Ni nini kazi ya Katibu Mkuu Kiongozi?

Ni nini kazi ya Katibu Mkuu Kiongozi?

Katibu Mkuu Kiongozi ni Mtendaji Mkuu wa Serikali. NinKatibu wa Baraza la Mawaziri. Yeye ni Mtumishi wa Umma. Huteuliwa na Rais lkn husalia ofisini pindi Rais anapomaliza muda wake na humpokea Rais ajaye. Rais ajaye huamua kuendelea naye au kuteua mwingine. Nilichokiona kila Rais hupenda kwenda na safu yake. Tatizo ukiondolewa kwenye hiyo nafasi lazima utapewa ubalozi tu akaishi huko uhamishoni ili usiathiri huku
 
Kwa hiyo ni kama katibu wa serikali. Ana kazi muhimu sana. Kwa nini hii kazi asiifanye waziri mkuu na badala yake PM anazururazurura tu?
Waziri mkuu anakosa kazi hadi anaishia kuponda barakoa za mabeberu wakati huo huo kavaa suti iliyonunuliwa kwa mabeberu.
 
Yaani ni kama Mungu na mwanae wa pekee, Yesu Kristo, ukaribu wa Mkuu wa nchi na Katibu Mkuu kiongozi. Sijui umeelewa? Maana tukikupa vifungu vya sheria ujue wajibu wa CS, hutajua vema. Umeelewa au bado umelewa?
Naona umeamua kukufuru, tubu mapema sana
 
Hapa napata swali lingine...
Mbona kama hakuwa na ulinzi wa kumlinda kivileee.. maana kwa maelezo yako.. yeye ni mtu mwenye siri nyingi sana za nchi
Uliwahi kumrushia hata kibunzi tu halafu ukaachwa uendelee na mishe zako ?
 
Katibu Mkuu Kiongozi ni Mtendaji Mkuu wa Serikali. NinKatibu wa Baraza la Mawaziri. Yeye ni Mtumishi wa Umma. Huteuliwa na Rais lkn husalia ofisini pindi Rais anapomaliza muda wake na humpokea Rais ajaye. Rais ajaye huamua kuendelea naye au kuteua mwingine. Nilichokiona kila Rais hupenda kwenda na safu yake. Tatizo ukiondolewa kwenye hiyo nafasi lazima utapewa ubalozi tu akaishi huko uhamishoni ili usiathiri huku
Balozi Ombeni Sefue alipostaafu hakwenda popote kuwa balozi.

Luhanjo alipomaliza muda wake, hakwenda kuwa balozi sehemu yoyote.

Mzee Opio baada ya kumaliza muda wake hakupewa ubalozi.

Sina hakika John Rupia nae alipewa ubalozi wakati anamkabidhi ofisi Marten Lubanga.

Ambae Alikuwa katibu mkuu kiongozi wakati wa Rais Mkapa ni Marten Lubanga, alipewa ubalozi wakati Rais Kikwete alimchukua Philemon Luhanjo kuwa kati Katibu Mkuu kiongozi.
 
Ndiye administrator mkuu wa ikulu anayesimamia mambo ya kiutawala kwa wafanyakazi wote wa Ikulu pamoja na wale walioteuliwa na rais. Kwa marekani anaitwa Chief of Staff.
Apa kuna mkanganyiko na majukumu wa katibu wa ikulu ni yapi?
 
Red Giant kama ni mpenzi wa series pakua na angalia moja inaitwa Designated Survivor utaelewa kazi ya katibu mkuu kiongozi, kule wanaita Chief of staff.
Designates Survivor,
24 Series
Scandal
Madam Secretary
Homeland season 7 na 8

24 Series na scandal zimeonesha kwa kina kazi za Chief of Staff kwa uzito mkubwa sana ambae majukumu yake ndio kama Chief Secretary hapa kwetu.
 
Kuna vilaza wengi huko mitaani hawajui hata katibu mkuu kiongozi ni nani hasa wamama,mwajabu Madela wa tandale ukimwambia katibu mkuu kiongozi hakuelewi
 
Kwa mnao mlinganisha chief secretary na chief of staff Wa marekani mnakosea. Mamlaka ya chief of staff Wa marekani yanaanza Na kuishia west wing. Hakuna chief of staff Mwenye mamlaka kwenye wizara yeyote marekani. Kwetu chief secretary ni Mkubwa Wa makatibu wakuu wrote. Kwenye utumishi wa uma usiokua Na siasa hakuna Mkubwa kumzidi. Yeye ni mkuu Wa utumishi Wa umma maana yake ndo mtumishi Wa umma namba moja. Pia ni katibu Wa baraza la mawaziri. Ni mjumbe asiyekua na kura kwenye baraza la mawaziri. Huandaa ratiba Na mihutasari ya yatokanayo na vikao hivo. Yeye ndiye mshauri namba moja Wa raising kuhusu mambo ya utendaji Wa serikali. Ndo kiungo kati ya siasa Na utendaji.

..Wamarekani pia wana Chief of Staff ambaye anafanana zaidi na Katibu Myeka wa Raisi wa Tz.

