sky soldier
JF-Expert Member
- Mar 30, 2020
- 5,407
- 19,264
Kiukweli paka ni wanyama wakatili sana, kuna paka hapa nyumbani huwa akikamata panya huko store inakuwaga ni mateso makali sana kwa panya.
Anachofanya anambeba panya kwa mdomo anamleta uwanja wa wazi anamwachia, hapo panya akianza kukimbia paka anamrukia anampiga makucha panya, anambeba upya kwa mdomo anamleta katikati ya uwanja anamwachia huku akijifanya kama vile hana muda naye.
Pindi panya akidhani kasemehewa anaanza kukimbia haraka lakini paka hamwachi afike mbali anamrukia anampiga makucha anambeba, yani ni hivyo hivyo mpaka panya anaishiwa matumaini kabisa anatulia tu kakubali yaishe ndio analiwa.
Ni mateso makali mno kwa panya, badala ya kuuliwa haraka anauliwa taratibu sana kwa maumivu makali sana kisaikolojia.