Elections 2010 Ni nani aliyeingiza udini kwenye kampeni hizi?

Elections 2010 Ni nani aliyeingiza udini kwenye kampeni hizi?

Status
Not open for further replies.
Shiefl, usilaumu kabla hujaangalia level of understandings za hawa watu wa makundi mawili. Utaumiza moyo wako bure. Tatizo siyo sisiem, tatizo ni watu. Natamani kabla sijaitwa kiongozi wa dini walau nihudhurie madarasa kadhaa kupanua kiwango cha uelewa wangu. Natamani niwaze kwanza kabla sijaongea mbele ya kamera badala ya ninavyofanya sasa... This is shame!
 
For sure CCM inachungulia kaburi lakini kila mchungulia kaburi haachi kupiga piga miguu, kik yao ya mwisho na wanayofikiri itawasaidia ni kupandikiza udini ili angalau wapate watu wa kwenda nao wasianguke wenyewe, i mean wakianguka wapate sababu kwa jamii kuwa tumeanguka kwa sababu ya udini.

Ndiyo maana Kikwete baada ya kuona umaarufu wake umeshuka kitu ambacho kiko wazi akaona salama yake ni kusingizia kuwa kashindwa kwa sababau ya dini yake. Sasa anajitahidi kufanya kila tukio lionekane linasababishwa na tofauti ya dini za watu, nenda vyuoni, kwenye siasa, kwenye vyeo kila sehemu siku hizi lazima ihusishwe dini tofauti na zamani kitu ambacho ni hatari sana.
 
Lakini nafikiri kuna ukweli , kwani hata hiyo picha yako ni ya kuchochea udini, sasa unafikiri nani utakae nae chini na kukusililiza wa dini nyingine?!
"Actions speak louder than words."
 
Watu wenye mawazo mafupi kama nyie ndio mnaouziwa udini na kuusambaza bila kujijua kuna avatar za watu wanatoboana utumbo hizo utasema zinahamasisha mauaji, short sited.
 
CCM nd'o wananaotumia silaha ya kugawa watu kwa dini ili wadumu madarakani. Mfan. Mwak 95 ,walipomwona mrema ni tishio kwao, ccm walijipendekeza kwa waislam wamlaani mrema nk. 2000/05 CUF ndio walikuwa tishio kwao, ccm ikajiweka upande wa wakristo wakidai cuf chama cha waislam. Sasa 2010-chadema wananguvu ccm wamegeuka wamejiweka na waislam tena wakidai cha wakiristo. Maaskofu wametoa tamko ccm imewashauri mashehe nao watoe tamko la kuwabeba ccm.. Kwa mifano hiyo watanzania tuwe macho na CCM. -- mdini ni nani hapo ?
 
Kuna ndugu yangu yupo Nzega kanitumia ujumbe kwenye sms unasema hivi;
Laa mzee M.MUNGU HAMFICHI Mnafiki. Maaskofu hatimaye wajihirisha kuwa chadema ni chama chao walipopinga matokeo ya umeya Arusha. Katibu wa CCM mkoa wa Arusha aliwapaka kishenzi , kuwa wakasajili chama chao ili waje kugombeya wasijifanye wanasiasa uchwara, wala hatashiki na matamshi yao. Chadema wamekuwa wajinga, unashindaje ukiwa unazidiwa wajumbe? Mbona hawadai uspika kuwa haukuwa wa haki!. Vipi kuna mapya kwenye internet?.

Hii ndiyo DHANA ya UDINI ilivyo na pia inaonyeha Udini uko wapi. Mwanzoni sikuielewa thread hii lakini ndugu yangu huyu kanisaidia kuielewa.
Naomba mwanzilishi anikosoe! Nimefikisha.

