Tindo
Platinum Member
- Sep 28, 2011
- 72,020
- 129,293
Sheria huwa hazifanyi kazi kuangalia nyuma. Zinaanzia sasa kwenda mbele. Hivyo Kikwete na Samia watakuwa salama, kitisho kwao ni familia zao. Lakini tatizo kubwa ni tabia yetu ya kulipa visasi, hofu yao ni wakiingia wengine wanaweza wasijali katiba inasema nini, wakawafanyizia.Unajua Katiba mpya inaweza kusema Raisi alie madarakani au ambae alikuwa madarakani tangu tupate uhuru anaweza kushitakiwa ikiwa jopo la majaji 5 wa Mahakama ya Katiba wataona kuna ulazima wakufanya hivyo?
Kwa sababu itakuwa ni Katiba mpya, itakuwa imebatilisha sheria za katiba ya zamani, kwa hiyo ikiwa kutakuwa na ulazima wakuwafungulia mashitaka Kikwete au Samia kwa mujibu wa Katiba mpya, itawezekana