Ni Rais au Spika? Mmoja lazima achomoke

Rais kupingwa na Spika wa Bunge au kupingwa na Mawaziri wake kipi kibaya zaid?
 
Aking'olewa Spika kwa kigezo cha kumpinga Rais itakuwa msiba mkubwa kwa Demokrasia…Spika mpya atakuwa very submissive kwa Rais badala ya kufanya kazi ya kusimamia Serikali

'Mawazo hayapigwi rungu'-JK

Kama mtu kakukosoa wewe toa ufafanuzi Jamii ndio itamuona hamnazo na kizuri zaid mkosaji kaomba radhi hadharan itoshe
Mazingira ni tofauti kabisa bwashee!
 
Ndugai hajampinga Rais bali amepinga mikopo!
 
Naielewa hoja yako. Lakin kwa maoni yangu huyu bwana Kazi tangu nianze kumjua, hasa alipokalia kiti cha usipika niwe mkweri kichwani ni mtupu. Huyu hawezi simamia hoja nzito nzito kama watangulizi wake walivyofanya. Kama issues kadhaa zilienda mezani kwake akazizima. Ningemuunga mkono leo kama angesimamia zile issue wakati wa mwendazake.
Lakin kudhihirisha kuwa ni mtupu kichwani akaenda kuomba msamaha kwa kusingiziwa ameeditiwa.
Tuna sipika ambae hana analoliamini na kulisimamia
 
Spika ajae atakuwa Muoga kuliko Job Ndugai kama ndugai ataondolewa kwa kigezo cha kumkosoa Rais hiyo ndio hoja yangu

Kama Spika atang'olewa kwa 'kosa' la kumkosoa Rais tujiandae kuwa na Bunge dhaifu kuwahi kutokea Nchini
 
Hii ngoma wala haitafika asubuhi, kila kitu kitatulia na maisha ya Unafki yataendelea.
 
Kupingwa na mawaziri ndio mbaya zaidi kuliko kupingwa na spika.
Hadi sasa sijaona kosa la ndugai, ndugai hayupo bungeni kumpigia magogi raisi. Yupo kuisimamia serikali na kuiwajibisha
 
Spika ajae atakuwa Muoga kuliko Job Ndugai kama ndugai ataondolewa kwa kigezo cha kumkosoa Rais hiyo ndio hoja yangu

Kama Spika atang'olewa kwa 'kosa' la kumkosoa Rais tujiandae kuwa na Bunge dhaifu kuwahi kutokea Nchini
Hata hili ni dhaifu. Hoja yako ni kwamba tutakua tunatengeza bunge dhaifu zaidi. Hili la Ndugai ni dhaifu sana. Wana CCM sasa ndiyo wameelewa udhaifu wa bunge lao. Hawana wa kumsingizia ndani ya bunge lao. Uamuzi wowote kwenye hili sakata, ni aibu tupu kwa CCM.
 
Kupingwa na mawaziri ndio mbaya zaidi kuliko kupingwa na spika.
Hadi sasa sijaona kosa la ndugai, ndugai hayupo bungeni kumpigia magogi raisi. Yupo kuisimamia serikali na kuiwajibisha
Amewahi kuisimamia na kuiwajibisha?
 
Vyovyote iwavyo, kukopa trillion 10 ndani ya miezi 9 kwa ajili ya madawati ni jambo ambalo hatuwezi kulikubali, hili lazima liondoke na mtu!
 
Kwa uzi wako huu, liko wazi Mama Samia atakaa pembeni. Team Hayati JPM bado mizizi imetitia ndani mama hawezi ogopwa maana amechongwa na team Hayati JPM hivyo hakuna kurudi nyuma.
 
Kwa uzi wako huu, liko wazi Mama Samia atakaa pembeni. Team Hayati JPM bado mizizi imetitia ndani mama hawezi ogopwa maana amechongwa na team Hayati JPM hivyo hakuna kurudi nyuma.
Vivaaa!!! sukuma gang.
Japo Ndugai alitusaliti bwagamoyo port.
 
Vivaaa!!! sukuma gang.
Japo Ndugai alitusaliti bwagamoyo port.
Hawa ndio wenye nchi kwa sasa, hivyo hawatishikia kabisa muda mwingine saa mbovu husoma muda sahihi kabisa hivyo waliomtengeneza na kumfikisha hapo hawuogopi..
 
Tiba ya yote ni katiba mpya
Nionavyo hata hiyo katiba hajazaliwa wa kuisimamia, msimamizi wa watunga sheria mwenyewe anajificha juu ya meza japo anayo ulizi kikatiba.
Kuna shida kubwa nchi hii na sio ubovu wa katiba pekee
 
Spika ni mtu mdogo sana ukimlinganisha na Rais.. Kumbuka Rais ni Mwenyekiti wa CCM ambacho kwa jinsi kilivyo ni chama -dola.. Hivyo kumwondoa Rais kwa kura za Wabunge ni ndoto za mchana..
 
Hakumuomba radhi Rais specific. Yeye kawaomba radhi wananchi ki
jumla jumla.

Uombaji radhi wa aina ile ilitakiwa awe ameshamuona before kutoka in public.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…