Ni Programming Language gani unaisoma sasa?

Sasa unamshauri nini haswa, maana yeye ni binadamu na sio mashini, lazima aanze kwa lugha moja kabla ya kutapatapa....
Na pia sio lazima ujue lugha tano ndio uwe competitive, kimsingi ili uwe competitive lazima ujue kutoa solutions zinazofanya kazi na kutatua matatizo kwenye jamii, haijalishi kama unajua lugha ishirini au tatu.
Vijana wengi hujaza majina ya lugha wanazozijua kwenye wasifu, lakini ukimhoji system ipi kakamilisha sehemu na inatumika na inasaidia kutatua matatizo, unakuta hana chochote cha maana cha kuonyesha.
So, muhimu kwa vijana kujifunza kutengeneza solutions, hapa namaanisha whole lifecycle ya software development, kuanzia kwenye feasibility, planning, kuja kwenye analysis, execution, tests, UAT mpaka project closure. Hii itamsaidia zaidi, sio kuhangaika kujaza lugha nyingi ambazo hata baadhi hatawahi kuzitumia.

Wakati naanza programming, nilijitesa kwa kukimbizana na lugha, nilizoma zaidi ya ishirini lakini mwisho najikuta hata nimesahau jinsi ya kufanya hello world kwenye asilimia kubwa ya hizo lugha. Yaani nimesahau kila kitu.
Solution ni basicof programming. Hilo ni la kawaida.
Lugha nyingi inakusaidia kuwa adaptive kwenye project mbali mbali kwa kutumia lugha tofauti.
Knowing si project zote utafanya kwa language moja.
 
Sio ushauri mzuri kumwambia mtu aanze kujifunza programming kwa kutapatapa kwenye lugha nyingi, anapaswa ajifunze moja na kujisindika kabisa, hiyo moja imfundishe principles muhimu za software development, kisha baada ya hapo ndio aanze kutafuna lugha zingine huko nje. Ni kama ilivyo kwenye lugha tunazoongea, lazima uifahamu lugha moja kwanza, hususan lugha ya mama, halafu hiyo moja itakupa muongozo wa kimaisha.
Sasa baadaye ndio uanze kujifunza lugha zingine za kukuwezesha kuongea na watu wasio wa lugha yako.

Kwenye programming uhitaji wa kujua lugha zingine mara nyingi hutokana na mahitaji unayokumbana nayo, mimi hapa kuna lugha nilijifunza kweye mradi ambao mteja alisisitiza ufanywe kwenye hiyo lugha, ila nilipokamilisha huo mradi, miaka imepita zaidi ya mitano sijapata mradi mwingine unaohusu kutumia hiyo lugha, na nimeishau wala hata sikumbuki chochote kuihusu, hata siwezi kuandika sentensi moja ndani yake ilhali niliwahi kukamilisha mradi tena mkubwa kwa kuitumia.

Ulimwengu wa programming ni mpana sana, ukiingia kichwa kichwa bila mkakati wowote utaangukia pua na kuchukia sana na kupoteza muda wako bure. Hapa nina uzoefu wa kama miaka kumi hivi kwenye programming lakini bado huwa najiona mchanga, bado najifunza na kutafiti kila siku, najihisi kama tone baharini...
 
Naunga mkono hoja hususani uliposema
"ukiingia kichwa kichwa bila mkakati wowote utaangukia pua na kuchukia sana na kupoteza muda wako bure"
Ni kweli kabisa kwamba unaweza kutumia nguvu nyingi na mda mwingi kujifunza language nyingi with no any focus.
Binafsi naona ni vyema kuchimba zaidi lugha moja. Then, ndipo ufikirie zingine kama kuna uhitaji.
 
Binafsi kwa sasa nazidi kujichimbia kwenye utaalam wa PHP, japo nina uzoefu wa miaka mingi kwenye kuitumia, ila nataka kufanya mtihani rasmi wa Zend Certified Engineer (ZCE), ni aina ya mtihani wa PHP ambao hauwezi ukafaulu bila uzoefu wa muda mrefu wa PHP. Wataalam wenye hiki cheti ni wchache sana

Kenya wako saba
Tanzania wawili tu
Uganda watatu
Rwanda mmoja
Sudan Kusini na Burundi hawana habari
Afrika Kusini wapo 117
Nigeria wako 39
 
Kijana naona unapambana na c++ sana.
Ni vizur.. lakin kqa experience yangu c++peke yake haitoshi.
And ulichoandika ni simple codes tu.
In real world ni more than that.
Atlest jifunze lugha 5 za programming ili uweze kuwa competitive kwenye ajira.