Mimi nadhani Watanzania tuachane na kufikiri kijinga kama M.M.Kijiji anavyotuasa. Una data gani kusema hivyo?
Mawazo kama haya yanajidhirisha pia jinsi gani tunafanya uamuzi. Sishangai serikali kukazania tuilipe kampuni ya kitapeli kwani viongozi wake wana mawazo kama yako na si rahisi kuchanganua kipi ni kibaya au kizuri. Ushauri wangu kwa wana JF wote ni huu: kwamba kama mtu anatoa 'claims' bila data tumpinge toka mwanzoni hadi hapo atakapoleta data na kuzisimamia. Let's argue things intelligently!
 
Udini hautokani na jina la mtu
wapo wenye majina ya kkiristu wameapa kwa qorani na wabunge wa majina ya kiislamu wameapa kwa bible
 
mzee nilidhani umesema "dhana ya udini" ndiyo ipo; lakini pia unasema "udini ukoje na uko wapi"?

Mzee Mwanakijiji, jana niliuliza swali kama hili kwa mfanyakazi mwenzangu, ambaye ni Mwislamu. Niliuliza: Udini Tanzania upo? Akajibu: Tena sana! Nikamwuliza tena, unapokaa mtaani upo? Akajibu haupo. Nikasema sasa hiyo "tena sana" inatoka wapi? Akasema uko kwenye taasisi - wanasiasa na viongozi wa dini wa ngazi za juu. Kisha ikabidi aseme: "Udini una Wakristo".

Aliendelea kusema Ukristo hapa Tanzania umewanyima Waislamu fursa za kusoma na kupata ajira nzuri serikalini hadi leo hii. Alisema pia hata waasisi wa Tanzania wengi waliluwa Waislamu lakini majina yao yameondolewa kwenye vitabu vya historia na Wakristo kwa maslahi ya kukuza Ukristo. Alisema shule za msingi wanafunzi wengi ni Wailsamu lakini wanaoenda sekondari au chuo kukii ni wachache. "Kwa nini?" aliuliza.

Alismea pia Rais Jakaya Kikwete kuchagua Wakristo wengi mawaziri na Waislamu wachache amezingatia utendaji kazi na siyo udini. Alismea mambo mengi ya kuonesha Waislamu siyo wadini ispokuwa Wakristo. Ila mimi nilisema hiyo ni 'prejudice' na 'suspicion' ya bure isiyosaidia chochote. Nilisema eneo ninakotoka mimi watoto kutoka familia za Kiislamu siku za wikiends wanaenda madrassa. Lakini wa Wakristo mara nyingi wanakwenda kula kitabu. Nikasema ukizingatia hilo utakuta kwamba pamoja na matatizo mengi tuliyo nayo, wanafunzi wanaweza kufanya vizuri ni Wakristo ukilinganisha na Waislamu. Mimi nilihitimisha kwa kusema tatizo la kusoma au kupata ajira linatokana na priorities na siyo ubaguzi wa kidini.

Ukisoma 'between the lines' utakuta kwamba wanaosema udini upo wanasema pia "wadini ni Wakristo". Lakini ni ukweli usiopingika kuwa shule nyingi, hospitali nyingi na nadhani hata vituo vya kulelea watoto yatima na wa mitaani hapa Tanzania viko chini ya Wakristo na sijawahi kusikia kama kuna mtu anabaguliwa kwenye huduma wanazotoa. Hata baadhi ya vituo vya radio vilivyo chini ya taasisi za Kikristo kama Radio ya St Augustine University Mwanza ina wafanyakazi ambao ni Waislamu na hata baadhi ya walimu wa St Augustine University ni Waislamu kuachilia mbali wanafunzi.

