa na mawazo madogo kama ya funza. ( kukusaidia kwani Salm Ahamed Salm, anaamini dini gani? na je alishawahi kuwa waziri mkuu?)
 
Ipo haja ya watu kuuzoea usawa. Watu wote wanaolalamika kwamba kuna udini hawana hata kielelezo kimoja cha kuthibitisha malalamiko yao. Kuna mmoja alikuja humu akasema, kwanini mabalozi wa Tanzania kwenye nchi tajiri wote ni waislamu, akathibitishiwa kwamba kuna mabalozi wengi wakiristo kuliko waislamu kwenye hizo nchi alizoziita tajiri.
Ukweli ni kwamba, huwezi kumkandamiza mwanadamu milele, na wale waliokuwa wakikandamizwa wamejitutumua kuhakikisha kwamba hakuna tena ukandamizaji. Tanzania ina usawa katika swala zima la dini. Lakini dini iliyozoea ukandamizaji haipendi usawa, na ndiyo maana kila siku kuna vilio vya "udini, udini, udini".
Nimesoma University of Pretoria na kwa sababu hiyo basi nina "marafiki" ambao ni boers, Afrikaans. Nilikutana na wawili Melbourne mwezi August mwaka huu na wakalalamika kwamba South Afrika ni nchi ya kibaguzi na inapendelea watu weusi. Kwa wale wenye kuijua historia ya South Afrika, na pia wenye kuijua South Afrika ya sasa, wengi hawatakubaliana nao, isipokuwa waafrikaan wenzao.
Waafrikaan walikuwa wamezoes ukandamizaji na kuanza kuamini kwamba wao ni juu ya wengine, sasa suala la usawa hawalitaki kwa sababu linawaweka sawa na wengine. Na hapa nyumbani hali kadhalika.
Mtauzoea tuu usawa.
 
Status
Not open for further replies.
Back
Top Bottom