Ni sababu ipi ya paka kumtesa panya kwa kumchezea badala ya kumuua haraka?

Ni sababu ipi ya paka kumtesa panya kwa kumchezea badala ya kumuua haraka?

Wa kwangu kwenye sofa anakona yake anapenda kukaa, tumeweka kitambaa kwa ajili ya manyoya sasa ikitokea ukakaa kwenye hiyo kona yake atakutoa kwa kukusukuma na viguu vyake ukiwa mbishi atatishia kukung'ata ukiwa mbishi zaidi anasusa hatokaa tena hata umuite vipi haji, hadi hasira zake ziishe
Huyo ana bahati. Angekuwa wangu hivi sasa angeshakuwa marehemu
 
Paka ni CCTV ya [emoji89], usiulize sana, namaanisha, unaweza ukawa unamfuga paka ili akutunzie nyumba yako dhidi ya Panya na wadudu wengine, lakini paka ni kiumbe mmoja mwenye uwezo mkubwa sana kuliko binaadamu tumchukiliavyo, paka wana mawasiliano ya moja kwa moja na viumbe tofauti na Binaadamu paka wanamtumia kum trace binadamu.
Punguza ushirikina mkuu,una ushahidi wa hayo ?
 
Wa kwangu kwenye sofa anakona yake anapenda kukaa, tumeweka kitambaa kwa ajili ya manyoya sasa ikitokea ukakaa kwenye hiyo kona yake atakutoa kwa kukusukuma na viguu vyake ukiwa mbishi atatishia kukung'ata ukiwa mbishi zaidi anasusa hatokaa tena hata umuite vipi haji, hadi hasira zake ziishe
Mimi paka nawapenda Sana,nakumbuka mzee alikuwa paka wake ni Mimi na mazee mwenyewe tu ndio tulikuwa tunampenda lkn mabro walikuwa wanapiga mabuti kila siku hata bimkubwa naye alikuwa hamkubali akimfuata jikoni anamfukuza
 
nadhani kwenye kuwinda Panya ni jadi yao akimuona sidhani kama anaweza akamuacha,
Mimi hua naletewa ndege akifurahi, sijui hata anamuwinda saa ngapi lakini utashtukia miguuni kwako au mlangoni kamuweka.
Sijajua wa kwako ila hawa viumbe wakizoea vinono hawakamati panya na wakikamata hawamli wanamuua tu au wakila wanatapika

Nimefuga hawa viumbe nimeshuhudia haya nikajua ni peke angu wengi wanakutanaga na hilo hadi unashangaa dunia imekwisha nini paka hamamat panya
 
[emoji1][emoji1787][emoji1787][emoji1787]
Kuna sehem nilisoma wameandika

"Cats have been blamed for the global extinction of 33 species in the world"

Infact nawapenda sana hawa jamaa [emoji76][emoji76]
It's 63 not 33
 
Mimi paka nawapenda Sana,nakumbuka mzee alikuwa paka wake ni Mimi na mazee mwenyewe tu ndio tulikuwa tunampenda lkn mabro walikuwa wanapiga mabuti kila siku hata bimkubwa naye alikuwa hamkubali akimfuata jikoni anamfukuza
Mie mwenyewe naelewa sana nyau my best friends!
 
Vipanya vidogo hua vinafanyiwa hivyo, kuna mapanya mengine paka anakamata kwa mbinde...
 
nadhani kwenye kuwinda Panya ni jadi yao akimuona sidhani kama anaweza akamuacha,
Mimi hua naletewa ndege akifurahi, sijui hata anamuwinda saa ngapi lakini utashtukia miguuni kwako au mlangoni kamuweka.
Iko hivi, mbwa na panya huwa wanaamini binadamu ni wawindaji wabovu, hivyo tunaishi kwa kuwategemea wao.

Ndio maana akiua au akiona mzoga anakuletea ili na wewe upate mlo.
 
nadhani kwenye kuwinda Panya ni jadi yao akimuona sidhani kama anaweza akamuacha,
Mimi hua naletewa ndege akifurahi, sijui hata anamuwinda saa ngapi lakini utashtukia miguuni kwako au mlangoni kamuweka.
Anawawinda juu ya bati. Wale ndege wanaojenga pembeni mwa nyumba
 
Sijajua wa kwako ila hawa viumbe wakizoea vinono hawakamati panya na wakikamata hawamli wanamuua tu au wakila wanatapika

Nimefuga hawa viumbe nimeshuhudia haya nikajua ni peke angu wengi wanakutanaga na hilo hadi unashangaa dunia imekwisha nini paka hamamat panya
kwenye kukamata Panya na asimle nakubaliana na wewe ndio tunarudi pale pale kuwinda ni jadi yao labda huyo Panya awe mkubwa sana kuliko Paka hua wanaogopa,

kwenye kutapika ni sahihi kama umemzoesha chakula cha kupika ukimpa samaki/nyama mbichi lazima atapike na ashindwe kabisa kula.
 
Kiukweli paka ni wanyama wakatili sana, kuna paka hapa nyumbani huwa akikamata panya huko store inakuwaga ni mateso makali sana kwa panya.

Anachofanya anambeba panya kwa mdomo anamleta uwanja wa wazi anamwachia, hapo panya akianza kukimbia paka anamrukia anampiga makucha panya, anambeba upya kwa mdomo anamleta katikati ya uwanja anamwachia huku akijifanya kama vile hana muda naye.

Pindi panya akidhani kasemehewa anaanza kukimbia haraka lakini paka hamwachi afike mbali anamrukia anampiga makucha anambeba, yani ni hivyo hivyo mpaka panya anaishiwa matumaini kabisa anatulia tu kakubali yaishe ndio analiwa.

Ni mateso makali mno kwa panya, badala ya kuuliwa haraka anauliwa taratibu sana kwa maumivu makali sana kisaikolojia.
Hiyo ni ndio forplay kabla ya kumla.
Joking. Anaonyesha kwamba yupo na control ya kummiliki adui na adui hawezi kubadilisha hali hiyo.
Akimchokesha anamuua.
 
jamani hivi mnamdiss paka mmesahau vurugu za mshenzi panya?panya jmn ni mshenzi wa tabia kabisa ana makusudi mengi sana ya kuharibu mali za binadam na hata kusababisha hasara kubwa kama vile nyumba kuwaka moto baada ya kukata nyaya na kupelekea shot ya umeme,,mimi binafsi namkubali sana paka coz analeta utulivu ktk nyumba kwa wadudu km panya na vyengine vitambaavyo mijusi,tangu,ng'e nk
 
  • Thanks
Reactions: Cyb
Back
Top Bottom