Kwa nini Waislamu wafikiri Wakristo ni wadini na wao wafikiri ni 'wadini-free'? What's behind here? Na baadhi ya topics kwenye mihadhara ya Waislamu inakuwa na ujumbe wa namna hiyo... watoto wanaaminishwa kuwa wanabaguliwa kwa misingi ya dini na Wakristo! Is it true? Pale Mbagala Mission kuna hospitali ya Kanisa Katoliki (inaendeshwa na masista). Ukienda pale utasikia majina ya akina mama wengi wajawazito au wenye watoto wanaoenda kliniki Amina, Hadija nk na wengine wamevaa hijabu na sijasikia wakisema wanabaguliwa kwa vile ni Waislamu. Anayebisha anaweza kwenda au kumtuma mtu aende pale kuanzia Jumatatu-Jumamosi aone hospitali hiyo inavyojaa watu wa kila aina na anaweza kuthibitisha yeye mwenyewe aidha kwa kuona au kusikia majina yanayoitwa hapo hospitali.
 
You don't need to go very far. Rais wao Ni MUISLAM. Makamu wake ni Muislam, Jaji mkuu ni Muislam, Jamaa wa Uslama wa taifa ni muislam. Zanzibari yooooooooote ni Waislam.

kile ni Chama Cha Muham-mad
 
You don't need to go very far. Rais wao Ni MUISLAM. Makamu wake ni Muislam, Jaji mkuu ni Muislam, Jamaa wa Uslama wa taifa ni muislam. Zanzibari yooooooooote ni Waislam.

kile ni Chama Cha Muham-mad
Akili za kushikiwa..

Mwasisi wa CCM ni JK.Nyerere(mkatoliki aliye simikwa utakatifu).
Iweje leo utuambie ccm ni chama kwa ajili ya waislam?
 
You don't need to go very far. Rais wao Ni MUISLAM. Makamu wake ni Muislam, Jaji mkuu ni Muislam, Jamaa wa Uslama wa taifa ni muislam. Zanzibari yooooooooote ni Waislam.

kile ni Chama Cha Muham-mad

Hahahahahahahaha hii nilikuwa sijaijua!
 
Umoja wa Mashehe na Maaskofu jana kwenye mazishi Arusha tayari imetubainishia NDUMIRAKUWILI wa kugawa taifa kwa kigezo cha udini ni CCM. Tangu pale hakuna madhehebu kati ya hizo mbili ambazo zitadanganywa tena na CCM na hoja kama hiyo tena maishani.

Mbinu zote chafu za CCM sasa hivi kweupe uwanjani.
 
You don't need to go very far. Rais wao Ni MUISLAM. Makamu wake ni Muislam, Jaji mkuu ni Muislam, Jamaa wa Uslama wa taifa ni muislam. Zanzibari yooooooooote ni Waislam.

kile ni Chama Cha Muham-mad

Umefilisika kimawazo, muone daktari. UPUPU MTUPU
 
Ulikuwa unategemea nini kutoka kwa padiri aliefukuzwa kanisani kwa zinaa?

Inabidi ajipendekeze kanisani kuonekana kuwa anajali kanisa, na huku ana mke wa mtu! Na dini na wadhifa wake hauruhusu hilo. ukishangaa ya Musa utayaona ya Slaa!
 
Kweli CCM imechezea akili za watu muda mrefu sana kwa kuvipakazia vyama kuhusu udini na miaka yote (except 2010) wamekuwa wakifanikiwa! Thanks God wameshashtukiwa hawana pa kujificha!
 
Ulikuwa unategemea nini kutoka kwa padiri aliefukuzwa kanisani kwa zinaa?

Inabidi ajipendekeze kanisani kuonekana kuwa anajali kanisa, na huku ana mke wa mtu!
Na dini na wadhifa wake hauruhusu hilo. ukishangaa ya Musa utayaona ya Slaa!

kunaweza kukawa na kaukweli hapo
 
Sasa mbona mmechelewa sana kung'amua haya? CCM ni genge la wezi wanaotumia siasa kama smoke-screen kutekeleza mambo yao ya kijambazi. Hivyo it is no news kama watazusha lolote lile of any magnitude ili mradi waendelee kushibisha matumbo yao na vimada wao.
 
Status
Not open for further replies.
Back
Top Bottom