Kama ni mfuatiliaji wa mambo unaweza kuona kuwa hata jana Raisi akiingia kumuaga Kijazi kuna umbali uliwekwa kati yake na wasaidizi wake.Kujibu swali lako ni kuwa maisha ya Raisi yanakuwa hatarini kwa kuwa karibu na mtu ambaye anaweza kumuambukiza ugonjwa wa hatari.Mfano kama mtu wa karibu wa rais akifa kwa korona hali ya afya ya rais inakuaje?
Rais ni kiongozi Mkubwa sana kiasi ambacho afya yake ikitetereka hata uchumi unaweza kuanguka.
Sidhani kwa hali ilivyo JPM anaweza tena kutoka na kuchanganyika na watu wa mtaa wa Congo na akifanya hivyo ina maana idara yetu ya kumlinda imeshindwa kutumia mamlaka yake.
Tumewahi Barack Obama akiingia mtaani na hata kula mkahawani lakini ukiangalia kwa makini tayari eneo lipo chini ya ulinzi mkali.