..vilevile Chief of Staff wa Marekani ni mjumbe na sehemu ya Cabinet ya Wamarekani.
 
Unataka awe na ulinzi kama wa Makonda?Gari anayotumia sio STK bali CS (chief secretary).Naamini alikuwa analindwa vizuri na ni mtu aliyekuwa very busy.
Anyway awamu hii kuna matumizi mabaya ya ving'ora na misafara kwani hiyo ni haki yako kuona kama alikuwa halindwi sana (relative to other state officials)

..siku hizi misafara imekuwa mingi sana.

..awamu ya kwanza na ya pili kulikuwa na msafara wa raisi, makamu, waziri mkuu, na katibu mkuu wa chama/ccm.

..wengine wote wakiwemo Mkuu wa Majeshi, Mnadhimu Mkuu, IGP, Jaji Mkuu, Chief Secretary, etc walikuwa hawana misafara
 
Hapana umekosea. Katibu mkuu wa Ikulu yupo na ana majukumu kama ya makatibu wakuu wengine wa wizara.

Katibu mkuu kiongozi siyo Chief of Staff bali ni Chief Secretary na ndiye mwenyekiti wa makatibu wakuu wengine wa wizara. Yeye ni mkuu wa watumishi wa umma wote yakiwemo mashirika na taasisi za serikali. Yeye ndiye katibu wa Baraza la mawaziri ambalo mwenyekiti wake ni Rais.
Pia ni mw/kiti wa wakuu wa vyombo vya usalama. Ni kiongozi mkubwa .
 
Kwa hiyo ni kama katibu wa serikali. Ana kazi muhimu sana. Kwa nini hii kazi asiifanye waziri mkuu na badala yake PM anazururazurura tu?
Ndiyo maana umeambiwa Katibu mkuu kiongozyni mtendaji zaidi lakini waziri mkuu Ni cheo Cha kupiga siasa zaidi.
 
Kwa lugha nyepesi tunaweza sema kazi yake ni kuendesha serikali....kwenye website yake kuna list ya majukumu yake, ni mazito kweli kweli

1613848547946.png


Source: Chief Secretary Roles
 
Apa kuna mkanganyiko na majukumu wa katibu wa ikulu ni yapi?
Neno Katibu lisinguangaishe; wewe angalia ni katibu gani. Kuna Katibu Myeka wa Rais, Katibu wa Ikulu, na kunaweza kuwa na katibu wa chochote kile, swali hapa ni kazi ya "Katibu Mkuu Kiongozi" anayepambanuliwa kwa kuwa Mkuu na pia Kiongozi.
 
Ndiye administrator mkuu wa ikulu anayesimamia mambo ya kiutawala kwa wafanyakazi wote wa Ikulu pamoja na wale walioteuliwa na rais. Kwa marekani anaitwa Chief of Staff.
Umechanganya bwana, siyo Katibu wa Ikulu! Huyu ndiye kiongozi mkuu wa Utumishi wa Uma kiserikali.

Pakiwa na uchaguzi huyu anaendelea kuongoza kawaida kwakuwa ni mtumishi. Huyu ni tofauti na katibu wa Ikulu au Katibu wa Rais
 
Apa kuna mkanganyiko na majukumu wa katibu wa ikulu ni yapi?
Katibu mkuu wa Ikulu majukumu yake ni usimamizi na utendaji wa shughuli za kila siku ofisi ya rais kiutalaamu zaidi yaani kwa kifupi huyu majukumu yake ni yale yale anayoyafanya katibu mkuu wa wizara yoyote Ile.

Kwa upande wa katibu mkuu kiongozi huyu ni mkuu wa makatibu wakuu wote akiwemo huyo huyo katibu mkuu Ikulu. Kiutendaji wa serikali ya Tanzania watumishi wote wa umma na taasisi za serikali wapo chini ya makatibu wakuu kulingana na taasisi husika ilipo ktk wizara. Hii humfanya katibu mkuu kiongozi kuwa mkuu wa watumishi wote wa umma pamoja na taasisi zake.

Kwa kifupi huyu katibu mkuu kiongozi ni sawa na waziri mkuu kabisa tofauti mmoja ni kiongozi wa kisiasa anachaguliwa na wananchi wa kawaida kupitia sanduku la kura ila huteuliwa na rais wadhifa huo kusimamia UTENDAJI wa shughuli za serikali ila kwa upande wa katibu mkuu kiongozi yeye ni MSIMAMIZI NA MTENDAJI wa shughuli za serikali kila siku na si mwasiasa huyu yeye yupo kitalaamu zaidi.
 
Kikatiba ni mtumishi wa umma lakini kiutendaji ni mtu wa karibu mno na kiongozi wa nchi .Ni mkono wa kulia wa Rais.Yeye ndiye mkuu wa watumishi wa umma,ndiye kiongozi wa makatibu wakuu wote,NI KATIBU WA BARAZA LA MAWAZIRI (Baraza la mawaziri ndiyo serikali yenyewe).Kwa ujumla baada ya Rais ndiye mtu wapili kujua mambo actually karibu yote ya serikali.
SI MTU MDOGO HATA KIDOGO!!
Na katibu ikulu?
 
Back
Top Bottom