Ni nani waliongeza cha juu kwenye manunuzi ya ndege ya mizigo?

Hivi ile trillion 1.5 iliyomfukuzisha kazi Assad iliishia wapi?

CAG alipotaka kuhoji gharama za manunuzi ya ndege (ambazo hazikuidhinishwa na bunge na Wala haikutangazwa zabuni kama Sheria ya manunuzi ya umma inavyotaka) akaambiwa aende ikulu yaani aachane na hiyo issue hukuona hilo? Bunge liliidhinisha ujenzi wa Chato International Airport? Kandarasi ya ujenzi ilitangazwa Ili makampuni ya ujenzi yashindanishwe? Kadhalika Burigi national park n.k n.k? CCM haikuwahi kuwa na msafi acha kujidanganya
 
Sema mama analalamika sana na hakuna watu wakumsaidia, huwezi ukasikia kuna chombo chochote cha serikali hasa polisi au takukuru kuwa wanafanyiakazi report ya jana.Hii nchi hatutafika kamwe..yaani kuanzia JUU mpaka CHINI wote wanalalamika
Si mliambiwa bunge lenu ni dhaifu mkaishia kum harass CAG Prof Assad na kumfurusha ofsini kibabe
 
Unamzungumzia yule mpigaji wa trillion 1.5 au
 
Hapa katikati si tuliambiwa ATCL imepata faida wakatoa na gawio[emoji23][emoji23][emoji23]
 
Sio mtu tunahitaji mifumo narudia tunahitaji mifumo thabiti
 
Mipuuzi itaanza kusema aliyeweka cha juu ni JPM inadhani na sisi ni ndondocha kama myenyewe
Hahahah hamtaki JPM aguswe kabisa, hivi Prof Assad alipohoji gharama za manunuzi ya ndege na upotevu wa trillion 1.5 akaliwa kichwa ilikuwa ni utawala wa nani vile
 
Hahahah hamtaki JPM aguswe kabisa, hivi Prof Assad alipohoji gharama za manunuzi ya ndege na upotevu wa trillion 1.5 akaliwa kichwa ilikuwa ni utawala wa nani vile
Tatizo hamkumjua JPM au kwa kutojua au kwa makusudi. Nitaanzisha sredi kuhusu ukweli wake
 
Haya mambo kipindi cha numa yalikuwa yanafichuliwa na vyama vya upinzani lakini saiv imekuwa tofauti...R.I.P upinzani
Na ndio maana inasemwa,asiyeutaka upinzani huyo ni mwizi bobezi anayetaka madudu yake yasiwekwe hadharani.
 
Tatizo hamkumjua JPM au kwa kutojua au kwa makusudi. Nitaanzisha sredi kuhusu ukweli wake
Tatizo mahaba yanakupofusha, angalia ripoti ya CAG Toka 2014 ATCL inapata hasara ya mabilioni ya pesa ila hapo katikati tuliambiwa ATCL imepata faida wakatoa na gawio? Halafu Kwa Nini ripoti ikionyesha ubadhilifu wa kuanzia 2016-2020 mnachukia na kusema sio kweli ila ukionyeshwa wa sasa mnafurahi sana
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…