Ni sahihi kumuacha Mkeo aparangane na biashara za masafa ya Mbali?

Wewe na mfano wako ndiyo mnawaza kumtawala mwanamke, ila sisi ambao tunajua stahiki na kuweka mambo mahala pake, tumamsimami mwanamke, tunamlinda,tunamtunza na kumpenda, ndiyo maana huwa tunapambana kuwakea mazingira salama wake zetu katika afya za akili zao, mali zao, heshima, na vizazi vyao.
 
Kitu maichokijua hakuna mwanamke rahisi kukusaliti kama huyo unayetaka awe tu nyumbani acheze uani hapo huyo ni rahisi kuchepuka kuliko anaechacharika maana mwili na akili vikiwa busy basi sijui hayo mawazo ya ngono atatowa wapi kama anajielewa
 
Kuna mtazamo wa watu wengi pia ukimuona mwanamke aliefanikiwa kushika noti na ana miradi yake mjini unahisi kahongwa hii naipinga wengine wanawake ni rael hustlers, mfano mzuri mama wa lori la wami kapambana hadi kufika pale sio kitu kidogo lazima muda mwingine wanawake tuishi nao kama marafiki zetu na tusiwachukulie kua viumbe dhaifu.
 
Ni ukweli pia uchumi wa familia nyingi siku hizi unajengwa na wanawake tukubali tukatae angalia mwanamke anaepambana kuanzia njombe kwenye kiazi au nyanya anaepiga safari za mtwara, angalia mwanamke wa tanga anaesafiri kufuata nazi mombasa kuja kuuza tanzania, angalia mwanamke mpambanaji anaechukua Dagaa wa tanga na kuwapeleka Congo lumbumbashi anatengeneza pesa huyo za kutosha hawa wote nawasifu na nasema haya kwa uzoefu wa kukutana na wanawake wapambanaji maeneo yote hivo natoa hoja nayoijua
 
Nimeshawishika kukupiga swali la nyongeza mkuu;

Katika shughuli za kusafiri naamini mwenza ametoa baraka zake na hilo ni jambo jema sana coz at the end of the day wote mnafanya kwa ajili ya welfare ya familia na hasa madogo.

Baada ya maelezo yangu, Je katika safari na shughuli hizo, unakutana na magumu gani ambayo kwa hakika kama ungekuwa home(mazingira ya home) ungeweza kuyakabili lakini ukashindwa?

Vipi kuhusu infidelity, unalizungumziaje hilo katika mazingira ambayo mwenza hayupo na hakika hayupo hata wa kuuliza nyendo zako?
 
Jurjani unafahamu kua hatma ya ndoa imeshikiliwa na mwanamke siku zote na usipomuongoza vizuri akiyumba hapo hata hiyo ndoa wala malezi bora ya watoto hayapo tena au haujui hatimiliki ya ndoa yako iko chini ya mwanamke
 
Unakosea sana Cariha, kusema "yeye ana uhuru wa kujiamulia maisha yake na kujitafutia kipato", that's very wrong na mindset za namna hiyo ndani ya ndoa ni sumu kali.

Ndani ya ndoa hatujiamulii, hatufanyi maamuzi ya mtu mmoja, tunakaa, tunazungumza na kufanya maamuzi kifamilia, iwe biashara, ujenzi, kusomesha/kusoma, watoto nk. Kama upo single, unajiamulia maisha yako, ukiwa kwenye taasisi hii nyeti kabisa hujiamulii, unakuja na wazo, mnashirikishana na kuamua as a family.

Take this with you and make sure you build a strong institution.
 
Wamama wengi wa kichaga ndio kazi zao za kusafiri mkoa kwa mkoa na ndoa bado zinadumu...
 
Wamama wengi wa kichaga ndio kazi zao za kusafiri mkoa kwa mkoa na ndoa bado zinadumu...
 
Wamama wengi wa kichaga ndio kazi zao za kusafiri mkoa kwa mkoa na ndoa bado zinadumu...

Muongoze mwanamke atimize yale anayohisi yatasaidia ustawi wa uchumi wa familia na sio kunyima uhuru wa kutenda yale anayoyaamini kwani ukimfanya mfungwa atakuja kukufanyia vituko hadi ushangae
 
mkuu mwanamke hata akiwa karibu vipi akiamua kuchepuka atachepuka tu...mtu anachepuka sababu ya tabia na maamuzi yake binafsi...mtu hachepuki sababu yupo free...mwanamke hata umuwekee ulinzi kiasi gani akiamua kukusaliti anakusaliti tu
Hapa nazungumzia kuchepuka kwa changamoto za kuwa mbali......Akiwa wa home kuchepuka kwake inakuwa kwa manati sana maana anahisi atajulikana na wambea ila akiwa huko NAMINYWIRI,NYAMISATI au KAZURAMIMBA Shambani huko anasaka mahindi au mpunga usiku akienda guest na jamaa hauwezi jua.
 
Kabisa Mkuu nina ushuhuda na hili, Mwanamke hatakiwi kucheza mbali na home! Na ndio maana mwanamke akitaka kuchepuka lazima atasingizia naenda kwa mjomba au naenda kusalimia njumbani nitakaa week hapo ndio atatumia huo mwanya kuchepuka otherwise akiwa home anahisi utamstukia.
 


πŸ˜ƒπŸ˜ƒπŸ˜ƒ! Sina Sana changamoto kwakweli! Kias kwamba niwaze ningekuwa home ningeweza kuitatua!
Kuhusu uaminifu mie nimeamua kujiamini tu mwenyew ....!nadhan coz am aged!


Alafu mie sidhani Kama nna vishawishi...mie kila kitu naonaga sawa tu hakuna wa kunitetemesha!
 

[emoji23][emoji23][emoji23][emoji23] I like u!
 
Jurjani uwe kiongozi kwa mke wako na sio kumsimamia utafika mbali sana amini
Huwezi kuwa kiongozi kiongozi bila kuwa msimamizi, sasa sijui kwanini hamjifunzi maana za maneno ? Kila msimamizi ni kiongozi mzee.
 
Jurjani unafahamu kua hatma ya ndoa imeshikiliwa na mwanamke siku zote na usipomuongoza vizuri akiyumba hapo hata hiyo ndoa wala malezi bora ya watoto hayapo tena au haujui hatimiliki ya ndoa yako iko chini ya mwanamke
Hata mwanamke anaweza kuomba talaka akiona mwanaume siyo msimamizi mzuri na ni muasi au mshirikina.

Na mama hawezi kuwa mlezi bora akiwa ni mtu wa kutoka toka hovyo, zaidi malezi ya mtoto yatakuwa yameshikiliwa na wasaidizi wa kazi, wasaidizi ambao leo yuko huyu mwezi ujao yuko yule, anacho fanya ni kuwa kazi yake ni kupokea mashitaka toka kwa dada wa kazi.

Hivi hujiulizi kama hii mifumo yenu ni bora zaidi na iliyo staarabika, kwanini zama hizi zimekuwa na mmomonyoko mkubwa wa maadili kuliko zama ambazo mnaziita za giza ? Au kisingizio chenu kuwa zama zimebadilika ? Ipa nitakwambia ya kuwa pia bibadamu ni wale wale na akili ni zile zile.

Ioa familia au ndoa inaundwa na vitu viwili vya msingi navyo ni asiki na mkataba (makubaliano ya kuridhiana baina ya pande mbili kimahusiano ya mapenzi chini ya sheria za kiroho zenye kutambulika). Kwahiyo ndoa au afya ya ndoa inashikiliwa na wote hao, si mwanamke pekee wala sisi pekee.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…