Ni nani aliyepitisha Katiba ya Rais kuwekewa kinga?

Ni nani aliyepitisha Katiba ya Rais kuwekewa kinga?

Katiba haina shida na ndiyo maana ilituongoza vizuri hadi 1992 wakati wa vuguvugu la vyama vingi.

Ila Katiba siyo kitabu kitakatifu ambacho hakiwi amended/ reviewed.

Kwangu mimi kuwalaumu walioandika na kupitisha Katiba ya mwaka 1977 siyo sahihi. Wanaopaswa kulaumiwa ni wale wa mwaka 2014 chini ya JK waliotumia Tsh 400 Bilioni bila kutuletea Katiba
Tatizo ni utaratibu unaotumika kupitisha katiba mpya. Mfano tunapenda wabunge wasiwe mawaziri. Kumbuka kila mbunge anafukizia uwaziri. Je, Bunge litaafiki kupitisha sheria hiyo katika katiba mpya?

Hivyo katiba mpya inafaa iandaliwe na kupitishwa na watu wasikuwa na interest zao katika katiba mpya
 
Tufanye Nakubaliana na wewe, so kiongozi mkuu hata akifanya madudu ni sahihi asiguswe?
Usisahau katiba inamlinda.
Kwanini unawatetea wa 1977 na hawakuwa sahihi pia?
Kila jambo lina wakati wake. Yawezekana kwa wakati wanaandika walikuwa na sababu zao maana ilikuwa era ya chama kimoja.

Ndiyo maana sioni tija kuanza kupoteza muda ku-challenge katiba ya 1977 na mazingira yake. Tuwalaumu wale waliofuja Tsh 400 Billion bila kutuletea Katiba.

Wale walio abandon Rasimu ya Warioba na kuchomekea Rasimu ya Chenge
 
Hivi kwa akili yako, hata katiba mpya itapita bila Samia kuwekewa kinga baada ya kutoka madarani?
Mkuu umepiga kwenye bull kabisa hapo. Hayo ndiyo mazingira yaliyopelekea kuipeperusha Rasimu ya Warioba kwa kuwa ilikuwa na hicho kipengele.

Walikosa busara kidogo. Ningekuwa mimi ningeshauri waweke Disclaimer kuwa Katiba hii haitafanya kazi retrospectively.
 
Mkuu umepiga kwenye bull kabisa hapo. Hayo ndiyo mazingira yaliyopelekea kuipeperusha Rasimu ya Warioba kwa kuwa ilikuwa na hicho kipengele.

Walikosa busara kidogo. Ningekuwa mimi ningeshauri waweke Disclaimer kuwa Katiba hii haitafanya kazi retrospectively.
Nafurahi kupata mtu anayenielewa katika kambo hili. Jinsi ya kufanya ni kwanza kuruhisu kuwepo ma mgombea huru. Baada ya hapo kuweka kifungu katika sheria kuwa mtu yeyote atakayeandaa na kupitisha katiba asiruhusiwe lugombea au kuajiriwa serikalini kwa muda wa miaka 20. Tatu hiyo uliyosema kuwa Samia katiba imlinde. İli baadaye kwa vile kuna mgombea huru akaangwe
 
Kinga ya raisi, ilianza tangu mwanzo haya mambo yaliopoanza, kwa bwana mmoja mwenye upeo wa mbali kuwazidi wenzie, akiamini mfumo wa siasa wa vyama vingi kwa nchi yetu baada ya uhuru, ingekua tatizo kutokana na uchache wa walio elimika kwa watu wake, kwaio Hawa waliofata walifatisha mfumo ambao tayari umewekwa.., na uzuri zaidi Sasa huu mfumo ata kama wewe ni mpinzani mkubwa wa mwenzio au chama Cha mwenzio, ukiingia wewe bado huu mfumo kwako unakua ulinzi kulingana na siasa za nchi yetu. Ki uhalisia wewe na Mimi tunaona ni mbaya lakini ukweli kwa sababu tupo nje ya huu mfumo, lakini si kumoja kama ungekua top, nadhani ungeweza kubadili vyote, ila sio mfumo ambao ukimalza madaraka yako unakua ulinzi kwako, mfano mdogo kipindi Cha magu, bila huo mfumo, kuna mtu ungemletea madhara makubwa, na hata mfano yeye mwenyewe kama angemaliza bila ya hio Kinga. Kwaio nadhani kuhusu hio Kinga sidhani kama vyama vyengine siku vikishika hatamu tofauti na chama tawala, wataweza kuondoa hio Kinga...
 
