Ni nini kazi ya Katibu Mkuu Kiongozi?

Umechanganya bwana, siyo Katibu wa Ikulu! Huyu ndiye kiongozi mkuu wa Utumishi wa Uma kiserikali.

Pakiwa na uchaguzi huyu anaendelea kuongoza kawaida kwakuwa ni mtumishi. Huyu ni tofauti na katibu wa Ikulu au Katibu wa Rais
Sikusema kuwa ni Katibu wa Ikulu, bali nimesema administrator wa Ikulu anayesimamia watumishi wote wa ikulu na wale wote walioteuliwa na rais; ni Chief of Staff wa Rais. Katibu wa Ikulu anafanya kazi chini yake kama walivyo makatibu wakuu wa wizara zote na walioko chini yao.
 
Mbona ombeni sefue hajapewa ubalozi?hayo huwa ni maamuzi ya rais mwenyewe
 
Ndio umejibu vyema na jk amekaa na makatibu wakuu viongozi wawili
 
Okay safi kiongozi; nilielewa vibaya-sorry!
 
Ndiye administrator mkuu wa ikulu anayesimamia mambo ya kiutawala kwa wafanyakazi wote wa Ikulu pamoja na wale walioteuliwa na rais. Kwa marekani anaitwa Chief of Staff.

Sio wafanyakazi wa Ikulu tu. Huyo ndiye mkuu wa civil service kwa upana wake wote!
 
Sio wafanyakazi wa Ikulu tu. Huyo ndiye mkuu wa civil service kwa upana wake wote!
Nilishafafanua swali hilo hapa
 
Ukitoka nafasi hiyo hupelekwi nje ya nchi tena na wala hupewi kazi nyingine yoyte ndani ya serikali kwani itakuwa ni kama demotion. Badala yake unastaafishwa kwa marupurupu mazuri sana, ingawa marehemu Timothy Opiyo na Paul Rupia hawakupata marupurupu hayo kwa vile sheria ilitoka wakati wao weshastaafu na haikuwa retroactive.
 

..mwenye majukumu uliyoyataja nadhani anaitwa Mnikulu.
 

Bado humjui vizuri Chief Secretary ni nani; usidhani anafanana na Chief of Staff wa White House. Civil Service yote iko chini ya Chief Secretary. Yeye yuko pale regardless ya nani ni Rais. Chief of Staff wa White House automatically anaondoka na Rais aliyemteua. Hana hata sekunde ya nyongeza!
 
Hii article (c) ndo hua inanichanganya. Nashindwa kumtofautisha na prime minister as all we know prime minister has mandate of give directions and instructions to any institution in the country the same applies to chief secretary.
Sasa mkuu, PM ana wizara na Vitengo vyake. Mfano TAMISEMI ishahamishiwa kwa Rais. Kuna wizara na Vitengo kibao haviko chini ya PM. Bali ni Rais na Katibu Mkuu Kiongozi ndio Final says.

Mkanganyiko unaupatia wapi labda?
 
Wadau je ni kwanini kwa hapa Tanzania katibu mkuu mara nyingi lazima awe na hadhi ya kibalozi? Hata dr Bashiru tayar ataitwa balozi maana kapewa hadhi hiyo
 
Hapa napata swali lingine...
Mbona kama hakuwa na ulinzi wa kumlinda kivileee.. maana kwa maelezo yako.. yeye ni mtu mwenye siri nyingi sana za nchi
Yaan hapo ni sawa unalinda computer kwa gharama kubwa kumbe doc. zote ziko kwenye flash na unatembea nayo kila siku lkn computer inalindwa na bunduki gate kali nk
 
Hii ya uteuzi wa Bashiru umeniibua. Hongera JPM. Kiongozi ni sifa junioni alizo nazo. Bashiru anazo. Maajabu aliyofanya ndani ya CCM yakadumishe yaliyo ndani ya serikali.

Apatikane mrithi atakaye vaa viatu vyake CCM.
Chama kisije kikarudi tena katika umahiri wa majungu na fitina.

Mh Jaffo tuongezee neno International kwenye stand ya mabasi ya JPM.
 
Katibu kiongozi ni sawa na chief of staff kwa vyeo vya ughaibuni.
 
Yaani ni kama Mungu na mwanae wa pekee, Yesu Kristo, ukaribu wa Mkuu wa nchi na Katibu Mkuu kiongozi. Sijui umeelewa? Maana tukikupa vifungu vya sheria ujue wajibu wa CS, hutajua vema. Umeelewa au bado umelewa?
Yesu n mtt wa bi mariham sio mung acha kutoa maneno ya kufuru
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…