Ni nyimbo zipi za Sugu zenye Ujumbe na zilizohit sana kuliko za Professor J?

Ni nyimbo zipi za Sugu zenye Ujumbe na zilizohit sana kuliko za Professor J?

Sistaduu anapokugeuza wewe ndio dingi
Mapenzi kidogo mizinga mingi
Leo atataka versace na mini skirt
Kesho atataka passport
Keshokutwa atataka tiketi aende London au America
Si bora nifanye part japo sio pasaka
Sema unachoweza....!!

Fanya unachowezaaaaa...!

Mbona unashangaaaaa....!

Mambo ya fedhaaa...!!
 
Habarini Wadau,

Kuanzia mwaka 2000 nilianza kumsikiliza Sugu au Mr II aliyekuwa akiitwa 2 proud zamani, ila kiukweli namtofautisha sana na Professor J katika kazi zao.

Mfano mzuri ni "Bongo Dar es salaam"

Nadiriki kusema nyimbo za Proffesor J zote ni nzuri, pia zipo zenye ujumbe na mashairi mazuri yenye Vina kuliko za Mr II.

Labda huu mpya wa "Freedom" japo pia chana yake na ujumbe sio bomba kiviile.

Mr II ni Mwanasiasa, Mwanaharakati na Mzalendo ila Kimziki naona kama anazidiwa sana na wasanii kama Proff J na Afande Sele.

Ni Mtazamo tu.
Umeanza kumsikiliza Sugu mwaka 2000. Basi jua kwamba 2proud alitoa album ya kwanza mwaka 1995 inaitwa ni mimi, 1997 akatoa album ya pili "ndani ya bongo", 1998 akatoa album ya tatu " niite mr II" na 1999 alitoa album ya nne "nje ya bongo". Wakati anatoa album zote hizo ulikua wapi?
 
1.Mambo ya fedha
2.Chini ya 18
3. Hayakuwa Mapenzi

Huko mbele tutaomba kila mwanzisha uzi, ataje na Umri wake.
Hiyo ana miaka chini ya 18 ni khabari nyingine kabisa ukiisikiliza inazungumzia madhira wanayoyapata mabint zetu kwa ndoto zao za alinacha ni utunzi uliotulia ila sisi wabongo ni mabingwa wa kuponda.
 
Nimesikiliza zaidi ya Album 5 za Sugu, sijui kama kuna mbongofleva amefikisha hata nusu ya Album alizotoa jamaa. Mpe heshima yake huyu Legend, kufungua njia sio mchezo, hata hao unaowasifia wamejifunza mengi kwa Sugu na pengine wamekuwa inspired naye kuingia kwenye game. Ni kweli Profesa Jay ana ngoma kali zaidi, ila Sugu lazima apewe heshima yake aisee, kumconvice Mengi kuanza kucheza rap (nyimbo za kihuni) kwenye redio yake haikuwa jambo rahisi kwa wakati huo ila yeye aliweza. By the way Sugu na Profesa nawapa heshima sawa, Sugu alianza mbio then Prof Jay alikipokea kijiti na kukimbia kwa kasi zaidi
 
Umeanza kumsikiliza Sugu mwaka 2000. Basi jua kwamba 2proud alitoa album ya kwanza mwaka 1995 inaitwa ni mimi, 1997 akatoa album ya pili "ndani ya bongo", 1998 akatoa album ya tatu " niite mr II" na 1999 alitoa album ya nne "nje ya bongo". Wakati anatoa album zote hizo ulikua wapi?
Itakuwa alikuwa ananyonya, kaanza kusikiliza Album ya Deiwaka halafu anajidai anamjua Sugu
 
Back
Top Bottom