Na yote hayo yakifanyika, mwanasheria mkuu akiwa warioba ambaye naye leo analialia utafikiri wakati wanaipitisha ile katiba alikuwa amebwia konyagi

Naam wala sipingani na wewe ni kweli Warioba alikua AG pengine hakujua madhara yake kwa wakati huo ila sasa ameyaona , kwa rasimu yake ya 2014 alijisahihisha ndio maana hata wahuni walimtumia jambazi la Kolomije
images - 2026-08-07T064453.088.jpeg
likamzabe kofi , Warioba kwangu kajisahihisha hana deni na alisimama pia dhidi ya October 29 kwangu hana deni pia.

Mzee wa hovyo kwangu namba moja ni Butiku.
 
Tatizo ni utaratibu unaotumika kupitisha katiba mpya. Mfano tunapenda wabunge wasiwe mawaziri. Kumbuka kila mbunge anafukizia uwaziri. Je, Bunge litaafiki kupitisha sheria hiyo katika katiba mpya?

Hivyo katiba mpya inafaa iandaliwe na kupitishwa na watu wasikuwa na interest zao katika katiba mpya
Tufanye kama Kenya. Walioshiriki kuandika katiba mpya walizuiwa kushiriki siasa kwa muda fulani baada ya katiba kupitishwa.
 
Sheria huwa hazifanyi kazi kuangalia nyuma. Zinaanzia sasa kwenda mbele. Hivyo Kikwete na Samia watakuwa salama, kitisho kwao ni familia zao. Lakini tatizo kubwa ni tabia yetu ya kulipa visasi, hofu yao ni wakiingia wengine wanaweza wasijali katiba inasema nini, wakawafanyizia.
Mbona sheria ya pension mfano kikokotoo inaanza kutumika kwa wote immediately baada ya kubadilishwa. Kwanini isiwe inatumika kwa wale wanaopata kazi kuanzia siku sheria imebadilishwa
 
Unajua Katiba mpya inaweza kusema Raisi alie madarakani au ambae alikuwa madarakani tangu tupate uhuru anaweza kushitakiwa ikiwa jopo la majaji 5 wa Mahakama ya Katiba wataona kuna ulazima wakufanya hivyo?

Kwa sababu itakuwa ni Katiba mpya, itakuwa imebatilisha sheria za katiba ya zamani, kwa hiyo ikiwa kutakuwa na ulazima wa kuwafungulia mashitaka Kikwete au Samia kwa mujibu wa Katiba mpya, itawezekana.

Tumpe challenge Pascal Mayala ikiwa tukiweka kipengele hiki kwenye "Katiba Mpya" kitatupa njia ya kuwafungulia mashitaka Kikwete na Samia ikiwa kuna makosa ya kuwapeleka mahakamani, kwa mujibu wa Katiba Mpya.

Principle hapa ni kwamba hatuwezi kuwa na Katiba Mpya ikitumika sambamba na Katiba ya zamani. Katiba Mpya inabatilisha kanuni zote za Katiba ya zamani, pamoja na sheria ya kinga za raisi kushitakiwa. Ni wazi Samia au Kikwete wakishitakiwa hawawezi kusema nilifanya jambo hilo ovu kwa sababu Katiba ya zamani iliniruhusu - itakuwa ni kujitia hatiani kwamba walifanya jambo walilojua lilikuwa ovu kwa sababu tu walijua wana kinga ya kikatiba.
Kumbe!
 
Back
Top Bottom