Ni sahihi fundi kupiga picha kazi aliyopewa aifanye, na kuitumia kujitangaza bila makubaliano na mwenye kazi?

Ni sawa na unampeleka mwanao shule alafu kesho unakuta ameekwa kwenye bango la shule mitaani na mitandaoni Nchi zingine unaweza kushtaki.
 
Hakuna kitu unique mkuu labda ujazunguka kuangalia...
 
Diamond hakuwa sahihi kumkataza jamaa kujitangaza kuwa kamuuzia nguo yeye. Ila kusema kamvisha hapo kidogo ni tofauti na kusema kamuuzia, na especially kama nguo sio special order, huwezi jua kuwa alinunua pair moja kwako na pea moja kwingine na zote zinafanana.

Mtengeneza nguo anaweza kusema kamvisha ila sio muuza nguo.

Tukija kwa suala lako, kama hao jamaa wanaopost picha zako wanafanya hivyo kwa ajili ya kutangaza biashara, una haki ya kudai mapato kutoka katika faida zao maana umetumika kuwaingizia fedha
 
Hata kama sio sahihi huyo fundi akipiga ni sawa sawa na amepiga na asipopiga ni sawa na amepiga. Utamfanya nini.
 
Uwe unawapa maelezo before kuwa picha zako wasizipost

Nadhani mmeshindwana maelewano tuu
Mtu ukimwambia before hawezi kukupost

Mimi kwenye biashara yangu wateja wenyewe wakinunua bidhaa huwa wanapiga picha makwao wananitumia nawapost na wanajivunia kupostiwa kwenye page zetu
 
Hapo haifai yaani ni km mm nimenunua malaya nikamzagamua then nikamlipa.... Halafu baadae aje aweke mtandaon kujibrand mizagamuo anayotoa... Sio vzr coz yeye anapata faida wakati jamii itaniona mm km mcheza x
Hiyo ni biashara haramu

Acha kufananisha na biashara halali
 
Kukuweka wewe ukaonekana sura yako au taswira bila idhini yako si sahihi. Wabongo huwa tunajifanyia tu mambo kienyeji + uchawi + ukuda ndio mambo yanatuharibia. Kwa hili ulilolieleza ukienda kisheria anakulipa fidia
 
Inabidi umwambie bwana bwana ukizitumia picha zangu kibiashara hatutaelewana.
Betpawa wenyewe ukila hela zao kwa dau dogo picha zako ni halali yao kwa mwaka mzima. Sasa ukute nyumbani hawajui kama ni mjasiriamali au ulikuwa unawatukana wajasiriamali wenzako kumbe na wewe ni mwenzao.
 
Huu ndio tunaita uchawi
 
Kwani akipiga hilo paa picha anakuoiga na wewe? Ufundi ujuzi ni mali yake nyumba ndio mali yako, pengine na wewe umempata kupitia mitando baada ya kuona kazi zake.
Acha kuwa na roho ya kwanini wewe sio wa kwanza kuvaa suti au kujenga.
 
vipi alizitoa au aliacha?
 
Kisheria jibu ni hapana. Sema wabongo tumeishi kijingajinga, hatujui hata haki zetu. Kuna watu ninaona hapa wanatukana na kukejeli. Ukweli huruhusiwi kutumia hiyo kazi kujinadi bila ya idhini ya mwenye mali.

Naona kwa ujinga huohuo,wapo ambao huomba hata ramani ya jengo. Ubunifu na uchoraji ni fani za watu. Wanaishi kwa kazi hizo. Wewe kuipata kwa free ni sawa tu na sisi tunaepakua kazi za sanaa na kuzitumia bila kulipia. Hii tunafanya dhuluma.

Hatusemi usifanye,bali hakikisha unapata idhini ya mmiliki.
 
Kwani akipiga hilo paa picha anakuoiga na wewe? Ufundi ujuzi ni mali yake nyumba ndio mali yako, pengine na wewe umempata kupitia mitando baada ya kuona kazi zake.
Acha kuwa na roho ya kwanini wewe sio wa kwanza kuvaa suti au kujenga.
huo ufundi angeufanya sasa kwa hela yake ndio ajitangaze.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…