Ni nani waliongeza cha juu kwenye manunuzi ya ndege ya mizigo?

PM anasemaje hapa.. Maana ndio alienda hadi kiwandani
 
Hizi ndege zinanunuliwa kwa sababu kuna mwanya wa kuiba pesa , si kweli kwamba Atcl inahitaji ndege,
Hitaji tunalo ila shida ipo kwenye manunuzi yaani wanaingia fisi kuongeza cha juu wapige manoti. Serikali imefanya busara kuikubali ripoti iende bungeni kujadiliwa bungeni haya ni mazingira ya uwazi. Huko nyuma prof alietumbuliwa alibainisha kuwa aliomba karatasi za manunuzi ya ndege akanyimwa. Watanzania tumshauri Rais kisayansi jinsi anaweza kukati angalau mizizi kidogo ya wizi maana inaonekana imejichimbia chini.
 
Hasara za Shirika la Ndege Tanzania (ATCL) kwa miaka 9 (2014-2022)

2014/2015 - Tsh. Bilioni 94.3
2015/2016 - Tsh. Bilioni 109.2
2016/2017 - Tsh. Bilioni 113.8
2017/2018 - Tsh. Bilioni 26.6
2018/2019 - Tsh. Bilioni 48
2019/2020 - Tsh. Bilioni 60.24
2020/2021 - Tsh. Bilioni 36.2
2021/2022 - Tsh. Bilioni 35.2

Ripoti za Mkaguzi na Mdhibiti Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG), zimeendelea kuonesha Shirika la Ndege Tanzania (ATCL) limeendelea kupata hasara tangu Serikali ilipoamua kulifufua kwa kununua ndege mpya 12.

ATCL imekodishwa Ndege 11 zilizonunuliwa kwa Tsh. Tril 1.47 zinazotoa huduma ya Usafiri sehemu mbalimbali ndani na nje ya Nchi, baadhi yake zimepata hitilafu za kiufundi na 1 inashikiliwa Nchini Uholanzi.
 
Hamna cha kutupisha wala nini, ilitakiwa wawe ndani.
 
Kwa wabunge waliopatikana uchaguzi 2020 ambapo upinzani ulidhulumiwa , Bado unaamini bunge linaweza kufanya kazi yake kwa weledi?
 
Katika vitu nilivyowahi kushangaa ni hao walamba asali kwenda kutoa taarifa ya ndege ya ATCL ikamatwe huko SA na huko Ulaya ili wapate udalali kweli wahuni sio watu wana laana ya asili...sijawatofautisha na wale wanasimama mahakamani na Mama yao aliejenga nyumba wakiigombania kama mzazi mmoja alitangulia mbele za Haki...
 
Shirika la ndege la Tz alijawahi kuleta faida yoyote na hasara ya ma billion hiyo pesa ingewekezwa kwa kupeleka maji vijijini huenda maisha ya mtazania wa kawaida yange badilika.
 
Kuna hili jingine huku..Uuuwiii kweli kila mtu anakula kwa urefu wa kamba yake

Rais wa Tanzania, Dkt. Samia Suluhu Hassan leo wakati akipokea Ripoti ya Mkaguzi Mkuu wa hesabu za Serikali (CAG) Ikulu Jijini Dar es salaam amehoji kuhusu mikopo chechefu na kusema kuna baadhi ya Maafisa wa Benki wanashirikiana na Wateja kupitisha mikopo kinyume na inavyotakiwa kisheria.

“Kuhusu mikopo chechefu na yenyewe unajiuliza why mikopo chechefu?, hivi ingekuwa Benki zinazotoa mikopo ni Benki binafsi kwenye rekodi zao kungekuwa na mikopo chechefu?, kusingekuwa, wetu sisi wa Serikali wanashindwa nini mpaka kunakuwa na mikopo chechefu?, kuna ushirikiano baina ya Maafisa wa Benki na hao wanaoenda kukopa, andika nitakupitishia ukipata chako hiki changu hiki, hailipiki tunasema mikopo chechefu”

“Kuna Mtu, Mfanyabiashara kakopa Benki zetu sita sijui tano Mabilioni kila Benki, kachukua fedha yetu kaitoa nje na yeye kaondoka, leo tunasema mikopo chechefu mlipompa huyu!, dhamana zote alizoweka ni feki, zote feki, kama sio ushirikiano kitu gani?

Lakini Watu wanazunguka tunawatazama, wapo na wanajua walichokifanya, hii mikopo chechefu itachechemea mpaka tujirekebishe na inapochechemea na Nchi inachechemea”

WANAJAMVI HEBU TUJUZANE HUYU ANAYETAJWA HAPA NI NANI?

View attachment 2570068
 

mkono wa rais mstaafu ndio uliowaweka walaji mama hana ubavu wa kuwaondoa ndio maana kawaomba watupishe
 

Wawafukuze tu na hela zetu je? Unamfukuza kwa kumwachia mtaji? Kamata mbane arudishe mali na akafie gerezani huko
 

hana ubavu maana wezi wamewekwa na rais mstaafu ndio maana mama kakasirika kabaki kutukana tena mwezi mtukufu
 
Duh, hatari sana!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…