Detective J
JF-Expert Member
- Oct 17, 2016
- 24,058
- 41,518
Solution ni basicof programming. Hilo ni la kawaida.Sasa unamshauri nini haswa, maana yeye ni binadamu na sio mashini, lazima aanze kwa lugha moja kabla ya kutapatapa....
Na pia sio lazima ujue lugha tano ndio uwe competitive, kimsingi ili uwe competitive lazima ujue kutoa solutions zinazofanya kazi na kutatua matatizo kwenye jamii, haijalishi kama unajua lugha ishirini au tatu.
Vijana wengi hujaza majina ya lugha wanazozijua kwenye wasifu, lakini ukimhoji system ipi kakamilisha sehemu na inatumika na inasaidia kutatua matatizo, unakuta hana chochote cha maana cha kuonyesha.
So, muhimu kwa vijana kujifunza kutengeneza solutions, hapa namaanisha whole lifecycle ya software development, kuanzia kwenye feasibility, planning, kuja kwenye analysis, execution, tests, UAT mpaka project closure. Hii itamsaidia zaidi, sio kuhangaika kujaza lugha nyingi ambazo hata baadhi hatawahi kuzitumia.
Wakati naanza programming, nilijitesa kwa kukimbizana na lugha, nilizoma zaidi ya ishirini lakini mwisho najikuta hata nimesahau jinsi ya kufanya hello world kwenye asilimia kubwa ya hizo lugha. Yaani nimesahau kila kitu.
Lugha nyingi inakusaidia kuwa adaptive kwenye project mbali mbali kwa kutumia lugha tofauti.
Knowing si project zote utafanya kwa language moja.