Si lazima kujifunza lugha 5. Kwenye programming ni vizuri kua very good in one or two kuliko kujua tano huku upo shallow kote. Diving deep into the language kujua ins and out ni muhimu sana, ila zaidi ya yote kujua programming yenyewe hapa naongelea Algorithms and Data Structures, kua na abstract thinking ni more important kuliiko hata language yenyewe. Kusema jua x number of languages haisaidii chochote.

Kwenye ajira inategemea unataka kuajiriwa kwenye kazi ipi, mfano web frontend developer, sitokaa niajiri mtu anayejua language 5 shallow huku kuna moja amemaster JavaScript in detail anajua vizuri how to build a frontend very quickly and efficiently.

Mleta mada anajaribu mengi sana kwa mpigo, angekomaa na moja kwanza amaster vizuri then ndiyo aanze nyingine. Kusoma languages mbili at the same time huku uko shallow huna experience na programming ni a total waste of time
 
Ndio nimeanza kujifunza chifu,hata hao wanaotengeneza application kubwa walianza kujifunza kwa level ya chini.kuna watu wamemaliza BSc in Comp Science hata kuandika mistari ya code kama hiyo hawawezi.Hapa nimesoma kidogo tu lakini nimetengeza kitu useful nikichimba zaidi nitafika mbali chief
Hii inakuwaje hii.
 
Binafsi kwa sasa nazidi kujichimbia kwenye utaalam wa PHP, japo nina uzoefu wa miaka mingi kwenye kuitumia, ila nataka kufanya mtihani rasmi wa Zend Certified Engineer (ZCE), ni aina ya mtihani wa PHP ambao hauwezi ukafaulu bila uzoefu wa muda mrefu wa PHP. Wataalam wenye hiki cheti ni wchache sana

Kenya wako saba
Tanzania wawili tu
Uganda watatu
Rwanda mmoja
Sudan Kusini na Burundi hawana habari
Afrika Kusini wapo 117
Nigeria wako 39
Naomba unisaidie majina ya hawa wabongo wawili. I need mentor on this sort of things brah!
 
Ndio nimeanza kujifunza chifu,hata hao wanaotengeneza application kubwa walianza kujifunza kwa level ya chini.kuna watu wamemaliza BSc in Comp Science hata kuandika mistari ya code kama hiyo hawawezi.Hapa nimesoma kidogo tu lakini nimetengeza kitu useful nikichimba zaidi nitafika mbali chief
Ndo mnavyodanganyana hivyo kuwa kuna graduates wa CS hawawezi kuandika simple code kama hiyo!
 
Binafsi kwa sasa nazidi kujichimbia kwenye utaalam wa PHP, japo nina uzoefu wa miaka mingi kwenye kuitumia, ila nataka kufanya mtihani rasmi wa Zend Certified Engineer (ZCE), ni aina ya mtihani wa PHP ambao hauwezi ukafaulu bila uzoefu wa muda mrefu wa PHP. Wataalam wenye hiki cheti ni wchache sana

Kenya wako saba
Tanzania wawili tu
Uganda watatu
Rwanda mmoja
Sudan Kusini na Burundi hawana habari
Afrika Kusini wapo 117
Nigeria wako 39
Nilijua hapo kwenye Tz lazima uweke 'tu'
Anyway Hongera
 
Hehehe!! Wacha kujishtukia, huku huwa hatupigi siasa, au ushindani wowote, ila huoni hapo kasoro kuwa karibia na idadi sawa na Rwanda ambao ni saizi ya kamkoa ilhali mpo milioni sitini.
 
Watakuwepo tu.Wengine hawajafanya mtihani bado,wengine wanakimbiza mwz kimyakimya 🤣 🤣.
 
Back
Top Bottom