Ni nyimbo zipi za Sugu zenye Ujumbe na zilizohit sana kuliko za Professor J?

Ni nyimbo zipi za Sugu zenye Ujumbe na zilizohit sana kuliko za Professor J?

Kwahiyo kumbe unamsifia kwa hayo na sio kazi yake kimuziki.


Nadhani hujasoma ukaelewa, muziki ndio umemtambulisha SUGU katika jamii. Na kukubarika huko kumemtengenezea njia ya kwenda Bungeni.
 
Umeanza kumsikiliza Sugu mwaka 2000. Basi jua kwamba 2proud alitoa album ya kwanza mwaka 1995 inaitwa ni mimi, 1997 akatoa album ya pili "ndani ya bongo", 1998 akatoa album ya tatu " niite mr II" na 1999 alitoa album ya nne "nje ya bongo". Wakati anatoa album zote hizo ulikua wapi?
Aisee wewe jamaa ni mnyama. Maelezo yako ni kweli kabisa. Ninazo kwenye tape album zote hizo. Ni Mimi inagongwa kwa redio One 1995 kwenye DJ show ndio nimetoka shule primary hiyo.
Wasiojua muziki ulikotoka ndio watakaouliza swali kama hili.
 
Habarini Wadau,

Kuanzia mwaka 2000 nilianza kumsikiliza Sugu au Mr II aliyekuwa akiitwa 2 proud zamani, ila kiukweli namtofautisha sana na Professor J katika kazi zao.

Mfano mzuri ni "Bongo Dar es salaam"

Nadiriki kusema nyimbo za Proffesor J zote ni nzuri, pia zipo zenye ujumbe na mashairi mazuri yenye Vina kuliko za Mr II.

Labda huu mpya wa "Freedom" japo pia chana yake na ujumbe sio bomba kiviile.

Mr II ni Mwanasiasa, Mwanaharakati na Mzalendo ila Kimziki naona kama anazidiwa sana na wasanii kama Proff J na Afande Sele.

Ni Mtazamo tu.
[emoji121]
MIKONONI MWA POLISI!

[emoji121] [emoji121] [emoji121]
 
Nadhani mtoa post hamujui 2 proud Bali anamjua sugu Tu, uliza wimbo unaitwa chini ya 18, siku nikianguka, mikononi kwa polisi, far dsm, deiwaka, nje ya bongo, wapi tunakwenda, unaweza kubeza kazi za ii proud au umezaliwa Na kumjua akiwa anaitwa sugu tayari?
Hawamjui 2Proud wanamjua Sugu,mzee wa mikononi mwa Polisi,bonge la goma
 
Aisee wewe jamaa ni mnyama. Maelezo yako ni kweli kabisa. Ninazo kwenye tape album site hizo. Ni Mimi inagongwa kwa redio One 1995 kwenye DJ show ndio nimetoka shule primary hiyo.
Wasiojua muziki ulikotoka ndio watakaouliza swali kama chili.
enzi hizo Radio one ndo kila kitu,Radio free nayo kwa mbaaaali,eti clouds hahah
 
Mleta thread naamini humjui vizuri Sugu, pengine sababu ya umri wako, nikipata muda nitakuwekea albamu zake zote hapa.

Kuhusu Prof Jay, sikiliza nyimbo zake zote yeye anasimulia hadithi na matukio.
2 proud alikuwa anaongelea hali halisi ya maisha,kama Mikononi mwa polisi,soo la kweli mbeya Day
 
Musics huwa unarekodiwa na tunaweza kuasses kazi za kila mmoja.

Kwahivyo kuwahi kumsikiliza sio tija ndio maana inawezekana wakati Bob Marley anatoa album ya kwanza wewe hukuwepo ila leo unaweza kujudge kazi zake.

Btw, nimeanza kumsikiliza tokea niko primary miaka ya 1997 ila nilikuja kumcompare na Prof. J miaka ya 2000 baada ya wote kufanya kazi kubwa.

Finally nikagundua kuwa Prof. J ni mkali zaidi.
Ukweli haujifichi japo sugu kaanza mziki kitambo zaid ya prof lkn ukiwakompea sugu haugusi moto wa prof.....prof mtu mwingne
 
Sugu haimbagi chochote kile cha maana zaidi tu ya kupata sifa kuwa eti ni rapper wa kwanza na mkongwe hapa Bongo na alichangia kuukuza mziki wa HipHop na rap.

Hamna kitu pale...Prof ndio Msanii Fundi.
umekula embe mbichi mkuu??
 
Back
Top Bottom