Ni sahihi fundi kupiga picha kazi aliyopewa aifanye, na kuitumia kujitangaza bila makubaliano na mwenye kazi?


Bila makubaliano sio sahihi.
Ni sahihi kwa kitu ambacho ni mali yako
 
huo ufundi angeufanya sasa kwa hela yake ndio ajitangaze.
Hii Mambo inaboa sana kwa ma MC wa shughuli aiseee

Mtu umeenda zako kwenye harusi
Umepiga zako masanga
Unaruka majoka kama yote

Afu asubuhi unakuta watu wanakutag instagram,
Kumbe mjinga MC kakupost instagram

Na wife home anakuwashia Moto coz ulienda kwenye harusi bila kuaga

Aiseee ma MC
Punguzeni huu ujinga
 
Hii sjui niiweke kundi la wenye chuki,wabinafsi au wivu kwa sababu hakuna shida yoyote kwa yeye kuipost popote pale
 
..hii nchi ina watu wa hovyo mno! na huyo ni mmoja wao hana akili hata 1
 
Hawa ndo wajinga kabisa yani wanatumia watu kujiongezea wafuasi...binafsi lazima aifute na fidia atanipa...sababu ata mm ninayo akaunti mtandaoni na sijipost y unipost wewe...??
 
Watanzania wengi hatujatofautiana roho mbaya na wale Polisi walioua huko Mtwara....unakuta yeye anafanya kila kitu kwa kuangalia mtandaoni ila cha kwake hataki watu wengine waangalie roho mbaya tu hiyo...
Ishu siyo kuangalia mtandaoni ila ni je ameongeza nn katika alichokiona ndo maana ya ubunifu...huyo fundi yeye kaongeza nn
 
Siyo kweli hizo ni janja janja zatulikotoka siyo tunakoenda cv ya picha ni huko nyuma lazima ujue hilo...fundi mjenzi lazima uwe umewahi kuona kazi yake au mtu wako wa karibu awe amemuona kinyozi pia na wengine pia...sasa kazi yako kuwepo kwenye picha haitoi uhakika wa ubora na uaminifu wako....ajue jinsi ya kubrand bidhaa yake ili apate imani na heshima toka kwa watu siyo kwa kutumia faragha za watu hivhiv mwisho ulaumu watu wana roho mbaya ni ujinga....
 
Kuchukuliwa video au picha bila ridhaa yako ni kosa kwa sheria ya cyber.
Privacy yako hapo imekuwa violated.
Hata hilo swala la fundi kufanya kazi na kupiga picha lazima aombe idhini kwako mwenye mali.
Ni vile wabongo hatuna tabia za kupeana mkataba hata kwenye kazi za ujenzi kama hizo. Kwenye mkataba unambana fundi kabisa
 
Sahihi kabisa kuna mtu anatetea huu ujinga anasahau ndo maana mitandao inatoa nafasi ya ww kumtag mtu nayeye kutoa ruhusa au kukataa wanakataa hizi kesi za hakimiliki na faragha za watu
 
Sioni shida,kwani hataji jina lako wala kuwa hapo ni wapi.Anazungumzia kazi yake tu
 
Hao ndio "Wachora Ramani".
Muda haupiti unaamia kwako, unaibiwa..
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…