Ni ngumu sana kumpata mchumba/mpenzi asiyetanguliza pesa mbele kizazi hiki

Kijana atafute pesa kwanza hao watu hawana ungwana bila pesa wote wako vile
Nadhani ujamuelewa pitia Tena uzi wake soma kwa umakini taratibu utamuelewa na kama hauelewa nitakuelewesha
 
Nakupinga kwa asilimia zote. Sababu yangu ni hii: Watu wengi hamjui maana ya sentensi ''kutanguliza fedha mbele''. Mtu kusema au kuzingatia mwenza awe na chanzo cha mapato kwa ajili ya matumizi ya kila siku huko siyo kutanguliza fedha mbele. Watu wote duniani wanafanya kazi ili kupata kipato cha kuendeshea maisha. Mwanamke kwa mfano, atakuwa mtu mjinga sana kama atakimbilia kuolewa na mtu asiye na kipato chochote. Kutanguliza fedha mbele maana yake haswa ni ile hali ya mke/mume kupenda fedha kupita kiasi kwa hali zote bila kujali kuna kupata na kukosa.
 
Wewe ndio umemuelewa vizuri mtoa mada Covax Beesmom Simara njooni hapa mtoa mada azungumzii mwanaume kukosa hela au kutokuwa na hela anachozumzia wanawake wamekosa ile staha ya kiuwanawake badala yake wamejikuta wanaweka tamaa mbele. Kwasisi Wanaume tunaojitambua tunapima wanawake kutokana na matendo yao kujua je huyu ni wakugonga au wakuanzisha maisha nae
 
Nazungumia hawa omba omba wanajifanya kama special group mbovu unakuta mshahara anakuzunguka hata mara 2 ila bado tu ana omba omba pesa zako wewe mwamba umevaa kiatu mpaka kimepinda yeye anaviatu pesa 14 na bado anakuomba mpunga wa kunununa viatu
Hao sasa ndiyo wanatanguliza fedha mbele. Na mara nyingi hili hutokea kwa wanaume wanaolazimisha mapenzi. Ukiona mwanamke anakutumia namna hiyo ujue huyo hakupendi bali anapedna fedha zako. Lakini mwanamke anayetaka mwenza wake awe ni kipato cha kuendeshea maishi ili amkubali huyo hatangulizi fedha mbele bali anatanguliza kanuni za kawaida kabisa za maisha.
 
Nadhani ujamuelewa pitia Tena uzi wake soma kwa umakini taratibu utamuelewa na kama hauelewa nitakuelewesha
Naomba mkuu unieleweshe zaidi ntashukuru sanaa kwa ufafanuzi wako
 
ukichukua namba ya mwanamke ikapita siku 3 toka muanze kuchat hajasema ana shida ya vocha vocha...anaumwa...hajalaaa...kodi imeishaa...gas imeisha...anataka akasuke ila hana hela AISEEE huyo kidogo anajitambua. ila siku hizi ukiomba namba cha kwanza mwanamke anakuwa yatima hapo hapooo wew nod unakuwa baba yake πŸ˜€ πŸ˜€
 
Kwahiyo tumsaidiaje Sasa?πŸ™„πŸ˜πŸ˜ 
 

Okaay nimekuelewa Mkuu
 
Sisi wanawake tuna shida sana, unapenda hela ili hali wewe mwenyewe hata elfu 10 huwezi tafuta? Mimi mahusiano yangu hayajajengwa au hayapo kwa ajili ya kupata hela kwa mwanaume. Tupo kwa ajili ya ku enjoy na kujenga familia.
Dada unajitambua hiv umetoka kabila gani?
 
Dada unajitambua hiv umetoka kabila gani?
Kabila sidhani kama linamfanya mtu ajitambue, maana kuna wa kabila langu pia wana tabia hizo. Wanawake tusipojitambua tutashushwa thamani yetu. Na kadri siku zinavyozidi kwenda ,haya mambo ya kupewa pesa hayatakuwepo unless uwe unajiuza.
 
Wengi ni wakugonga tuu mwanawane. Wakuweka ndani ni wacahache sana. Wanawake wenyewe wanakuja na kauli mbofu mbofu eti hela yangu nitachangia nikitaka....sasa nani anataka mwanamke kama huyo awe mke.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…