Ni nini kazi ya Katibu Mkuu Kiongozi?

Katibu Mkuu Kiongozi ni Mtendaji Mkuu wa Serikali. NinKatibu wa Baraza la Mawaziri. Yeye ni Mtumishi wa Umma. Huteuliwa na Rais lkn husalia ofisini pindi Rais anapomaliza muda wake na humpokea Rais ajaye. Rais ajaye huamua kuendelea naye au kuteua mwingine. Nilichokiona kila Rais hupenda kwenda na safu yake. Tatizo ukiondolewa kwenye hiyo nafasi lazima utapewa ubalozi tu akaishi huko uhamishoni ili usiathiri huku
 
Kwa hiyo ni kama katibu wa serikali. Ana kazi muhimu sana. Kwa nini hii kazi asiifanye waziri mkuu na badala yake PM anazururazurura tu?
Waziri mkuu anakosa kazi hadi anaishia kuponda barakoa za mabeberu wakati huo huo kavaa suti iliyonunuliwa kwa mabeberu.
 
Yaani ni kama Mungu na mwanae wa pekee, Yesu Kristo, ukaribu wa Mkuu wa nchi na Katibu Mkuu kiongozi. Sijui umeelewa? Maana tukikupa vifungu vya sheria ujue wajibu wa CS, hutajua vema. Umeelewa au bado umelewa?
Naona umeamua kukufuru, tubu mapema sana
 
Hapa napata swali lingine...
Mbona kama hakuwa na ulinzi wa kumlinda kivileee.. maana kwa maelezo yako.. yeye ni mtu mwenye siri nyingi sana za nchi
Uliwahi kumrushia hata kibunzi tu halafu ukaachwa uendelee na mishe zako ?
 
Balozi Ombeni Sefue alipostaafu hakwenda popote kuwa balozi.

Luhanjo alipomaliza muda wake, hakwenda kuwa balozi sehemu yoyote.

Mzee Opio baada ya kumaliza muda wake hakupewa ubalozi.

Sina hakika John Rupia nae alipewa ubalozi wakati anamkabidhi ofisi Marten Lubanga.

Ambae Alikuwa katibu mkuu kiongozi wakati wa Rais Mkapa ni Marten Lubanga, alipewa ubalozi wakati Rais Kikwete alimchukua Philemon Luhanjo kuwa kati Katibu Mkuu kiongozi.
 
Ndiye administrator mkuu wa ikulu anayesimamia mambo ya kiutawala kwa wafanyakazi wote wa Ikulu pamoja na wale walioteuliwa na rais. Kwa marekani anaitwa Chief of Staff.
Apa kuna mkanganyiko na majukumu wa katibu wa ikulu ni yapi?
 
Red Giant kama ni mpenzi wa series pakua na angalia moja inaitwa Designated Survivor utaelewa kazi ya katibu mkuu kiongozi, kule wanaita Chief of staff.
Designates Survivor,
24 Series
Scandal
Madam Secretary
Homeland season 7 na 8

24 Series na scandal zimeonesha kwa kina kazi za Chief of Staff kwa uzito mkubwa sana ambae majukumu yake ndio kama Chief Secretary hapa kwetu.
 
Kuna vilaza wengi huko mitaani hawajui hata katibu mkuu kiongozi ni nani hasa wamama,mwajabu Madela wa tandale ukimwambia katibu mkuu kiongozi hakuelewi
 

..Wamarekani pia wana Chief of Staff ambaye anafanana zaidi na Katibu Myeka wa Raisi wa Tz.

..vilevile Chief of Staff wa Marekani ni mjumbe na sehemu ya Cabinet ya Wamarekani.
 

..siku hizi misafara imekuwa mingi sana.

..awamu ya kwanza na ya pili kulikuwa na msafara wa raisi, makamu, waziri mkuu, na katibu mkuu wa chama/ccm.

..wengine wote wakiwemo Mkuu wa Majeshi, Mnadhimu Mkuu, IGP, Jaji Mkuu, Chief Secretary, etc walikuwa hawana misafara
 
Pia ni mw/kiti wa wakuu wa vyombo vya usalama. Ni kiongozi mkubwa .
 
Kwa hiyo ni kama katibu wa serikali. Ana kazi muhimu sana. Kwa nini hii kazi asiifanye waziri mkuu na badala yake PM anazururazurura tu?
Ndiyo maana umeambiwa Katibu mkuu kiongozyni mtendaji zaidi lakini waziri mkuu Ni cheo Cha kupiga siasa zaidi.
 
Apa kuna mkanganyiko na majukumu wa katibu wa ikulu ni yapi?
Neno Katibu lisinguangaishe; wewe angalia ni katibu gani. Kuna Katibu Myeka wa Rais, Katibu wa Ikulu, na kunaweza kuwa na katibu wa chochote kile, swali hapa ni kazi ya "Katibu Mkuu Kiongozi" anayepambanuliwa kwa kuwa Mkuu na pia Kiongozi.
 
Ndiye administrator mkuu wa ikulu anayesimamia mambo ya kiutawala kwa wafanyakazi wote wa Ikulu pamoja na wale walioteuliwa na rais. Kwa marekani anaitwa Chief of Staff.
Umechanganya bwana, siyo Katibu wa Ikulu! Huyu ndiye kiongozi mkuu wa Utumishi wa Uma kiserikali.

Pakiwa na uchaguzi huyu anaendelea kuongoza kawaida kwakuwa ni mtumishi. Huyu ni tofauti na katibu wa Ikulu au Katibu wa Rais
 
Apa kuna mkanganyiko na majukumu wa katibu wa ikulu ni yapi?
Katibu mkuu wa Ikulu majukumu yake ni usimamizi na utendaji wa shughuli za kila siku ofisi ya rais kiutalaamu zaidi yaani kwa kifupi huyu majukumu yake ni yale yale anayoyafanya katibu mkuu wa wizara yoyote Ile.

Kwa upande wa katibu mkuu kiongozi huyu ni mkuu wa makatibu wakuu wote akiwemo huyo huyo katibu mkuu Ikulu. Kiutendaji wa serikali ya Tanzania watumishi wote wa umma na taasisi za serikali wapo chini ya makatibu wakuu kulingana na taasisi husika ilipo ktk wizara. Hii humfanya katibu mkuu kiongozi kuwa mkuu wa watumishi wote wa umma pamoja na taasisi zake.

Kwa kifupi huyu katibu mkuu kiongozi ni sawa na waziri mkuu kabisa tofauti mmoja ni kiongozi wa kisiasa anachaguliwa na wananchi wa kawaida kupitia sanduku la kura ila huteuliwa na rais wadhifa huo kusimamia UTENDAJI wa shughuli za serikali ila kwa upande wa katibu mkuu kiongozi yeye ni MSIMAMIZI NA MTENDAJI wa shughuli za serikali kila siku na si mwasiasa huyu yeye yupo kitalaamu zaidi.
 
Na katibu ikulu?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…